Dr.Slaa Tatizo Lako Nini Hapa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr.Slaa Tatizo Lako Nini Hapa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Junius, Oct 23, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Imeandikwa na Fidelis Butahe na Salim Said

  SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kuagiza mitambo ya kuzalisha umeme ya Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), iwashwe wadau mbalimbali wamepokea kwa hisia tofauti uamuzi huo huku, Dk Willibrod Slaa, akisema uamuzi huo hautasaidia kuondoa kero za umeme nchini.

  Mitambo ya IPTL, ilisimama kuzalisha umeme baada ya kubainika kuwa ilikuwa ikiuza umeme wake kwa bei ya juu.

  Wiki iliyopita Dk Slaa, alielezea kushangazwa kwake na hatua ya Rais Kikwete kuzungumza lolote kuhusu tatizo la umeme ambao makali yake yanazidi kuongezeka.

  Lakini jana akizungumza na gazeti hili, Slaa alisema hatua hiyo ya rais haitasaidia na kusisitiza kuwa upungufu wa maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme unajulikana tangu mwaka 2005.

  "Kipindi hiki chote alikuwa wapi, hebu tujiulize ni kiasi gani cha fedha ambacho Watanzania wamekikosa kutokana na kukosekana kwa umeme, Bunge liliiagiza serikali inunue mitambo ya IPTL lakini ilikataa hivi sasa ndio inaona umuhimu wake," alisema Dk Slaa.

  Dk Slaa mbaye ni Katibu Mkuu wa Chadema, hatua kamwe hatua hiyo haitasaidia kutatua tatizo la muda mrefu la umeme hapa nchini na kwamba serikali inapaswa kutafuta suluhisho la kudumu badala ya utaratibu wa zima moto.

  Katika agizo lake kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Rais Kikwete alitaka kuhakikisha kuwa umeme unapatikana haraka iwezekanavyo na kuitaka Wizara ya Nishati na Umeme, kwa kushirikiana na Tanesco, kusimamia masuala yote ya kiufundi.

  Masuala hayo ni pamoja na upatikanaji haraka wa mafuta, ili umeme wa IPTL uanze kuzalishwa mara moja.

  Hali kadhalika aliitaka Wizara ya Fedha na Uchumi, kuhakikisha kuwa inatafuta fedha za kuwezesha ununuzi wa mafuta na mahitaji mengine muhimu, ili umeme uweze kuzalishwa.

  Rais pia aliiagiza Wizara ya Katiba na Sheria, kusimamia masuala ya kisheria kuhusu suala hilo.

  Agizo hilo la Rais Kikwete limekuja siku kadhaa baada Dk Slaa, Zitto Kabwe na wafanyabiashara mbalimbali, kumuomba aingilie kati ili kulinusuru taifa katika maafa makubwa ya kiuchumi yanayosababishwa na tatizo la umeme.

  Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Juma Duni Haji, alisema uamuzi huo ni ishara ya kwamba Rais Kikwete ameanza kutapatapa.

  "Huu ni mwaka wa nne tunaimbiwa nyimbo za matatizo ya umeme lakini serikali ya Rais Kikwete imeshindwa kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hili" alisema Duni.

  Alisema kitendo hichno ni cha aibu kubwa kwa serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na Rais Kikwete.

  "Miaka mitano inakaribia kumalizika sasa lakini serikali imeshindwa kutatua kero moja tu kwa wananchi ambayo ni umeme, tunapoteza mabilioni ya fedha kutokana na kukosekana kwa nishati ya umeme," alisema.

  Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Samwel Ruhuza alisema kinachoiponza serikali ya awamu ya nne ni kutosikiliza ushauri wa wapinzani na wataalamu mbalimbali.

  "Serikali imekuwa na tabia ya kupenda kutibu ugonjwa kuliko kutafuta kinga kwanza," alisema.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Fordia, Bubelwa Kaiza, alisema hatua ya rais kuagiza mitambo ya IPTL kuwashwa ni jambo zuri kwa kuwa serikali ina mamlaka kisheria kufanya hivyo.

