Dr. Slaa; Tafadhali Uliza kwa SAUTI KUU haya! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa; Tafadhali Uliza kwa SAUTI KUU haya!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MsandoAlberto, Jan 22, 2011.

 1. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  1. Ni kesi gani ilifunguliwa Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara mwezi Dec 2010 inayohusu Dowans? Mbona kesi hiyo haipo tena?

  2. Ni kesi gani imefunguliwa Mahakama Kuu Masjala ya Kawaida (Normal Registry) na ni nani ameifungua kesi hiyo? Ni wakili gani amepeleka hizo Documents? Kama ni Rex Attorney kwa nini wamepeleka na wao si mawakili wa Dowans?

  3. Je Rex walihusikaje katika kuhaulisha mkataba kutoka Richmond kwenda Dowans? Na walihusikaje katika kuvunjwa kwa mkataba huo? Na kwa nini wameshauri Dowans walipwe? Walishiriki vipi kwenye kesi ICC?

  4. Je kabla ya Rex kuhamia kwenye jengo lao waliwahi kuwa wapangaji kwenye jengo la Rostam? Wanamfahamu vipi Rostam?

  5. Kwa nini serikali iko tayari kulipa bila hata kupata baraka za mahakama? Sheria zetu za nchi ziko wazi. Dowans wanajua au wanapaswa kujua kwamba hukumu waliyopata lazima isajiliwe kwenye Mahakama yetu na wanasheria wake waitetetee. Hakuna kuvunja sheria za kimataifa hapo. Ni kuheshimu sheria za nchi kama ambavyo tunatakiwa kuheshimu sheria za kimataifa.

  6. Kwa nini serikali inataka kudharau sheria za nchi kwa kusingizia kuheshimu sheria za kimataifa? Suala la Dowans si sheria ya kimataifa, ni makubaliano ya kibiashara kwamba tukigombana tutapeleka ugomvi wetu ICC. Atakayeshinda atafuata sheria kama zilivyo. Sheria ni kwamba hukumu lazima isajiliwe. Tatizo liko wapi kufuata sheria?

  Tafadhali Dr. Slaa. Nisaidie kuuliza hayo maswali. Kilio cha watanzania kinaishia hewani. Machozi ya samaki!!!

  Wasalaam diwani wako!
   
 2. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Haya maswali ni vizuri ukampatia Mbunge wako kama si wa CCM atakuwa na utashi wa kuuliza tofauti na hapo majibu unayo
   
 3. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Dr. Slaa sio Mbunge hawezi kuuliza Bungeni. Anaweza kwa nafasi yake akauliza kwa Msajili wa Mahakama Kuu, Akamuuliza Waziri wa Sheria, akamuuliza Waziri Mkuu au akawauliza watanzania!

  Nategemea utasoma between the lines kinachosemwa hapa!
   
 4. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  lile jengo la MIRAMBO 5O ni la ROSTAM?hapo nitaunganisha dots
   
 5. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #5
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mbunge wangu ni kwa tiketi ya CCM. Kamati kuu ya CCM imeshatoa msimamo wake. Mh. Mbunge wangu ambaye pia ni Mh. Waziri haya hayamuhusu. Chama chake kimeshasema 'uungwana ni kulipa....lakini kwa sababu kuna watanzania wameenda mahakamani...'. Kwa maneno hayo suala la Dowans kutokulipwa ni la watanzania kwa Kamati Kuu ya CCM uungwana utumike tulipe.

  Natamani sana ningeweza kumuuliza Mbunge wangu. Hata huko bungeni kwa idadi ya wabunge sioni ahueni yoyote! Itabaki story!
   
 6. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #6
  Jan 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Maswali ni ya msingi ila serikali ya CCM haina utamaduni wa kujibu maswali ya msingi. Uwezo wao ni kujibu kwa mipasho tuu
   
 7. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #7
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Au majibu aliyokuwa anatoa Tambwe Hizza jana. Kwao suala la Katiba ni propaganda! Analiongelea kwa wepesi sana. Eti ni watu wachache ndio wanataka Katiba mpya!
   
 8. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #8
  Jan 22, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Mahakamani imeshasema mlalamikaji na mlalamikiwa wanaruhusa ya kumalizana nje ya mahakama hata kama hukumu haitasajiliwa na mahakama. Hata kama watanzania watakula pumba au kukaa gizani miaka mitano lazima deni la 94 billion lilipwe.
   
 9. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #9
  Jan 22, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mbunge wake kwa bahati mbaya sana ni Cyril Chami wa chama cha jembe na nyundo na bahati mbaya zaidi ni waziri wa jk.

  Kwahiyo kuomba Dr. Slaa amsaidie kuuliza, huenda ni kutokana na kujua kwamba mbunge wake hawezi hata kuthubutu kwenda pale mahakama kuu kutaka kujua kinachoendelea.
   
 10. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #10
  Jan 22, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,982
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Huyo waziri ambaye ni katibu wa nini sijui kwenye chama cha SISIEM Mh Chiligati si alisema kuwa pomoja na kulipa wanangojea majibu ya hiyo kesi iliyofunguliwa mahakamani???????
  Sasa wewe unasema hiyo kesi kule mahakamani haipo tena???????
  Tufanyeje sasa, maana ndo tumekwisha hivyo, maana wangesema swala hili lipelekwe bungeni labda lingejadiliwa, ingawa hawa wabunge wa SISIEM ni wengi huwezi kuwapiku.
  Lakini wanatengeneza kitanzi cha kujimaliza, tunganganie kuunda KATIBA MPYA YA KUTUKOMBOA, huo ndio utakuwa mwisho wao. Kwani mtu akituibia si tunataifisha mali zake?????????
   
