Dr. Slaa uso kwa uso na Zitto kwenye Mdahalo tarehe 18 June!

Wana jamvi, Wasalaam!

Dr Slaa anataraji kukutanishwa na wataalam wa uchumi akiwemo Prof Lipumba na Zitto kabwe!

Mdahalo huo ulioandaliwa na Ndugu Mafuruku unataraji kuwa wa aina yake kwani Slaa anakutanishwa na watu wawili ambao ni moto wa kuotoa mbali kwenye mambo mbali mbali hasa ya kitaalam.... na wengi wamekuwa wakijiuliza Slaa ataongea ni mbele ya wataalam hawa wakina Lipumba na Zitto?

Namshauri Dr Slaa ajiandae mapema na chama kimpe muda wa kitosha na material kwaajili ya mdahalo huu wa kitaalam unao subiriwa kwa hamu!

Wengi wamekuwa wakijiuliza kuwa Slaa atajenga hoja gani mbele ya vichwa hivi hasa Lipumba na Zitto!

Pia kuna watu wameanza kufikiri kuwa huu mdahalo unaweza kumpa ushindi lipumba na kusababisha kuteuliwa kuiwakilisha UKAWA kwenye mbio za Urais 2015!

Karibuni wana jamvi!

Huu uzi upo kimipasho zaidi,laiti ungepelekwa studio na kutengenezewa beat nzuri!,bila shaka nao ungeshinda tuzo ya KTMA mwakani
 
Hui mdahalo niwatiania ya urais au sielewi
iposiku utasikia mdahalo wa waziri wa afya na devis mwamnyange kadrilani pengo halafu mada utaambiwa ulinzi wa mipaka yetu.

Hakuna popote ambako wagombea urais watakwepa debate juu ya uchumi.Uchumi ndio msingi wa uchaguzi wa nchi.Haukwepeki.
 
kama hii ni kweli itakua mojawapo ya vichekesho vya.mwaka .... debate ya presidential aspirants ... wakati aliyetangaza nia ni mmoja tu hapo .... hii debate haitafanyika!
 
Kwako philosopy ni nin?kwanini Dr Slaa na Lipumba wana same culture kuliko Lipumba na Samweli Sitta?kwako culture ni nin?hapa nadhani kuna tatizo la definition yako ya philospoy ni nin na culture ni nin?

Fahamu tu haiwezekani watu wote ata wakiwa chama kimoja kuwa watakuwa na mtazamo mmoja kwenye kila kitu, ukiona hivyo jua kuna tatizo kubwa kwenye kundi hili kwenye bongo zao, vinginevyo binadamu watakuwa na tofauti hapa na pale.

Pia ni vizuri tuwe tunajifunza ata nchi zingine wanafanya nini, Angalia hapa: Wagombea wa chama kimoja, democratic mwaka 2008, akiwepo Clinton na Obama.
0221_debate_460x276.jpg

imrs.php

From left to right, Democratic presidential hopefuls former Sen. John Edwards, Sen. Barack Obama, New Mexico Gov. Bill Richardson, Sen. Hillary Clinton, Sen. Joseph Biden, and Sen. Christopher Dodd, are seen before the Des Moines Register Democratic Presidential Debate in Johnston, Iowa, Thursday, Dec.13, 2007. (AP Photo/Charlie Neibergall)

Hivyo tujifunze kuzoea democrasia na kuzoea kupima uwezo wa wagombea kwenye issues.Tatizo tumezoa kubeba mbuzi kwenye gunia ndio maana tunaogopa wagombea/mgombea tunayempenda kuwa atashindwa kuperform kwenye debate hivyo tunaficha udhaifu wake.Tuache hayo mambo.Tupime uwezo wa wagombea.

Hakuna mdahalo wa namna hiyo duniani,mgombea mbunge kushiriki mdahalo na wagombea urais?Ni ujinga mtupu, jifunzeni kwa jirani yenu Kenya. Tumevurunda kwenye tuzo za muziki za KTMA na Mpira wa miguu, hata kuandaa mdahalo pia tushindwe?Au tumelogwa?
 