  Kaiza ambaye ni mwanasheria alisema jambo hilo ni la dharura na kusisitiza kuwa rais lazima atakuwa ameshauriana na wanasheria wake.

  "Rais kipindi chote alikuwa kimya ni wazi kuwa alikuwa akijadiliana na wasaidizi wake ili kuona jinsi ya kutatua tatizo hili, ni uamuzi mzuri kwa maslahi ya taifa, binafsi ninampongeza," alisema Kaiza.

  Mitambo ya IPTL ina uwezo wa kuzalisha megawati 90 hadi 100 za umeme ambazo zinatosha kuziba pengo la megawati 80 katika Gridi ya Taifa na kumaliza mgawo unaolikabili taifa.

  Mgawo wa umeme ulioanza wiki mbili zilizopita, umetokana na kuharibika kwa mtambo wa Songas UGT1 wenye uwezo wa kuzalisha megawati 20, mtambo mmoja wa Kihansi unaotoa megawati 60 na Hale uliokuwa unazalisha megawati nane.


  SOURCE: MWANANCHI
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kwa hiyo anavyoona ni kuwa watanzania waendelee kukaa gizani wee mpaka hapo serikali itakapotata ufumbuzi wa kudumu na si "wa zimamoto" wa tatizo la umeme, wakati huo huo ni wao waliopiga makelele kumtaka rais achukuwe hatua haraka kulinusuru taifa na hasara za kiuchumu n.k kutokana na tatizo hili,au labada mlitaka aje au alete mvua na mafuriko ya kujaza mito, Au Dr.Slaa na wenzako labda mumsaidie rais huo ufumbuzi wa kudumu ndiyo upi,mtakuwa mushawasadia wananchi na credit itakuwa kwenu...vinginevyo hatujuwi mnataka lifanyike lipi katika tatizo hili ambalo kwanza lilihitaji ufumbuzi wa dharura kwanza..na mengine yafuatie kwa hatua badae.
   
 3. M

  Magezi JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Labda hujamuelewa Dr. Slaa, yeye argument yake ni kwa nini serikali imekaa kimya miaka minne mpaka leo ndo wanakurupuka tena kuomba mitambo ambayo walisha isusa wakati wangeweza kuwa wamenuua mitambo mingine siku nyingi??

  Pia hii ni solution ya dharula ambayo haina tofauti na dharula iliyo leta richmonduli!!! Hoja hapa ni kwa nini serikali (CCM) hawawezi kupanga mipango na wakatafuta solution ya kudumu wanakuwa busy na temporary planning tu kila wakati???
   
 4. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  walipomtaka rais achukue hatua kwa tatizo lililopo walimaanisha nini....long or short term measures?
  Na kwanini sasa ameshachukua hatua za dharura kwanza bado wanapayukwa tu...upinzani wa kupinga kila kitu hausaidii kitu...wala haukuengezei mtaji wa kisiasa kama ndo chadema na Slaa wanatazamia hilo.
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  Oct 23, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Tatizo lililoonekana hapo ni namna muungwana anavyoshughulikia suala la UMEME. yaani mpaka wapinzani wameanza kumpa directions za kufanya badeala ya kushauriwa na kabinet yake hivyo anajiondolea uwezo wa kuaminika.

  na anachotumia slaa ni campaign chaos ambapo baada ya muungwana kubend na kukubali ushauri wao, basi alijiingiza mtegoni mwenyewe hivyo wacha waendelee kulimana naye shekhe
   
 6. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #6
  Oct 23, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mkuu,

  Nakuunga mkono asilimia mia moja!

  Nia ya Dr Slaa ni ya kweli na dhati kabisa.Ni lazima yeye kama Mtanzania ahoji ni kwa nini a kipindi cha miaka mitano kero imekuwa ile ile tuu ya ukosefu wa umeme.

  Nashindwa kuamini kama hii serikali imekosa njia mbadala ya kutatua tatizo hili sugu na kama hali ndio hii,basi hata miaka mingine mitano tutaendelea kuwa na matatizo ya umeme maana Slaa anachotaka ni suluhisho la moja kwa moja kwa tatizo hili!
   
