Dr. Slaa ziarani Manyara

Dr. Slaa ziarani Manyara

safi kabisa dr. hakika ziara yako umepanga kisomi na kisayansi zaidi ila pia kama kuna uwezekano kuna maeneo ya upareni,tanga,monduli,maeneo mengine ambayo kirusi ccm bado inawaua wananchi tunaomba ufike na kupanda mbegu zitakazostawi katika fikra pevu
 
Jamani mbona kila siku hukohuko tu....? Kanda ya kusini RUVUMA,LINDI NA MTWARA vipi? Hata kanda haijazinduliwa,maandalizi ni kama yanasuasua.....Makao makuu CHADEMA itambue kwamba kanda ya kusini inakabiliwa na uchumi duni,haina mbunge hata mmoja,ni kama yatima kwa jinsi ilivyo,watu wake wapo yatari kwa mabadiliko......Naomba makao makuu waibebe hii kanda na ikibidi walezi wake wawe ni mwenyekiti na katibu mkuu,inaweza kuleta maajabu kama itabebwa vizuri...Ikumbukwe pia Histiria ya ukombozi wa Tanzania dhidi ya wakoroni hawezi kukamilika bila kuitaja kanda hii kupitia MAJIMAJI WAR.....Vivyohivyo ukombozi wa nchi yetu mara ya pili hautakamilika tukiitenga kanda hii.
 
duh maneno mazito aya jamani, nafikili ni muhimu kwa chadema kuizindua ii kanda as soon as possible pia kujipanga namna nzuri ya kwenda kueneza elimu ya uraia kwa wakazi wa huko ambao sio siri wamekuwa wakidanganywa na mafisad pia watawala dharim wa ccm miaka yote ilopita
 
Ziara hii inanikumbusha jinsi alivyompiga kibuti Rose Kamili jukwaani alipodai hakuwa mkewe. Chezea Dr Kanjanja wewe.

unaona yale yale ya uelewa mdogo, maccm badala ya kujadili issues za namna ya kuwasaidia watu walogubikwa umaskini wa kutisha ulosababishwa na utawala dhalimu wa ccm, wao wanakimbilia kumjadili mtu.

wao wanamsema dr slaa na chadema wkt sisi tnajadili mwarobaini pia jinsi ya kuwakomboa iwapo tutapewa ridhaa ya uongozi, jaman ccm kweli 2015 kitakuwa kimeoza kikinuka kwan kina kina dalili kuwa kinakufa kwa sasa
 
Kila la heri dr slaa,mwenyezi Mungu akutangulie kwa kila hatua,ufanikiwe katika ziara yako uwe na afya teeeele!MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI CHADEMA.na iwe ivyo.
 
Kama Dr. Slaa anaenda manyara. Ina maana uvumi ulioenezwa hapa Arusha kuwa atazindua kampeni kimandolu ni wa uwongo?
 
Tuendelee kupiga kampeni za vijana kuwa na uzalendo wa kupiga kura pindi chaguzi zinapofika otherwise ushabiki huu wa kijinga 2015 tunaweza kuambulia patupuuu tenaaa
 
Dk Nakuonea wivu unavyopendwa. Mungu akubariki sana, akupe nguvu na kukuzidishia afya tele. Kazi unayoifanya ni kubwa sana.
Single party system was not a circumstantial necessity as declared by TANU and CCM leaders, it was a fear of opposition of the first president. Naamini sintakufa kabla sijaiona CCM nje ya ikulu, kama KANU na UNIP na Kaburu.
 
Dr.Slaa, ndiye rais wa mioyo ya Watanzania; Nawatakia kila la kheri makamanda.

Mungu wabariki viongozi wa CHADEMA,
Mungu wabariki Makamanda,
Mungu Mbariki Dr. Slaa.
 
Kila la heri dr slaa,mwenyezi Mungu akutangulie kwa kila hatua,ufanikiwe katika ziara yako uwe na afya teeeele!MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI CHADEMA.na iwe ivyo.

