Elections 2010 Dr. Slaa usiache kwenda kwetu

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,827
4,172
Kuna tetesi kuwa Dr. Slaa atamaliza kampeni zake kwa Sugu (Mbeya Mjini).

Yuko sahihi.

Lakini chondechonde Dokta. Usiache kwenda jimbo la Songwe. Watu wa jimbo la Songwe nadhani wamerogwa kama si kulaaniwa.

Jimbo la Songwe ni jimbo masikini kuliko yote mkoa wa Mbeya. (Kuna dhahabu. Wamepigwa marufuku kulima pamba, japo ni zao linalostawi huko. Wamekubali kijinga). Elimu hovyo, barabara hovyo, afya hovyo, kipato cha mtu mmoja-mmoja hovyo, maji hovyo. Taja kila kitu cha hovyo, utakipata jimbo la Songwe.

Kuna wakati walikuwa na mbunge anaitwa Ntwina. Jamaa ana kiburi. Hazungumzi kitu bungeni kama EL. Akizungumza anazungumza pumba. Kuna kipindi alileta utapeli. Akajifanya analeta umeme. Akarundika nguzo kipindi chote cha awamu ya pili ya Mkapa. Hakuna umeme. Wananchi wakapandwa hasira. Wakazichoma moto nguzo za umeme. Nikadhani labda wamepata somo. Kipindi cha Awamu ya kwanza ya JK, wakachagua mbunge mwingine. Kama kawaida. Tapeli. Amepigwa chini uchaguzi huu. Kinachonishangaza ni kwamba wameshindwa kujua kuwa tatizo siyo wabunge wanaowachagua.....tatizo ni CCM. Hapo ndipo tatizo lipo. Heri wanaopewa hongo ya fulana; hawa wakwetu wanahongwa mataputapu. Aibu!

(Ukiondoa familia yetu) Hawa jamaa wamerogwa kama si kulaaniwa. Nasikia wamepitisha mbunge wa CCM bila kupingwa.

Dr. Slaa naomba upite huko. Japo dakika 15. Kura ya baba ni ya kwako 100%. Usijali naomba uende. Japo hutaenda, utakapokuwa Mbeya, lipe jimbo la Songwe japo aya moja kwenye hotuba yako maridhawa.

Pamoja tutaikomboa Tanzania.
 
Nani atapigia kura chama cha vilaza??

Mbowe V11

Mgombea Mwenza V11

Raisi wao Mchungaji Bible study

Nikuisaliti nchi kuwakabidhi hawa jamaa, Mungu aepushembali
 
Nani atapigia kura chama cha vilaza??

Mbowe V11

Mgombea Mwenza V11

Raisi wao Mchungaji Bible study

Nikuisaliti nchi kuwakabidhi hawa jamaa, Mungu aepushembali

Kumbe wajua kama Dr. Slaa ni Rais?

Safi?

VP jamaa yenu mwenye kifafa anayeanguka-anguka hovyo?
Vipi jamaa yenu anayeishi kwa nguvu za maruhani?
Vipi jamaa yenu alivyo na upeo mdogo wa kufikiri kiasi cha kuamini kuwa nchi haiwezi kwenda bila misaada? Matonya, ombaomba,
 
Jamani hizo ni habari njema, wahusika tafadhali fanyeni juu chini mpeni taarifa Dr Slaa afike hapo Songwe ili watu wapate kupona huu ugonjwa wa ccm. Ni hatari sana.
 
Hivi Dr. Slaa anaenda lini Lindi, Mtwara, Mafia, Unguja na Pemba? Mwenye ratiba iliyorekebishwa atuhabarishe.
 
Hivi Dr. Slaa anaenda lini Lindi, Mtwara, Mafia, Unguja na Pemba? Mwenye ratiba iliyorekebishwa atuhabarishe.

Hivi kwa nini hivi sasa Kikwete hafanyi kampeni? Amerudi Dar kuvaa msuli. Au ana break ya kale ka ugonjwa?
 
Ni mgeni rasmi kweny mechi ya stars na morroco

Of course that is what he (Kikwete) knows.

Mkapa mwenyewe aliyebuni mradi wa Uwanja wa Taifa hajui hata kama kuna mechi. Anashughulika na watu wa Dafur wanaoteswa kwa sababu ya weusi na ukristo wao.
 
jk anahudhuria kama mgeni rasmi ktk mpambano kati ya stars na moroco, lazima 2pigwe bao/mabao maana huyu jamaa hata kuwa mshindi kwa chochote mwaka huu labda udiwani kule kwao chalinze, kadeclare failure kwa timu yote. pls jk dont come, stay away...
 
Back
Top Bottom