 7. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #7
  Oct 23, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kutaka...kutaka...kutaka...suluhuisho la kudumu...si aseme Dr. Slaa ni suluhisho gani kwa hali ya nchi linaweza likawa la kudumu, kuongoza nchi kazi...nyinyi...si kupiga makelele tu,upinzani wa aina kama hii ya kina Dr. Slaa wa kupinga kila kitu hata chenye chembe za mafanikio unatia kichefuchefu wakti mwengine...ni kama washabiki na mpira wa miguu wakiwa jukwaani...wanasema kila kitu lakini anayejuwa joto ya game ni mchezaji uwanjani...kina Slaa wawe na chembi ya shukurani alau ufumbuzi wa dharura umepatikana...watz mkubali kuwa nchi hii haina uwezo wa hivyo wa kulala na kuamka na mpango wa kudumu wa tatizo la nishati kama umeme...panahitaji mambo mengi yafanyike. Mambo ya kulalamika lamika tu inafika wakati serikali inajiona haina uchaguzi na hatimae inajikuta katika deals za kujitia hasara tu kama za richmond.
   
 8. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #8
  Oct 23, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  It is unfortunate kwamba Dr. Slaa ameripotiwa kusema kwamba hii move haitasaidia. At this point, every little bit helps. Kama Dr. Slaa angekuwa mwanasiasa mkomavu kuliko alivyo angeanza kwa kusema hilo kabla ya kusema lingine la maana sana ambalo nina mashaka ripoti hii ambayo kama kweli ni direct iko responsible inatishia kulimeza.

  Miminaona hapa kuna tatizo kwamba rais anatoa quick fix itakayoaddress symptom badala ya ku address ugonjwa.Tamko la rais ni quick fix, tunajua uchaguzi unakuja na CCM hawataki bad publicity. Lakini hii move haina strategic thinking, na ninapata sense kwamba Dr. Slaa, even though the political animal in him reportedly got the better of his judgement kwa kusema hii haisaidii, the bigger statement ni kuwa hakuna strategic change.
   
 9. M

  Magezi JF-Expert Member

  #9
  Oct 23, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mkuu nadhani bado huelewi jinsi gani wananchi wanakerwa na uendeshaji wa serikali ya sasa ya CCM chini ya JK. Baada tu ya JK kuingia madarakani alisema hadharani kuwa mgao wa umeme utakuwa historia muda si mrefu lakini tangu atamke maneno yale hakuna jitihada zozote za kuwa na miakakti ya muda mrefu na mfupi kuhakikisha tatizo la umeme linapunguzwa.

  Angalia issue ya mitambo ya Dowans, hii mitambu imekiuka sheria za uwekezaji kwa nini isitaifishwe naserikali?? hilokashindwa, bunge liliiagiza serikali inunue mitambo ya IPTL na bajeti ikapangwa lakini ni nini kimefanyika?? zaidi ya porojo za ngeleja tu eti tuna mazungumuzo!! mazungumzo gani yasiyokwisha??

  Kuna mradi wa kujenga transmission line kutoka kusini kwenye mitambo inayozalisha umeme wa gesi kuunganisha na tunduma, je ni nini kimeshindikana?? kwa sababu gharama ni US$700m, kwa nini hizi zisitafutwe??

  Hapo juu mkuu unasema kuendesha serikali si mchezo????.....kwa nini kama JK kashindwa asijiuzuru??? mbona kaisha ambiwa muda mrefu ajiuzuru na anakaa kimya????...ah....anaboa sana JK na hatukutegemea angekua hivi alivyo.
   
 10. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #10
  Oct 23, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  .,SIJAONA Sehemu DR.Slaa amepinga hatua za Rais.
  Amelaumu kitendo cha rais kukaa kimya muda mrefu na kuja na utatuzi wa dharura tofauti na matarajio ya ukimya kwamba ungekuwa na mshindo mkuu.UFUMBUZI WA KUDUMU.
   
