Dr. Slaa uso kwa uso na Zitto kwenye Mdahalo tarehe 18 June!

Usifikiri Kuitwa Dr kwa mapadri wa kanisa katoliki ni kusoma maandiko tu.. those dudes are packed with stuff... tough shyt!! dont miss the debate..
 
Umri haumruhusu hivyo hata kama ana aspire ni irrelevant kwa uchaguzi wa Mwaka huu.

Mufuruki kakurupuka.

It is just an aspiration. . . . .Yeye kateua hao labda tungehoji vigezo vyake lakini si kusema Zitto hafai kuwa katika huo mdahalo. . . .

Hebu niambie hasara au athari zitazotokea iwapo Zitto atashiriki
 
Usifikiri Kuitwa Dr kwa mapadri wa kanisa katoliki ni kusoma maandiko tu.. those dudes are packed with stuff... tough shyt!! dont miss the debate..

Ni Ph.D ya nini mkuu??!!
Hiyo ni level ya super specialization. . . ., . . So alichosoma ndio anachokijua zaid hili wala halihitaji mjadala mreeeefu weka mapenzi kando ona ukweli
 
Huyu mtoa mada nae ni chizi tu!

ZK ana masters ya uchumi iliyo jaa Politics and not reality!! Kuna wasomi wengi tu na Masters na PhD za uchumi ila hawatumiki ipasavyo!

Ebu weka hoja hapa za kiuchumi alizo isaidia serikali ya CCM kuondokana na wizi, umasikini, maradhi, ufinyu wa kufikiri, nk.

Huyu ZK alishiriki ktk kamati ya Madini, hakurudi na jipya (ni mchumi tumbo tu).

Una chuki na zito,
hukumbuki hata sheria mpya madini kwamba ni matunda ya kamati hiyo?
 
Ruttashobolwa

MADA ITAKUWA NI NINI?
Muhimu sio kukutanisha Zitto,Lipumba na Slaa,
cha Muhimu ni nini wanaenda kujadili?,kwani Slaa ni Mchumi?,wanaenda kujadili mageuzi,mustakabali wa Nchi yetu,au sera zao au nini?wote ni Vyama vya Upinzani...Au ni mdahalo wa Jumla/Mi sijaelewa kabisa hapo...Au kila Mtu ataeleza sera za chama chake?
Maanake Mtoa mada alivyoibua hii hoja utadhani wanaenda kutafuta nani Mshindi au kusutana...hivyo watu tukae Mkao wa kula...

kumbe umeona mkuu,alafu kama lengo lake anataka dr slaa aibike hv
 
Last edited by a moderator:
Ndiyo maana wanaCCM walimkimbia.Labda walimjua. Walimshtukia kuwa Mufuruki hana ajenda nyingine zaidi ya uchonganishi na kuwa na dalili zote za kutumika. Makada wa CCM waliotangaza nia na kuchukua fomu za kugombea Urais kupitia CCM wanamshtukia na kumkimbia. Wakati ule alitenda kosa la kuwabadilishia ratiba ghafla wahusika na hivyo wengi wakashindwa kujitokeza.

Tena, Mufuruki anafanya kosa lingine kuelekea kwenye Mdahalo ulioandaliwa na Taasisi yake hapo tarehe 18/6/2015. Anaalika hata wasiohusika. Amemwalika Dr. Emmanuel Makaidi na Zitto Kabwe. Hawa wote si wagombea Urais watarajiwa. Wote hawa wasatangaza kugombea Ubunge : Dr. Makaidi atagombea Masasi na Zitto ni Kigoma Mjini. Halafu, Zitto hata akitaka kugombea Urais hawezi kwa mwaka huu. Hana na hatakuwa na miaka 40 itakiwayo kikatiba.

Waalikwa waliobaki ni sahihi. Prof. Lipumba ameshatangaza kugombea. Dr. Slaa anatajwatajwa nawanaCHADEMA. Angalau. Ameachwa wapi Dr. Kahangwa wa NCCR-Mageuzi? Yuko wapi Prof. K. Mkumbo? Kuwaweka wasiotakiwa kwenye Mdahalo ni uchonganishi na kutumika.

Unataka kukimbiwa tena?


Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Mtoa mada unatakiwa kuweka ushabiki pembeni na kuzungumza kitu chenye manufaa kwetu wote. Kwanza inatakiwa tujue ni mada zipi zitazungumziwa.
Pili ndugu mtoa mada unatakiwa kutambua kuwa ishu siyo kusomea uchumi au kutosomea uchumi. Ukiangalia vizuri, mheshimiwa Mkapa kwa taaluma ni mwandishi wa habari lakini kwenye uongozi wake walau aliimarisha aliimarisha uchumi ukilinganisha na mheshimiwa aliyepo madarakani ambaye kwa taaluma ni mchumi lakini uchumi wenyewe umeporomoka. Rais anaweza asiwe mchumi lakini akateua cabinet ya wataalam wakatengeneza uchumi imara na kumfanya aonekane wa maana zaidi kuliko wataalam wenyewe.
Tatu, uongozi si taaluma uliyosomea darasani bali ni kipaji mtu anachokuwa nacho katika kuongoza. Tukifuatilia watia nia tunaona kwa taaluma ni watu wa kada tofauti lakini wanaamini kuwa wanaweza kuongoza. Sasa kama suala ndo hilo Slaa kama walivyo wengine anaweka nia ya kuutaka urais kwa kuwa anajua vipaumbele vinavyopaswa kuwekwa ili kuikwamua nchi kiuchumi kama walivyo wagombea wengine. Kinyume chake unataka kutuambia kuwa hata hajui kwanini anagombea? Au unataka kumfananisha na kiongozi mwanauchumi aliyebobea ambaye hajui kwanini nchi yake ni maskini?
 
