Dr. Tulia Ackson, nani amekutuma? Unataka nini? Kwanini?

Dr. Tulia Ackson, nani amekutuma? Unataka nini? Kwanini?

Naonza kuona Rais yangu anafanya Yale Yale kwahiyo mabadiliko hapa hakuna
 
Tatizo ni katiba chakavu inayokibeba chama tawala. Mihimili mikuu yote ya nchi inaongozwa na chama tawala. Demokrasia itatoka wapi kwa hali hii??
 
Kwani mkuu unafikiri watumishi wa umma hawana vyama? Akikosa nafasi ya kisiasa anarudi kwenye utendaji ambacho hakiruhusiwi ni kuonesha maslahi ya Chama kwenye utendaji basi.

Mkuu hapo unazunguka tu, ukweli ni kwamba mtumishi wa umma anaruhusiwa kujihusisha na maswala ya kisiasa wakati wowote ila awe "CCM"
 
Naweza kuamini kuwa sasa umeshaanza kunogewa na vyeo. Ulianza kuwa Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba. Ukafuata kuwa kiongozi wa Kamati ya Bunge Maalum la Katiba. Kama hiyo haitoshi, ukateuliwa kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Sasa unataka Uspika wa Bunge.

Ukiwa ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, hukupaswa kujitokeza kisiasa na kugombea Uspika wa Bunge. Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali si mtu mdogo. Ndiye Kaimu Mwanasheria Mkuu wa Serikali pale ambapo Bunge hufanyika kwakuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali huwa Bungeni Dodoma. Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni mtu wa kitaifa zaidi.

Kujianikaanika kama kada wa CCM si jambo jema wala vutizi. Kutakuwa na kitu na watu wanaosababisha. Nani kakutuma? Unataka nini hasa? Kwanini? Dr. Tulia, umejianika kama kada. Watumishi wa Ofisi yako na wananchi kwa ujumla watakuonaje ikiwa utaendelea kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali?

Ili kulinda heshima yako, jiuzulu Unaibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali na urejee Shule Kuu ya Sheria, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ukahadhiri pale ambapo Uspika utagoma kupatikana. Ujiuzulu haraka!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)

- Ninaamini kwamba ndiye the next Deputy Speaker, Ndugai ndiye Spika.

Le Mutuz
 
Haya sasa kelele hizi ziishe rasmi!.

attachment.php

Uteuzi huu ni salaam za rais , Dr.John Pombe Joseph Magufuli kwa wabunge wa CCM kuwa anamtaka nani awe spika mpya wa Bunge!.

Hongera sana Dr. Tulia kwa kuwa mbunge wa kwanza wa kuteuliwa na rais na Spika Mpya (in waiting) wa Bunge la 11 la JMT!.

Pasco
 
Asante sana mkuu maana watu badala ya kufanya uchambuzi wenye tija wanaleta mahaba kwenye issue za msingi.

Asante Dr Magufuli umejibu hoja kwa usahihi kwani kitendo cha kutengua uteuzi wake ktk nafasi ya unaibu AG bila shaka unaelewa nini maana ya utumishi

#HapaKaziTu.
 
sioni tatizo nadhani ni wakati wa wasomi kuingia kwenye siasa ili mambo yaende
 
Ccm vituko kweli.haiwezi kufanya maamuzi sahihi wao kama wao.wanasubiri mpaka upinzani uwakosoe.
 
Wewe wakati chama tawala walipotaka kupitisha ktiba ili itumike nyinyi haohao mkasema haraka yanini. Ngoja tufanye uchaguzi.hivyo mkaafiki kutumia katba ya zamani sasa mmeangukia pua mnazinduka mnataka katiba mpya. Hiyo ndio itapiga kura?mshinde?acheni mbwembwe. Badala ya kuuanza kujipanga.2020.mnajadiri uteuzi wa wabunge wa Ccm.mnapoteza muda wenzenu Ccm.wanapsnga saafu.2020.nyinyiwapinzani mnabwbwaja tu.uchaguzi umekwisha. Fanyeni kazi 2020.sio mbali.
 