Ukweli hauko mbali sana zama ujanja ziko ukingoni kabisaa. . . . . . . time will tell
 
Nimepitia hotuba ya Dr. Makaidi na kugundua kwamba alisema UKAWA wameshafanya kikao chao na kumpitisha mgombea Urais, Sasa nashangaa Lipumba katangaza majuzi na nasoma mahala pengine Chadema wanasema wao watatangaza mgombea Urais kupitia Chadema 8/8/2015 muda mfupi tu kabla ya uchaguzi. Kazi kweli kweli..
Kama UKAWA wameishampitisha mgombea urais kulikuwa na haja gani Prof Lipumba, kuchukua fomu za kugombea urais au hamna kuaminiana.
 
Mzee Makaidi wakati mwingine uwa napata shaka sana na umakini wa anayoyaongea.

Sitaki kuamini kama kuna mtu anaweza akaamini kuwa mtu wa aina ya Prof Lipumba eti anaweza akachukua fomu, kuitisha press, kuita watu wengi na kutumia gharama kubwa eti huku akiwa "anaigiza".Hilo silioni!!

Kuonyesha kuwa Prof Lipumba yupo serious, CUF washatangaza wagombea ubunge, na Lipumba hajaachiwa jimbo lolote.
 
Ali Mufuruki is after something bad for prosperity of the drastic changes of the way we want to govern ourselves! You're going to find out soon what the Bad thing Mr. Mufuruki is after with!!
 
Naona taasisi ya Uraisi inazidi kudhalilishwa kila siku. Huyo Ali Mafuruki inatakiwa apimwe akili, utaitaje Presidential Aspirants debate wakati hata wagombea wenyewe bado hawajajulikana? Kama ni hivyo nialikeni na mimi nishiriki maana nasikia huko CCM watangaza nia wamefikia zaidi ya thelathini. Lingekuwa jambo la maana kama mdahalo ungewahusisha angalau watangaza nia ingawa ingefaa zaidi kwa wagombea ambao wameshateuliwa na vyama vyao. Kabla ya hapo wajulikane hao ni wagombea uteuzi ndani ya vyama vyao.
 
Mleta mada anamihemko kweli kweli. Uzi wa ziara ya Dr Slaa Marekani upo humu. Sina shaka na uwezo wa Dr Slaa dhidi ya zzk japo jamaa atajitahidi na kujitutumua sana.
 
Mag3, wewe ni mtu makini sana, sitaki kuamini kuwa tafsiri yako ya presidential aspirants ni wagombea wateule!
 
Mleta mada anamihemko kweli kweli. Uzi wa ziara ya Dr Slaa Marekani upo humu. Sina shaka na uwezo wa Dr Slaa dhidi ya zzk japo jamaa atajitahidi na kujitutumua sana.

Sijaelewa mantiki yako ni nin, lakini itoshe tu kusema wote hawa wawili ni wanasiasa wenye uwezo.Nadhani watu wengi wenye perspective kama yako ndio wanaohofu sasa kama kiongozi wanayempenda ataperform vip dhidi ya mwingine.

Hili kwa mwananchi wa Tanzania sio muhimu, muhimu tujue viongozi wanasimama wapi kwenye issues mbalimbali.
 
Inaonyesha wengi tuko kishabiki zaidi na tunajiandaa kuendelea kumuunga mkono 'Mtu wetu' hata kama itadhihirika wazi kua hana 'uwezo' kiakili bali ni mpiga kelele tu!
 
Kama kusema ukweli ndio kuwa ''m-bavicha'' basi wacha niwe! Zitto saizi yake ni kina Ben Saanane. Hatuwezi kumkweza asimame na Lipumba au Slaa!

...well spoken zito anahangaika angalau arudi bungeni, tofauti na Dr Slaa ni international political figure kavuka level za akina zito zamani sanaaa...
 
Let's stop being too judgmental... Wait for the day ndipo muanze na miluzi yenu. Kuweni na subira.
 
Back
Top Bottom