Dr. Wilbroad Slaa yuko wapi?

Dr. Wilbroad Slaa yuko wapi?

laki si pesa.

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2015
Posts
9,984
Reaction score
9,757
Wana jf.
Dr.Wilbroad Slaa, rais wa mioyo yetu toka uchaguzi mkuu ufanyike yuko kimya hatujasikia maoni yake. Yuko wapi rais wa mioyo yetu,? Yuko Tanzania au bado yuko mapumzikoni Marekani?
Dr. Slaa popote ulipo tunakuomba ujitokeze utoe maoni yako roho zetu zitulie.

==============================

Majibu ya Dr Slaa

===============================

Makamanda,

Alipo Dr Slaa hapako siri Wala hapajawahi kuwa Siri. Nilipowaaga Watanzania kupitia Azam TV na baadaye STarTV niliwaambia Watanzania kuwa ninaenda Sabbatical Leave.

Nitatumia wakati huo kurudi shule, kujikumbusha mambo mbali mbali mapya katika maeneo yangu ya Masomo. Mwanzoni nilifikiria kuanza na masomo ya Sheria.

Hata hivyo nimeanza na masomo ya Psychotherapy na Psychoanalysis. Kwa wale wanaojua Branches mbalimbali ya Falsafa ( Philosophia) watakumbuka kuwa nilisoma Psychology kama sehemu ya Masomo yangu ya Falsafa Seminari Kuu ya Kibosho.

Sasa nimeona niingie kwa undani zaidi, kufahamu zaidi Tabia na mfumo wa akili ya Binadamu unavyofanya Kazi. Hadi sasa nimekwisha kuingia kwenye Module insyodeal na Cognitive Therapy, Strategic Family Therapy, Brief Therapy.

Wapenzi wangu nawaomba watulie tu. Kama nilivyowaambia Nimeachana na Active Party Politics, walidhani maana ya kauli hiyo ni kufunga Mdomo.

Nilisema pale patakapohitaji kupiga kelele nitapiga kelele kupinga uonevu wa aina yeyote, kupinga ufisadi wa aina yeyote.

Nitasimamia misingi yote muhimu katika Taifa langu kwa kutumia haki zangu za Kikatiba ( ikiwa ni pamoja na kusimamia uchumi wa Taifa letu
.
 
Kuna tetesi ana mchumba mpya na atapewa ukuu wa wilaya kama kifuta machozi.
 
Huyo mzee watu walikuwa wakijinasibu rais wao wa moyoni lakini pesa imebadali hadi mioyo ya watu teh!
 
Wana jf.
Dr.Wilbroad Slaa, rais wa mioyo yetu toka uchaguzi mkuu ufanyike yuko kimya hatujasikia maoni yake. Yuko wapi rais wa mioyo yetu,? Yuko Tanzania au bado yuko mapumzikoni Marekani?
Dr. Slaa popote ulipo tunakuomba ujitokeze utoe maoni yako roho zetu zitulie.

Dr mihogo
 
Watu wenye jibu ni ama Bi Jose Mushumbuzi (mchumba wake) au Mzee Mwanakijiji (shosti wake). Nje ya hapo utaiona namba!
 
Bonyeza HAPA kuweza kujua yupo wapi
 
Na ukiambiwa yupo California Marekani utafanyaje? Asee jitahidi kutafta mambo yenye tija sio mambo ambayo hata ukiambiwa majibu hayatakusaidia kitu
 
Back
Top Bottom