Dr. Wilibrod P. Slaa: Special Thread

Dr. Wilibrod P. Slaa: Special Thread

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
57,946
Reaction score
134,018
Habari Wakuu.Ninaleta kwenu Dr.W.P Slaa The Special Thread.Uzi huu una malengo makubwa mawili
  1. Kumshawishi Dr.Slaa aone umuhimu wa kuomba ridhaa ya kugombea urais kupitia UKAWA.Na vilevile kuwashawishi UKAWA waone busara ya kumptisha Dr.Slaa kupeperusha bendera ya UKAWA.
  2. Kuweka pamoja katika JF harakati za Dr.Slaa(kama atapitishwa) kuanzia kuchukua fomu,harakati zote za kipindi cha kampeni mpaka kusimikwa na kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
chadema8.jpg mchungaji3.jpg
Dr.W.P Slaa

th.jpg
Mama Maria Nyerere akimsihi jambo Dr.Slaa
Mambo 10 Kuhusu Dr.Wilbroad Slaa
1. Anachokisimamia

Dk Slaa anasimamia maadili, uadilifu, umakini na uwajubikaji katika uongozi wa nchi na utendaji serikalini.
Dk. Slaa anaamini kuwa Watanzania wanaweza kuleta mabadiliko wanayoyataka wakipata uongozi bora na thabiti.

2. Kuzaliwa, elimu ya msingi na sekondari

Dk. Slaa alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1948 katika Wilaya ya karatu. Alipata elimu ya msingi katika shule za Karatu na Kwermusi (Mbulu) kati ya mwaka 1958 na 1965. Alisoma elimu ya sekondari katika Shule za Dung'unyi Seminari na Itega Seminari kati ya mwaka 1966 na 1971.

3. Mafanikio ya DK. Slaa kielimu na Kitaaluma

Dk. Slaa ana shahada na atashahada zifuatazo.
Sharada ya Uzamivu (PhD) katika Sheria ya kanisa kutoka Chuo kikuu cha St. Urban, Rome.
Stashahada ya Theolojiaü kutoka Kipalapala Seminari.
Stashahada ya falsafa kutoka Kiboshoü Seminari.
Stashahada ya Afya ya Macho kutoka Kituo cha Kimataifa chaü Macho.


4. Mafanikio ya Dk . Slaa kikazi na kitaalamu

Dk. Slaa amefanya kazi katika maeneo na sehemu mbalimbali. Baadhi ya nyadhifa alizoshika na kazi alizofanya ni hizi zifuatazo:
Mkurugenzi Mtendaji, Chama chaü Wasioona Tanzania, 1992 – 1998
Katibu Mkuu, Baraza la Maaskofu Tanzaniaü (TEC), 1985 – 1991
Mkurugenzi wa Maendeleo (Jimbo Katoliki la Mbulu), 19977ü – 1979 na 1982 – 1985
Padri wa Kanisa Katoliki kuanzia 1977 hadiü 1991

5. Vitabu alivyoandika

Utimilifu wa Msichana (1977) na Utimilifu wa Mvulana (1977)
Expediency and Exigency Liturgical Legislationü (1981)

6. Ufasaha katika lugha nane (8)

Dk. Slaa anajua kuzungumza na kuandika lugha nane za kimataifa zifuatazo:
Kiswahili, Kiingereza, Kilatini, Kiitaliano, Kijerumani, Kihispania, Kireno na Kifaransa.

7. Uzoefu wa Dk. Slaa Kisiasa

Dk. Slaa ana uzoefu wa musa mrefu katika shughuli za kisiasa. Baadhi ya nyadhifa alizoshika ni hizi zifuatazo.

Mbunge wa karatu kwa miaka 15 kutoka 1995 hadi 2010

Katibu Mkuu wa CHADEMA, 2002 hadi sasa
Makamu Mwenyekiti Taifa wa CHADEMA, 1998 – 2002

Mjumbe wa Kamati Kuu na Baraza Kuu wa CHADEMA kutoka 1995 hadi sasa

8. Uzoefu wa Dk. Slaa KItaifa na Kimataifa

Dk. Slaa ana uzoefu mbalimbali kitaifa na kimataifa kama ifuatavyo.

Mjumbe w akuwakilisha Bunge la Tanzania katika Bunge la Afrika,Carribean na Pcific-FU (ACP-EUC Joint Assembly), 1996 – 2000.

Mjumbe kamati ya Uongozi (ACP-EU Joint Assembly)

Mjumbe katika Bunge la SADC kutoka 1998 hadi 2010

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge la SADC(Interü Parliamentary Cooperation and Capacity Building Committee) kutoka 1998 hadi 2010.