Mungu atasikia kilio chako
 
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willbroad Slaa, anatarajiwa kuanza ziara ya ujenzi na kukagua uhai wa chama katika maeneo mbalimbali ya wilaya za Mkoa wa Manyara,siku ya Jumamosi, tarehe 18-26, Mei 2013

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu Dkt. Slaa ataambatana na watendaji wa Makao Makuu ya CHADEMA pamoja na wabunge wote wa CHADEMA Mkoa wa Manyara. Akiwa katika ziara hiyo, mbali ya kupokea taarifa na kukagua uhai na ujenzi wa chama katika maeneo atakayopita, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atafanya mikutano ya hadhara takriban miwili kwa kila siku pamoja na mikutano ya kikazi ya ndani, ambapo atakutana na wanachama na viongozi wa maeneo husika.

Ratiba ya ziara hiyo itakuwa kama ifuatavyo:

Atawasili Babati Mjini 18/5/2013 asubuhi; ambapo kutakuwa na mapokezi na kisha salamu kwa wananchi eneo la Minjingu, baadae atakuwa na mkutano wa hadhara saa 9 mchana viwanja vya Kwaraa, Babati mjini. Akiwa njiani kuelekea Hanang, tarehe 19/5/ 2013, Katibu Mkuu atapita na kuwasalimia wananchi wa maeneo ya vijiji vya Masqaloda, Measkron, Nangwa na Dirma, kabla ya kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo ya Balangida na Gendabi (Hanang). Tarehe 20/5/2013, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atafanya mikutano ya hadhara Basutu (Hanang) na Hydom(Mbulu)

Siku ya tarehe 21/5/ 2013, Katibu Mkuu wa CHADEMA atakuwa na mkutano wa hadhara Dongobesh na Mbulu Mjini. Tarehe 22/5/2013 akiwa njiani kuelekea Babati Vijijini, Katibu Mkuu atawasalimia wananchi wa vijiji vya Mutuka na Mwikansi kabla ya kufanya mkutano wa hadhara Galapo Babati vijijini kuanzia saa 8 mchana.

Siku ya tarehe 23/5/ 2013, Katibu Mkuu atakuwa na mikutano ya hadhara maeneo ya Riroda, Dareda na Bashnet, Babati Vijijini. Tarehe 24/5/2013, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atakuwa Simanjiro na atafanya mikutano ya hadhara katika maeneo ya Musitu wa Tembo, Ngorika na Ngage.

Siku inayofuata, tarehe 25/5/2013, Katibu Mkuu atakuwa na mikutano ya hadhara katika maeneo ya Orkesimet, Namaruru kisha atamalizia kwa kufanya mkutano mkubwa Mererani kuanzia saa 10 jioni.

Imetolewa leo, Mei 17,2013 na;

Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa CHADEMA.

mkuu molemo hii inanikumbusha ahadi ya dr.slaa 2010 wakati wao wanachakachua kwenda ikulu yeye atapeleka elimu ya uraia vijiji vyote na sasa anaendelea kutimiza ahadi kwa vitendo.nimatumaini yangu akimaliza manyara atapita arusha kuongeza nguvu
viva dr.slaa viva cdm
 
Mtwara na Lindi,
Asanteni kwa kilio. Kwa bahati mbaya nadhani taarifa hazikuwa zimewafikia. kanda ya Kusini ambayo inahusisha mikoa ya Mtwara, Lindi, na Ruvuma inazinduliwa rasmi tarehe 25 na 26 May, 2013. Tuliwajulisha kuwa hakuna eneo litabaki bila kufikiwa. Hivyo, pamoja na kilio chenu nadhani kitajibiwa walifika wataalamu wetu wa kuunda Kanda wakiongozwa na Mhe. mwenyekiti wa Taifa, Mhe. Freeman Mbowe(mb), Kiongozi wa Kanbi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mhe. benson Kigaila Mkurugenzi wa Organizesheni wa Chama.

Tukishikamana ukombozi hautakuwa mbali. Utekelezaji huu wa Kanda, unaendana na Kilio cha Wananchi wa Mtwara na Lindi kuhusiana na maswala ya Gesi. Kila Kanda na kila eneo uwezekaji ni lazima uhusishe wananchi. Nawaunga mono wananchi wa Mtwara na Lindi kwa kusimama kidete kuhusiana na Rasilimali za Taifa zilizoko kwenye maeneo yetu. Kila eneo likifanya hivyo ukombozi wa kiuchumi wa Taifa hili utakuwa umekamilika, kwani wahusika, wenye uchungu na rasilimali zetu watazisimamia.