Ni Ph.D ya nini mkuu??!!
Hiyo ni level ya super specialization. . . ., . . So alichosoma ndio anachokijua zaid hili wala halihitaji mjadala mreeeefu weka mapenzi kando ona ukweli
Ndani ya Kanisa Katoliki mtu kufikia PhD level anakuwa amesomea vitu vingi siyo mambo ya kanisa pekee. Jiulize kwa nini wanaena kusoma chuo kinaitwa De Propaganda Fidei?
 
It is just an aspiration. . . . .Yeye kateua hao labda tungehoji vigezo vyake lakini si kusema Zitto hafai kuwa katika huo mdahalo. . . .

Hebu niambie hasara au athari zitazotokea iwapo Zitto atashiriki

Mpwa

Toka lini unapima kila kitu kwa msingi Wa Hasara na Faida?

Wakati mfuruki anawaita watia nia Wa CCM alisema mijadala hii ni kwa wale wote wanaotaka kuwa ma Rais Wa nchi yetu kwa kutaka kugombea. Ndio maana aliwaita wale waliotangaza nia tu.

Kwa sisi wananchi tuko tayari kumsikiliza yeyote mwenye mawazo mema kwa Taifa letu lakini ni vizuri objectives za mdaharo zikazingatiwa.

Hats Dr Slaa bado ugombea wake haujajurikana na hajawahi kusema atagombea.Na yeye anamuita wa nini?

Afadhali ya zitto ambaye yeye kaishasema ni razima awe rais.

Hivyo huu mjadala zito hausiki labda uandaliwe mjadala Wa vyama vya siasa kwa ujumla.
 
mmh napata wasiwasi na muandaaji wa huo mdahalo Mara ya kwanza alisema watia nia ya urais ndio watakaohusika .....Dr Slaa bado hajatangaza nia ya kugombea urais pia sijasikia Zitto akiweka nia ya kugombea urais .....nahisi kuona maluweluwe mbeleni juu ya huu mdahalo isijekuwa upo kisiasa zaidi baada ya kiuchumi kama alivyotangaza hapo awali
 
Wana jamvi, Wasalaam!

Dr Slaa anataraji kukutanishwa na wataalam wa uchumi akiwemo Prof Lipumba na Zitto kabwe!

Mdahalo huo ulioandaliwa na Ndugu Mafuruku unataraji kuwa wa aina yake kwani Slaa anakutanishwa na watu wawili ambao ni moto wa kuotoa mbali kwenye mambo mbali mbali hasa ya kitaalam.... na wengi wamekuwa wakijiuliza Slaa ataongea ni mbele ya wataalam hawa wakina Lipumba na Zitto?

Namshauri Dr Slaa ajiandae mapema na chama kimpe muda wa kitosha na material kwaajili ya mdahalo huu wa kitaalam unao subiriwa kwa hamu!

Wengi wamekuwa wakijiuliza kuwa Slaa atajenga hoja gani mbele ya vichwa hivi hasa Lipumba na Zitto!

Pia kuna watu wameanza kufikiri kuwa huu mdahalo unaweza kumpa ushindi lipumba na kusababisha kuteuliwa kuiwakilisha UKAWA kwenye mbio za Urais 2015!

Karibuni wana jamvi!

Tangazo linasema Presidential Aspirants. Bado naendelea kujiuliza kama Zitto ni mgombea urais mtarajiwa. Kisheria, kikanuni na kiutaratibu hataweza kugombea kwa mwaka huu. Kama ndivyo na kama kweli ni mtu wa kutafakari sitarajii atokee kwenye mjadala huo lakini pia sitarajii Dk. Slaa, Prof. Lipumba na Dk. Makaidi wafanye mjadala unaohusu wagombea urais 2015 na mgombea ubunge 2015. Aidha, najiuliza kama hii Tweet kweli ni ya Ali Mufuruki au hacking..........Vinginevyo sikutarajia atumie neno Presidential Aspirants akijua kuwa kati ya wanaoalikwa mmojawapo hana vigezo Kikatiba.......THINK BIG GUYS
 
Mleta mada, hivi hapa tunajadili nini sasa??
Je Unaweza kusema matokeo ya football match kabla mechi haijachezwa??
Kajipange.
Shame upon you.
 
Back
Top Bottom