Nibu kiongozi wa kamati ya Upinzani Bungeni, 2006-2010

Mwenyekiti Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Bunge la Tanzania 2008-2010

9. Mafanikio kisiasa na kiutendaji

Dk. Slaa amekuwa mbunge wa karatu kwa miaka 15 mfululizo.
Karatu ni moja ya wilaya hapa nchini zenye maafanikio makubwa ikiwamo miundo mbinu bora, maji na huduma nyingine za kijamii, Dr. Slaa anataka kutumia uzoefu wake wa miaka 15 ya ubunge wa Karatu na uongozi madhubuti wa ukatibu mkuu CHADEMA, kwa ajili ya taifa zima.

Ndiye katibu Mkuu aliyefanikiwa zaidi kuijenga CHADEMA kwa kushirikiana na viongozi wengine ameweza kuipitisha CHADEMA katika changamoto mbalimbali na kukifanya kuwa chama kilicho tayari kushika uongozi wa taifa.

Bila kujali vitisho vya watawala aliibua rasmi kafsha za ufisadi mbaya kuliko zote zilizowahi kutokea hapa nchini zikihusisha wizi wa fedha za umma katika Benki kuu. Madai yake mazito Bungeni yalimlazimisha aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu nchini kutoroka nchini.

10.Zaidi ya yote Dr.Slaa anajua maisha ya watanzania wa kawaida na mateso yao ya kila siku


Kuhusu List of Shame
1. Dk Daudi Balali

2. Benjamin William Mkapa

3. Patrick W.R. Rutabanzibwa

4. Nimrod Elirehema Mkono

5. Andrew J. Chenge

6. Basil Pesambili Mramba

7. Grey S. Mgonja

8. Nazir Karamagi

9. Rostam Aziz

10. Edward Lowassa


11. Jakaya Mrisho Kikwete

Tutawakumbuka daima kwa jinsi Dk Slaa alivyotueleza tarehe 15/09/2007 jinsi kila mmoja wenu alivyosababisha leo hii nchi yetu ni maskini. Tunatamani mfe hata leo.

Karibuni


 
The Upcoming President Of Tanzania.
 
Mambo 9 Kuhusu Dr.Wilbroad Slaa

1. Anachokisimamia

Dk Slaa anasimamia maadili, uadilifu, umakini na uwajibikaji katika uongozi wa nchi na utendaji serikalini.

Dk. Slaa anaamini kuwa Watanzania wanaweza kuleta mabadiliko wanayoyataka wakipata uongozi bora na thabiti..

...Kwa mtizamo wangu dr.slaa hana maadili na sio muadilifu na haaminiki..angekuwa muadilifu na mwaminifu asingelisaliti kanisa katoliki.
 
Samahani naomba kuuliza kama BANDIKO lako lina baraka zote toka KURUGENZI YA HABARI ya CHADEMA?
 
excellent CV
CV YA ELIMU YA KAWAIDA YA KIDUNIA NA ELIMU INAYOMTAMBUA MWENYEZI MUNGU!
 
kwenye cv yake umesahau kuhasi kiapo cha mungu na cha upadre kutokuoa ​hadi kufa
 
Mleta mada,

Huna haja ya kuweka historia ya Dr Slaa upya humu JF. Sijui weweni mgeni ama vipi, lakini tayari historia ya Dr Slaa ipo humu kabla ya kushindwa kwake uchaguzi wa mwaka 2010.

Haya yote unayofanya hapa ni marudio tu. Na Membe leo amewachana LIVE kuwa hao wafalme wenu ndio wanafanya CCM ushinde kwa kishindo katika kila uchaguzi. Naona na wewe kwa akili zako ndogo unarudia yale yale.
Invisible...tafadhali unganisheni uzi huu na ile uzi ya kipindi kile ya Dr Slaa.
 
Last edited by a moderator:
Dr.Slaa ni lina atafunga ndoa na Josefin Mushumbusi? Nilimchangia mchango wa harusi yake mpaka leo haijafanyika,,,Kama harusi imemshinda aturudishie pesa zetu
 
Mambo 9 Kuhusu Dr.Wilbroad Slaa

1. Anachokisimamia

Dk Slaa anasimamia maadili, uadilifu, umakini na uwajibikaji katika uongozi wa nchi na utendaji serikalini.

Dk. Slaa anaamini kuwa Watanzania wanaweza kuleta mabadiliko wanayoyataka wakipata uongozi bora na thabiti..

...Kwa mtizamo wangu dr.slaa hana maadili na sio muadilifu na haaminiki..angekuwa muadilifu na mwaminifu asingelisaliti kanisa katoliki.
huo ni mtazamo wako
 
Back
Top Bottom