Dr. W. Slaa for 2015 (Presidential election) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. W. Slaa for 2015 (Presidential election)

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Moseley, Sep 14, 2011.

 1. Moseley

  Moseley Senior Member

  #1
  Sep 14, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 184
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Ndugu zangu,
  kuna msemo unasema, "The future is for those who prepare for it today"..

  • Nchi inakwenda mrama
  • Maisha yanazidi kuwa magumu
  • Ufisadi unaongezeka
  • Tulisikia magamba yanavuliwa, lakini utafiti wangu unaonesha magamba yanavaliwa upya kwa kasi na ari mpya
  • Nidhamu serikalini haipo, uzalendo haupo, Utu hakuna.. Ubinafsi "A"
  • N.k

  Mimi kama Mtanzania, nisiyefungamana na Chama Chochote, napendekeza Dr. Slaa agombee tena uraisi 2015.. Maana naamini ni mtu anaefaa kuwa Rais wa nchi hii 2015. Ni mzalendo wa kweli katika nchi hii..

  Kwa sababu hiyo basi kwa sababu uchaguzi utafanyika mwaka 2015, Nimeona nianzishe thread hii kwa ajili ya kupanga mikakati ya kuhakikisha Dr. Slaa anaingia Ikulu mwaka 2015..

  2010 kulikua na lafu nyingi za chama tawala kwa kutokuwa na Tume huru ya Uchaguzi na uwepo wa katiba inayokipendelea zaidi chama tawala..

  Kwa hiyo naomba tuweke mikakati ya kuwang'oa CCM ikulu na tumweke Slaa Ikulu..
   
 2. h

  hoyce JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,119
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Naunga mkono hoja
   
 3. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Kwa maneno hayo kweli nimeona hufungamani na chama chochote
   
 4. Moseley

  Moseley Senior Member

  #4
  Sep 14, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 184
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Uwezo wako wa kufikiri unafahamika!
   
 5. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #5
  Sep 14, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hata uchaguzi uliopita alishinda akaiibiwa ushindi wake na wanaitafuna nchi hii na kundeleza umaskini mkubwa na mgao wa umeme wa kujitakia, Wakati tukimuombea afya njema na nguvu afike 2015 lazima iwepo mikakati mahususi ya kutoa elimu kwa wapiga jinsi ya kulinda kura zisiibiwe na jinsi ya kupambana na hao wezi kwani nao game watakuja na mbinu mpya za wizi lazima kuzifahamu na kuweka mikakati ya kukabiliana nazo
   
 6. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,112
  Trophy Points: 280
  we mwenye cirlcle cell, unamtania ndg yako.

  hata dr. Mabunduki anapenda pesa. Kuna tetesi alidai kulipwa sitahili kama za mbunge ili agombee uraisi kwa kuwa aliamini itakuwa ngumu kushinda na alijiandaa kushindwa uchaguzi ndo akadai alipwe vizuri kuwa katibu wa cdm kwani tayari atakuwa amepoteza ubunge wake karatu. Chadema walikubali na analipwa sawa na mbunge mpaka hivi leo.

  Mie nampendekeza zitto kwa kuwa bado ni kijana, na hawa akina slaa, watakuwa washauri wake wa karibu kabisa.
   
 7. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #7
  Sep 14, 2011
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Kwa Katiba hii ambayo watawala wanaing'ang'ania kwa jinsi inavyowapa mamlaka kama Mungu, Tume hii ya Uchaguzi, Polisi hii iliyofunzwa kuwanyenyekea CCM, JWTZ hii yenye Makamanda wa aina ya Lut. Jen Shimbo, na mfumo huu wa Utawala, labda Mungu amshushe Malaika kupambana na CCM.
  Kama hatutahakikisha tunapata Katiba mpya kabla ya uchaguzi 2015, CCM itaondoka na roho za Watanzania wengi , katu hawataachia madaraka kwa amani.
  TUHAKIKISHE TUNA KATIBA MPYA 2015
   
 8. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #8
  Sep 14, 2011
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Kuwa na katiba mpya ni jambo jema. Swali: je, itaheshimiwa? Kitu kimoja ni kuwa na katiba mpya, na kitu kingine ni kuiheshimu. CCM watakuwa tayari kuitii katiba hiyo? Sheria ngapi mpaka leo hata hizo zilizo kwenye katiba ya leo wanaendelea kuzivunja kwa ubabe? Katiba tu haitoshi, lazima kuwe na utashi wa kuitii. Na jinsi ccm ilivo haitaweza kuitii katiba yoyote inayoigharimu bila shinikizo. Na hapo ndo kutakuwa na kuumizana kwani ccm haitakuwa tayari kuachia madaraka. Ni mpaka tuchapane tu ndo tunaweza kujenga new order for our nation.
   
 9. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #9
  Sep 14, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  haya ni maoni yako tu ndugu. Chadema kama chama kina utaratibu wa kuchagua wagombea. Hata hivyo asante kwa maoni yako. Wakati ukifika usisahau kuleta maoni yako tena kama hutakuwa umeungana na mafisadi kuimalizia nchi......
   
Loading...