Wadau mimi si mwanasheria au mtaalamu wa mambo ya kisheria, ila kuhusu hili la naibu mwanasheria mkuu wa serikali kuonyesha maslahi ya uchama na kuamua kugombea nafasi ya spika kupitia CCM. Je ni halali kwa nafasi yake kama mtu asiyetakiwa kufungamana na siasa wala makundi yeyote mbali na taaluma yake kuwa na mwelekeo huo? Au ni ule ule mkondo wa majaji nao kuwa watiifu kwa vyama vyao. Nawasilisha naomba msaada.
 
Kuwa mwanasheria mkuu hakuzuii mtu kuwa mwanachama wa chama cha siasa. Tukisema tumilike hayo mambo ya kadi za chama...wapo majaji wa kichaga wana kadi za CHADEMA. Hapo vipi sasa?
 
Ni Ibara/kifungu kipi cha Katiba hakimtaki AG/Naibu AG kufungamana na chama chochote?
 
Rais ameshatengua Cheo cha Unaibu mwanasheria na Amemteua kama mbunge na pia kupitishwa kuwa mgombea wa unaibu spika
 
Aah naona mnatetea uwozo sio sheria ipi inaruhusu mtumishi wa umma kushiriki kwenye siasa acheni kujitoa ufahamu
 
Kuwa mwanasheria mkuu hakuzuii mtu kuwa mwanachama wa chama cha siasa. Tukisema tumilike hayo mambo ya kadi za chama...wapo majaji wa kichaga wana kadi za CHADEMA. Hapo vipi sasa?

Sijambo zuri kwa mtumishi wa serikali kujionesha moja kwamoja bora angekaanayo tusijue
 
Kitu unazungumza.
Kwani CHADEMA inawateua kushika nyadhifa za kiserikali? Elewa mada. Elimu elimu elimu

Eti... elimi elimu elimu....... Mwenzenu alijua kuwa hamna ndio maana akaja nayo kuwasaidia watu wa aina yako. mnafikri wote tu akili kama zenu. Wenzenu tunayo. Tunajitambua tangu zamani.
 
Eti... elimi elimu elimu....... Mwenzenu alijua kuwa hamna ndio maana akaja nayo kuwasaidia watu wa aina yako. mnafikri wote tu akili kama zenu. Wenzenu tunayo. Tunajitambua tangu zamani.

na wew ulideki barabara kwani
maigizo ya kula kwa mama ntiliye ukubwani ndio elim au
 
Naweza kuamini kuwa sasa umeshaanza kunogewa na vyeo. Ulianza kuwa Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba. Ukafuata kuwa kiongozi wa Kamati ya Bunge Maalum la Katiba. Kama hiyo haitoshi, ukateuliwa kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Sasa unataka Uspika wa Bunge.

Ukiwa ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, hukupaswa kujitokeza kisiasa na kugombea Uspika wa Bunge. Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali si mtu mdogo. Ndiye Kaimu Mwanasheria Mkuu wa Serikali pale ambapo Bunge hufanyika kwakuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali huwa Bungeni Dodoma. Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni mtu wa kitaifa zaidi.

Kujianikaanika kama kada wa CCM si jambo jema wala vutizi. Kutakuwa na kitu na watu wanaosababisha. Nani kakutuma? Unataka nini hasa? Kwanini? Dr. Tulia, umejianika kama kada. Watumishi wa Ofisi yako na wananchi kwa ujumla watakuonaje ikiwa utaendelea kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali?

Ili kulinda heshima yako, jiuzulu Unaibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali na urejee Shule Kuu ya Sheria, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ukahadhiri pale ambapo Uspika utagoma kupatikana. Ujiuzulu haraka!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
Sasa hivi huishi kumsifia
 
Back
Top Bottom