 11. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #11
  Oct 23, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Magezi, Shaycas.
  Labda kuna jambo jingine zaidi ya hayo linalokufanyeni baadhi yenu, mumsulubu JK kama Jk na si kama rais...this is obvious...JK hakusema hilo tu, alisema mengi na hayajafanyiaka...na si kama hataki yasifanyike...JK is surrounded by wrong decision makers...plus matatizo serikali yake iliyoyarithi kutoka awamu iliyopita..ni makubwa na yanaigharimu nchi kwa kiasi kikubwa..kiasia ambacho nathubutu kusema mipango mingi ya serikali imekwamishwa na athari za uozo wa serikali ya mkapa...nyumba ilipohamiwa na JK ilihitaji usafi kwanza kabla ya kuweka fanicha nyingine...this is what he is doing...nafikiri shida yenu mlitaka rais baada ya umeme kuzimwe aje aseme o.k tutanunuwa nyuklia...au akurupuke tu bila ya utafiti wa kina wa hilo mnalotaka liwe suluhisho la kudumu...hebu kuweni wakweli mnachompinga JK ni zaidi ya uongozi wake...mm mpinzani always I identify myself as such....lakini I do not appose any and everything...this guy Slaa and his fellows oppose unreasonably.
   
 12. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #12
  Oct 23, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  I am tired of this "JK is surrounded by wrong decision makers" as an excuse.

  If JK is surrounded by the wrong decision makers, then he is the chief wrong decision maker by having these wrong decision makers around him. Kila siku tunasikia "Rais alishauriwa vibaya" as if rais hatakiwi kufanya vetting ya ushauri. Katika system ya collective responsibility, rais akikubali ushauri unakuwa wa wote, na kwa sababu yeye ndiye mkubwa, in reality unakuwa wake.

  Mbona kwenye credit hatuwapi advisors ila tunampa yeye? Harry Truman had it right when he assumed responsibility kwa kuwa na kibao katika meza yake, kibao kilichosema "The Buck Stops Here". Meaning the buck of blame for anything under his administration can be passed around as much as possible, but it will always stop at his desk.

  Nyerere said something similar when he said, paraphrasing "Urais mzigo, si kitu cha kukimbilia, unazunguka nchi nzima unaona watu masikini, hawana nguo, wana njaa, yote hii ni kazi yako"

  We need a president and population that can understand this. We need to stop uttering the enbling words "the president was not advised properly" or "the president does not have good advisers"

  If the president, with all the unfettered majestic powers of his office, cannot even assemble a team of good advisers, what good do you expect from him?
   
 13. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #13
  Oct 23, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Bluray,
  May be and for what I Perceive that JK within him is the right man in the wrong system...chama ndo kilichochoka...JK might be a new trick in the hunting game...and the system...sema chama tawala...is an old dog. So can we teach an old dog new tricks...ney and never,don't expect any stupid rabbit to fall under its claws.
  what is this collective responsibility that wananchi for 45 years can't share the blames for failures?
   
 14. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #14
  Oct 23, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135

  1. First of all i don't think JK is the right man in the wrong party, actually JK is one of the more mediocre people among the pool of CCM national leadership.

  2. Hata kama JK angekuwa allright, you can't have "the right person in the wrong party" right people hawa join wrong party, once the right person anapojoin wrong party na yeye anakuwa wrong person by association.Ndiyo maana unaweza kuwa mtu safi tu, lakini ukafungwa jela kwa sababu tu ulisimama mtaani na rafiki zako waliotoka kuiba gari wakakukuta mtaani wakakupa lifti, katika gari lililoibwa, polisi wakija kuwakamata kwa sababu mko katika gari la wizi wote mnaenda kunyea debe, mpaka wakijua kuwa wewe huhusiki utasota at least mwaka ndani. Kwa hiyo this business ya right person in the wrong party ni apologism tu.

  3.Halafu, kama JK ni right person in the wrong party, kwa nini asikisafishe chama? Yeye si ni Mwenyekiti? Si ana nguvu? Ninavyojua mimi, watu wenye honor zao huwa na principle moja ukiwapa kazi, either wanaifanya kazi vizuri, ama wakiona kazi imewashinda wanajiuzulu na kukurudishia kazi yako utafute mwingine atakayeweza.Sasa JK hajafanya lolote kati ya haya mawili, uzuri wake uko wapi?
   
Loading...