Vmatongo
Senior Member
- Dec 8, 2021
- 156
- 237
Wengi tuliamini Sugu alikuwa hasikilizwi kwa sababu alikuwa anatoka upinzani, kumbe sio! Ile barabara kuu ya ajali nyingi za kutisha kutoka Mbeya kwenda Tunduma sie tuliamini sasa imepata mwarobaini ambaye ni Tulia Aksoni kumbe tulikosea sana, hamna kitu kabisa.
Hiyo barabara ndio haizungumzwi kabisa, bora Sugu alikuwa anaipigia kelele. Hvi nyie wabunge wa Mkoa wa Mbeya hasa nyie ambao mpo kando kando ya hiyo barabara eti mnaendesha matambiko ya kupunguza ajali wakati hiyo barabara ni nyembamba kupishana tu shida inataka ipanuliwe angalau njia nne, lakini mmekazana na waganga wa kienyeji!
Sisi wananchi tunamshangaa Tulia, ye ndio angekuwa mstari wa mbele kwenye hili kwa sababu wanasema ana nguvu serikalini sasa hata yeye ziiiii! Sasa tofauti yake na Sugu ipo wapi?
Mambo mengi Tulia pale Mbeya ni kama umeshindwa na ndio maana badala kupambana unakazania Marathon tu, maana ndio kitu unakijua zaid!
Sasa tumeshaamua jimbo halitagawanywa, utagombea hapo hapo Mbeya mjini ili tukufundishe adabu.