Dr. Ulimboka: Hali ya afya (Updates)

Atapona manake Mungu ni mwema!.....shetani daima yuko bize, lakini unapokuwa na imani hakuna kingine kitakachomzuia Mungu kufanya alichopanga!
 
Pole sana Kamanda, aluta kontinua!

Aisee kumbe hawa vijana wa Kova hawana huruma aisee, jamaa wamtesa sana aisee. Lilaaniwe jeshi zima la Polisi waendelee kupewa bajeti ndogo na bunge hasa katika makazi na mishahara ili waendelee kukaa ktk nyuma za kuku
 
Mwenyenzi MUNGU mwenye mamlaka Mbinguni na Duniani,fanya mwujiza na huyu Ndg yetu anyanyuke na kushuhudia kwa kinywa chake alichotendewa na hw majambazi wa serikali tawala dhaifu.

Nina Imani MUNGU mwenye uweza wa yote atatenda mwujiza.
 
Mungu ni Yeye yule jana leo na hata milele. Hashindwi kuonyesha muujiza wake, Dr. Ulimboka kupona nayo ni kazi yake. Mungu mjaliye na mpe kupona!
 
Asante kamanda Isack kwa kutuhabarisha kupitia picha safi sana na asante mungu, majaribu ya mungu ni mengi hata yesu aliuawa wakati alikuja kuwakomboa wanadamu
Mkuu tupac umenena yaliyo sahihi.Jina la Ulimboka litabaki kwenye historia ya nchi hii
 
Atapona tu! wameumbuka

Kwani wameumbuka kidogo? Mungu ndiye anayetupa na kuchukua uhai kwa sisi tunaoamini. Haya matishio mengine kama wengine hawatakufa hayana tija. Siamini kabisa katika kuteketeza maisha ya mtu au watu wengine....either kwa siasa, ujambazi, wivu au lolote lile!
 
Kesho anafanyiwa operation na nani?kwani si bado wamegoma?kama wamerudi kazini na mimi mgonjwa wangu niliyemrudisha nyumbani nimpeleke kesho akafanyiwe operation.

 
Wee unadhani hata kama wamegoma wao wenyewe wakigua hawatibiani wao kwa wao? au kama mwenzao kama hivyo kaugua hawamtibu? watamtibu tu ila serikali na jumii nyingine isiyo ya madaktari ndio imegomewa
 
Kesho anafanyiwa operation na nani?kwani si bado wamegoma?kama wamerudi kazini na mimi mgonjwa wangu niliyemrudisha nyumbani nimpeleke kesho akafanyiwe operation.

Hapana, nasikitika kusema mgonjwa wako wewe mpeleke India mpaka utakapojua kudai haki yako kwa vitendo. Ni wale tu waliojitolea kwaajili ya Tanzania bora ijayo (Wazalendo wa kweli) ndio wanatibiwa kwasasa. Mgomo uko pale pale!!
 
Get well soon, dr.& profesa wa ukweli, Uliii...mboka!!!

Kilicho dhaifu kwa Mungu ni dili, maana yeye hukiteua kilicho dhaifu ili kukiaibisha chenye nguvu, amen!
 
nimeiona hii picha ya dr ulimboka machozi yamenitoka. Mungu mwenye huruma na uwezo amponye haraka na awaumbue na kuwatia laana wale wote walioshiriki katika uchafu na uonevu huu na wale wote waliowatuma hao jamaa kufanya unyama huu. Hakika moto wa jehanamu na majuto ya milele vitakuwa juu yao milele.
 
Hakuna aliye mkuu zaidi ya mwenyezi mungu.

MUNGU AKUTANGULIE
 
Huko ikulu usalama watakuwa wanatoana roho wenyewe kwa kushindwa kutekeleza kazi

Hawa watu hakuna kitu wanachoweza kufanya wakafanikisha kwa ufasaha. Naamini kabisa ni Mungu anayewakwamisha mambo yao ndio maana hawafanikishi chochote. Wamefanya dili lakuiba twiga- mambo yamekuwa hadharani; wanaiba hela wanapeleka nje- hadharani, wanabadilisha rasilimali kwa suti- mambo hadharani, wamefanya dili za umeme wameshtukiwa, wamehonga wabunge (Jahiro saga) mambo yamekuja hadharani, wanahangaika kufungua kesi za wabunge wa upinzani (wananchi wameshtuka). Naomba Lema naye aweke wazi mazungumzo waliyofanya na Baba Mwanaasha mapema kabla wazushi hawajaanza conspiracy zao.
 
Mungu mwema akuponye haraka na akupunguzie maumivu atende muujiza wapeleke tu kokote hata the hague maana kwa kweli inauma sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…