 11. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #11
  Jan 22, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hapo ndipo nimeanza kuwa na wasiwasi kwamba huenda hawa wezi walivyoona wanaharakati wamefungua kesi mahakama kuu kitengo cha biashara wakipinga hiyo tuzo kusajiliwa wakafanikiwa kuona mlango wa uani na unapitika bila ajizi wakaamua kupitia huko.

  Naona hapa mahakama inaisaidia dowans wapate malipo kiurahisi, kilichobaki kwa wananchi sasa nadhani ni kuishinikiza tanesco isije kuthubutu kulipa bila tuzo kusajiliwa mahakama kuu kama sheria inavyotaka.
   
 12. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #12
  Jan 22, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Kwa maamuzi ya kamati kuu, uhuru wa mahakama umeshaingiliwa na lazima tuzo isajiliwe. Anayesajili tuzo si ameteuliwa na aliyekuwa mwenyekiti wa Kamati Kuu iliyoamua DOWANS walipwe. Muhimu hapa kila mtu alilie yeye na familia yake wafanye nini maisha yasomge mbele. Pengine mnapiga kelele wakati labda pesa zimeshachukuliwa kama "IOU" kinachifuata ni kuandikia tu hati za malipo lakini pesa ilishatoka
   
 13. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #13
  Jan 22, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Alberto, nilidhani una direct contact na katibu mkuu wa chama chako, au ulitaka watu Hapa janvini wakuongezee mawazo? Kama ndivyo basi bora uweke taarifa zote bayani ili hilo lifanyike. Hatari yake ni pre-emption lakini.

  Vinginevyo, andaa waraka wako kisha usaidiane na dr Slaa ufuatilie majibu halafu utuletee hapa jamvini. Just thinking aloud!
   
 14. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #14
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hii haraka ya kuwalipa sijui inatokana na nini. Haiingii akilini mtu anakudai halafu wewe ndio unaenda kufungua kesi unadaiwa. Hao Dowans si wafuatilie kesi yao wenyewe? Kwa nini hawajitokezi? Watalipwa bila kukatwa hata kodi? Inafika mahali unakereka mpaka basi. Kwa nini tunanyanyasika hivi?
   
 15. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #15
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Gurudumu, ninayo na nimeshamtumia maswali yangu. Kwa kweli nimeongea na mtu anayefuatilia hii kesi imeniuma sana. Watanzania tunafanywa wajinga na tunadanganywa mchana kweupe. Ila naamini kwamba hili lina mwisho. Hali hii haitaendelea hivi kamwe.

  Nimeweka maswali yangu jamvini ili wanaJF wafahamu najiuliza nini. Naamini kwamba na wao pia watauliza hayo maswali popote pale watakapopata nafasi ya kuuliza!
   
 16. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #16
  Jan 22, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kuna tatitizo la watalaamu wetu hususani wanasheria kupenda kuongelea sana matatizo na makosa serikari wanayofanya bila ya kuchukua hatua za kisheria, either kuishitaki serikari au kuwangulia kesi watu wote waliohusika kulisababishia taifa hasara kwa uzembe au makusudi, Ni wakati wa vitendo wazalendo na watalaamu wetu wa sheria wazalendo mtusaidie kwenye mapambana haya sisi wananchi tutawaunga mkono kwa hali na mali kuliokoa taifa mikononi mwa lobyist na mafisadi
   
 17. P

  Popompo JF-Expert Member

  #17
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  msando nakukubali ila hawa kina Tambwe hiza wa JF hawashindwi kuropoka:nono:
   
 18. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #18
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  LHRC walipoenda kuulizia waliambiwa kesi imefunguliwa. Kesi hiyo ni No. 4 ya 2010. Ndipo walipoamua kuweka pingamizi. Lakini cha kushangaza baada ya kufuatilia wameambiwa kesi hiyo haipo waende Mahakama Kuu Masjala ya Kawaida!! Walipofika huko ndio wakakuta attachments zinazoonyesha mwenendo wa kesi ya ICC ambazo Rex ndio wamepeleka mahakamani kwa madai kwamba wametumiwa kwa DHL!

  Hapa kuna maswali mengi sana. Kwa nini hili suala liwe na usiri mkubwa hivi? Ina maana hawa wenzetu haliwahusu? Hawana uchungu nalo? Wanataka tulipe?
  Kwa nini hawatusaidii? Suala hili limebaki ni la wananchi ambao kilio chao ni sawa na kumulika giza nene na tochi!
   
 19. T

  Topical JF-Expert Member

  #19
  Jan 22, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nasikitika kuwa hana sauti tena ya kuuliza hayo maswali?

  Amebanwa sana kazi nyingi na hivi sasa mshahara hautoshi, and mchumba amekuw very demanding!
   
 20. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #20
  Jan 22, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  Topical ... . bosi wenu Tambwe Hiza tulimwona jana akifafanua pumba zenu... vipi ameshawalipa posho zenu...?
   
Loading...