Dr. Slaa, umeketi upande gani sasa?

Dr. Slaa, umeketi upande gani sasa?

Criterion

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2008
Posts
11,797
Reaction score
11,899
Sote tunalifahamu hili. Lakini kwa kukumbushana tu, Dr. Aliondoka CHADEMA kwa sababu ya Ukaribisho wa Lowasa ambao ulikuwa ni kinyume na utashi wake. Hoja kuu ilikuwa kwamba Lowasa ni fisadi na hakupashwa kutendewa na upinzani namna alivyotendewa.

Dr Slaa hakuishia kuondoka tu, bali pia alikwenda hatua moja mbele ya kusaliti upinzani na kupigia kampeni Chama Cha Mapinduzi akiamini kwamba kwa kuondoka kwa LOwasa, basi ufisadi umekwisha ccm. Bila shaka aliamini kwamba yeye na CCM sasa watakuwa wakiongea lugha moja, wakitembea njia moja, na kushare vision.

Lakini hivi punde, Mwenyekiti wa CCM ametamka suala linaloonyesha kwamba Lowasa hana hatia yoyote na anastahili kuenziwa kwa mambo makuu aliyolifanyia taifa hili.

Ninaomba kusikia kutoka kwa Dr. Slaa. Nini msimamo wako Dr kwa sasa, juu ya ubia wako na ccm, ccm inayotangaza kumuenzi Lowasa kwa kuwa ni mtu safi, mtu safi kwa rafiki zako CCM ambao umeingia nao ubia wa imani ambao wanamsifu mtu unayeamini ni mbaya kiasi cha kubadilisha kwa sehemu kubwa ndoto za maisha yako?

Uliamini wa haraka haraka kwamba CCM without Lowasa ni takatifu. CCM hiyo hiyo inatangaza kumuenzi Lowasa kwa ubora wake. Unajisikiaje baada ya hapa?

CCM wote, semeni, Lowasa ni fisadi ama si fisadi?
 
Tabby Dr Slaa hakuondoka Chadema sababu ya ukaribisho wa Lowasa, Dr Slaa aliondoka Chadema sababu hakupitishwa kugombea urais ila Lowasa alipitishwa. Laiti Lowasa angekaribishwa tu na yeye Dr Slaa kupitishwa kugombea urais angekuwa bado Chadema.

Kilichomtoa daktari Chadema ni tamaa ya urais
 
Nimeandika sababu aliyoisema yeye. Sikupenda kusema maoni yangu ije ya alichokitamka mwenyewe. Kwa hali ya kawaida ninategemea kusikia msimamo wake kwa kuwa kilichopo ni sawa na "Nguruwe kachinjiwa mskitini". Ataendelea na imani hiyo ama atahalalisha nguruwe?
 
Dr.mihogo sjui ataapishwa lini tangu ateuliwe ubarozi
 
Sote tunalifahamu hili. Lakini kwa kukumbushana tu, Dr. Aliondoka CHADEMA kwa sababu ya Ukaribisho wa Lowasa ambao ulikuwa ni kinyume na utashi wake. Hoja kuu ilikuwa kwamba Lowasa ni fisadi na hakupashwa kutendewa na upinzani namna alivyotendewa.

Dr Slaa hakuishia kuondoka tu, bali pia alikwenda hatua moja mbele ya kusaliti upinzani na kupigia kampeni Chama Cha Mapinduzi akiamini kwamba kwa kuondoka kwa LOwasa, basi ufisadi umekwisha ccm. Bila shaka aliamini kwamba yeye na CCM sasa watakuwa wakiongea lugha moja, wakitembea njia moja, na kushare vision.

Lakini hivi punde, Mwenyekiti wa CCM ametamka suala linaloonyesha kwamba Lowasa hana hatia yoyote na anastahili kuenziwa kwa mambo makuu aliyolifanyia taifa hili.

Ninaomba kusikia kutoka kwa Dr. Slaa. Nini msimamo wako Dr kwa sasa, juu ya ubia wako na ccm, ccm inayotangaza kumuenzi Lowasa kwa kuwa ni mtu safi, mtu safi kwa rafiki zako CCM ambao umeingia nao ubia wa imani ambao wanamsifu mtu unayeamini ni mbaya kiasi cha kubadilisha kwa sehemu kubwa ndoto za maisha yako?

Uliamini wa haraka haraka kwamba CCM without Lowasa ni takatifu. CCM hiyo hiyo inatangaza kumuenzi Lowasa kwa ubora wake. Unajisikiaje baada ya hapa?

CCM wote, semeni, Lowasa ni fisadi ama si fisadi?

Hao wa lumumba wanachojua ni kushangilia na kushabikia kila kitu maadam chatoka kwa Jumbe wa Magogoni, bila kuchelewa hata kama hawajaelewa. Wamejaaliwa nyuso za chuma, zisizo na soni.
 
Maadam kashakubali kale ka cheo kwisha habari yake.
 
Lowassa Ni kiboko yao, akiwa ccm upinzani unasema Ni fisadi, akienda kwa upinzani ccm wanadai Ni fisadi Sasa amewachanganya kweli kweli hadi mkuu wa nchi hajui Lowassa Ni nani, Sasa kwa umoja wetu ccm na upinzani tuimbe kwa pamoja.... Tuna...imaaniii na Lowaaassaaa...... Oyaaa oyaaaa
 
Dk slaa ashaapishwa ubalozi alioteuliwa? na ni balozi wa wapi?
 
Maadam kashakubali kale ka cheo kwisha habari yake.

20180126_102413.jpg

Mkiwa mko busy na majungu yeye a napambana na hali yake........
Loud and clear.
 
Back
Top Bottom