Jamani mbona kila siku hukohuko tu....? Kanda ya kusini RUVUMA,LINDI NA MTWARA vipi? Hata kanda haijazinduliwa,maandalizi ni kama yanasuasua.....Makao makuu CHADEMA itambue kwamba kanda ya kusini inakabiliwa na uchumi duni,haina mbunge hata mmoja,ni kama yatima kwa jinsi ilivyo,watu wake wapo yatari kwa mabadiliko......Naomba makao makuu waibebe hii kanda na ikibidi walezi wake wawe ni mwenyekiti na katibu mkuu,inaweza kuleta maajabu kama itabebwa vizuri...Ikumbukwe pia Histiria ya ukombozi wa Tanzania dhidi ya wakoroni hawezi kukamilika bila kuitaja kanda hii kupitia MAJIMAJI WAR.....Vivyohivyo ukombozi wa nchi yetu mara ya pili hautakamilika tukiitenga kanda hii.
 
Mtwara na Lindi,
Asanteni kwa kilio. Kwa bahati mbaya nadhani taarifa hazikuwa zimewafikia. kanda ya Kusini ambayo inahusisha mikoa ya Mtwara, Lindi, na Ruvuma inazinduliwa rasmi tarehe 25 na 26 May, 2013. Tuliwajulisha kuwa hakuna eneo litabaki bila kufikiwa. Hivyo, pamoja na kilio chenu nadhani kitajibiwa walifika wataalamu wetu wa kuunda Kanda wakiongozwa na Mhe. mwenyekiti wa Taifa, Mhe. Freeman Mbowe(mb), Kiongozi wa Kanbi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mhe. benson Kigaila Mkurugenzi wa Organizesheni wa Chama.

Tukishikamana ukombozi hautakuwa mbali. Utekelezaji huu wa Kanda, unaendana na Kilio cha Wananchi wa Mtwara na Lindi kuhusiana na maswala ya Gesi. Kila Kanda na kila eneo uwezekaji ni lazima uhusishe wananchi. Nawaunga mono wananchi wa Mtwara na Lindi kwa kusimama kidete kuhusiana na Rasilimali za Taifa zilizoko kwenye maeneo yetu. Kila eneo likifanya hivyo ukombozi wa kiuchumi wa Taifa hili utakuwa umekamilika, kwani wahusika, wenye uchungu na rasilimali zetu watazisimamia.

Thanks Dr.for updates.
 
Dr Slaa tukumbuke na sisi Wanyisanzu na Wanyiramba wa Iramba Mashariki. Nimefanya kadri yaliyo ndani ya uwezo wangu kuimarisha chama Iramba mashariki ila wananchi wanahitaji na huduma yako wewe pia. Ujio wako utaleta hamasa na uamusho sana. Please put us into your calendar.
 
Kanda Lisu anatosha......Wenzio hatuna hata wa dawa,ndo maana tunapeleka ombi maarumu.....
 
Mtwara na Lindi,
Asanteni kwa kilio. Kwa bahati mbaya nadhani taarifa hazikuwa zimewafikia. kanda ya Kusini ambayo inahusisha mikoa ya Mtwara, Lindi, na Ruvuma inazinduliwa rasmi tarehe 25 na 26 May, 2013. Tuliwajulisha kuwa hakuna eneo litabaki bila kufikiwa. Hivyo, pamoja na kilio chenu nadhani kitajibiwa walifika wataalamu wetu wa kuunda Kanda wakiongozwa na Mhe. mwenyekiti wa Taifa, Mhe. Freeman Mbowe(mb), Kiongozi wa Kanbi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mhe. benson Kigaila Mkurugenzi wa Organizesheni wa Chama.

Tukishikamana ukombozi hautakuwa mbali. Utekelezaji huu wa Kanda, unaendana na Kilio cha Wananchi wa Mtwara na Lindi kuhusiana na maswala ya Gesi. Kila Kanda na kila eneo uwezekaji ni lazima uhusishe wananchi. Nawaunga mono wananchi wa Mtwara na Lindi kwa kusimama kidete kuhusiana na Rasilimali za Taifa zilizoko kwenye maeneo yetu. Kila eneo likifanya hivyo ukombozi wa kiuchumi wa Taifa hili utakuwa umekamilika, kwani wahusika, wenye uchungu na rasilimali zetu watazisimamia.

Asante Dr kwa updates.....Lkn ombi langu la kuwa mlezi wa kanda hii hujlisemea......
 
Back
Top Bottom