Elections 2010 Dr. Slaa

werema01

Member
Feb 10, 2010
47
0
Tupe muongozo kiongozi, ila kuwa nje ya bunge naamini utaimarisha chama mpaka kila kona ya kila nchi
 
Swali lako jema lakini naona kuna mambo mhimu ya kutafakari kwa sasa kuliko hilo; uimara wa chadema sasa ni zaidi ya 51, wengine wanagawana, kikubwa ni jinsi gani ya kuweza kudhibiti wizi wa kura wa waziwazi ilhali kuna watu na bunduki/mabomu zinazonunuliwa kwa kodi zetu wakiwazuia raia wema kwenda kupiga kura
 
Swali lako jema lakini naona kuna mambo mhimu ya kutafakari kwa sasa kuliko hilo; uimara wa chadema sasa ni zaidi ya 51, wengine wanagawana, kikubwa ni jinsi gani ya kuweza kudhibiti wizi wa kura wa waziwazi ilhali kuna watu na bunduki/mabomu zinazonunuliwa kwa kodi zetu;
Kuna vingi vya kufanya lakini tusifumbie macho wizi huu wa kura kwani kuachwa kwake kutasababisha kuendelea kwa utamadani wa ubabe na kutojali wala kuheshimu matakwa na utashi wa Watanzania. Ni lazima tupambane kila nyanja bila kuogopa uhaini huu mkubwa.
 
Nimewapata wadau, nimekuwa nikiwaza hilo pia....... Ila nakumbuka tulisoma jukumu la ulinzi na usalama ni la kila raia...

Hapa naleta pointi kuwa ni vizuri chama kikajiimarisha kila kona ya nchi na kuweka wazalendo watakaosimamia wakati wa uchaguzi bila woga wowote.... Rasilimali yetu ni watanzania wenye nia ya kweli ya mabadiliko.... Mapinduzi ya kifikra ni silaha kubwa hapa.

Mfano majimbo tuliochukuwa ni uimara wa waliosimama pamoja na wananchi kulinda haki yao, solidarity must be there forever
 
Ni muhimu sana kwa CHADEMA kuwatumia wale wabunge wailopata yale majimbo tunayoyaita HOT-CAKE kama vile Ubungo, Kawe, Arusha, Mbeya, Moshi na yale ya mwanza ili utendaji wao uwe ni mfano kwa wale waliochagua kutoipigia kura CHADEMA au kutokupigakura kabisa (kwa sababu ya kutokuwaamini au kutokujua) ili next-time wajue kuwa kupanga ni kuchagua na chama makini kweli ni CHADEMA.

Pia kwa wale ambao hatujajiingiza kwenye wajibu wa chama mojakwamoja kwa sababu ya muda na mambo mengine basi tutumie busara zetu kuwaelimisha watanzania wenzetu katika kipindi cha miaka mitano mpaka 2015 ili waweze kupiga kura (wasisuse) kama walivyo fanya sasa. Hii itasaidia pale ambao ukiwa na petroli ya lita elfu kumi ukataka kuichachua kwa mafuta ya taa ya lika elfu moja au mbili basi inakuwa ni ngumu kitu ambacho hakitoleta matunda yaliyokusudiwa kwa wale waizi wa kura!.
 
Kama nilivyosema kuna vingi vya kufanya ikiwa ni pamoja na kuanzisha redio na TV si kwa ajili ya propaganda bali kutoa nafasi ya Chadema kutoa sera tofauti na zinazofaa kuongoza nchi yetu na kuwaelimisha Watanzania wenzetu. Vilevile lazima kuangalia uchaguzi wa wenyeviti wa vijiji ambao hauko mbali sana. Ni lazima kuzitwaa serikali hizo pia.
 
Kuna vingi vya kufanya lakini tusifumbie macho wizi huu wa kura kwani kuachwa kwake kutasababisha kuendelea kwa utamadani wa ubabe na kutojali wala kuheshimu matakwa na utashi wa Watanzania. Ni lazima tupambane kila nyanja bila kuogopa uhaini huu mkubwa.

usihofu wana maombi tupo, kama kikwete ameingia kwa wizi madarakani basi hatamaliza huu mwaka. mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni
 
Back
Top Bottom