Dr. Slaa: Siasa siyo maneno "Hapa Kazi tuu" Awasiliba Mbowe na genge lake

Bavicha mko kwa ajili ya Mbowe na siyo kwa ajili ya chama cha chadema.

Mko tayari chadema ife kabisa ila mbowe abaki salama.!!
Hapa ndiyo usomi wenu unakuwa wa kutia mashaka.

Mbowe kula ruzuku ya chama kula ruzuku ya chama ,bavicha watakulinda.
Mbona Mbowe hakauki kwenye vichwa vyenu au bei yake kubwa
 
Mbowe you made us as country to be the poorest. Hakuna kinachofanyika ni wewe tu. Ila komaa mpaka ubaki peke yako kwa kuwa tubinadamu tutakuunga mkono 2025.
Mnajidanganya sana, Muheshimiwa mbowe ndiye anayeshikilia amani ya nnchi hii la siyo mngekimbia na chupi mkononi
 
Kwa mtu mwenye akili zinazofanya kazi sawasawa isingekuwa rahisi kwa mtu kama Dr Slaa kuendelea kubaki Chadema hasa baada ya ukaribisho wa upande ule wa pili.
Ukiongozwa na mahaba ya chama kamwe huwezi kuelewa alichofanya Dr Slaa kujiondoa Chadema.
Turudi kwenye msingi wa hoja ya siasa ni sayansi na sayansi haitaki uwongo. Tuliendeshwa na mahaba ya chama kipindi cha kampeni na kutokuona mbali, sasa ile dhana ya siasa ni sayansi na haitaki uwongo naona inajidhihirisha kwa upande wa Chadema kadiri siku zinavyozidi kwenda.
 
Uzalendo unapimwa kwa upendo wako kwa wenzako.Majivuno na kiburi kwa kuwa wewe unacho na mwingine hana alafu unamukejeri asiekuwa nacho badala ya kumusaidia atoke hapo alipo.hayo sio mambo ya kujivunia uzalendo Mwenyezi Mungu uwa anafundisha mtu badae hata kama ameisha sahau kama alimudhurumu mtu huko nyuma
 
Njaa mbaya saana aiseeee! Huu Upuuzi unazungumzwa na mtu aliyewahi kuwa Upande huo
Nonsense unataka aseme siasa ni mbwembwe na matusi.....
Siku zote alisema siasa si maneno,ndiyo maana alifanya kazi na Chadema ikaheshimika.....Leo chadema iko wapi?
Mnapoteza watu mliowatafuta na kuwapigania kwa gharama ta damu bado mnacheka.
 
Mnaojaribu kufuta nyayo za Dr Slaa hamtafanikiwa maana anatakiwa mtu mwenye mtazamo wake kuvaa viatu vya Raisi 2025. Najua kwa umri wake atakua hafai kuwa rais lakini Tanzania inahitaji sana mtu kama yeye kuendeleza mapambano dhidi ya umasikini, ujinga na Maradhi
 
Labda kwa vile sometimes siasa ina miscalculation. Kinachopangwa huenda tofauti. Kitendo cha kumkaribisha lowassa Cdm japo inasemwa ndio ilichangia wapitakane wawakilishi wengi bungeni, lakini madhara yake yake wamepatikana wabunge ambao hawakuwa na uchungu na chama. Wababaishaji na wapitia njia tu. Ni mara mia hata slaa angebakishwa wangelipata cream inayofahamu uchungu wa chama. Haya ya kuhisiana kuna mnada unafanyika pengine isingekuwepo. Cdm ya kina dr slaa ndiyo iliyowafanya c.c.m imtafute Rais wa sasa magufuli. Binafsi niwe muwazi, dr slaa pamoja na upungufu wake, alihitajika kwa muda ule. Na ndio maana swali lake la assets and liability(nadhani) hadi sasa linafikirisha. Dr slaa aliondoka cdm kwa kinyongo, na hivi kama anawashambulia cdm still ni kinyongo tu. Kwa maoni yangu, ilimpasa akae kimya, tu kwani mchango wake unathaminika, wanaojua maana ya siasa za ukweli hawatapönda hapa. Pamoja na sifa zote nazompa, dr slaa, angekuwa sasa katika huu mwenendo wa siasa nchini angeleta upinzani lakini sio kama ule wa kabla hajaamua kutoka. Naiona cdm ikirudi kwenye grassroot yake kwa kubaki wenye itikadi nacho.(wale ambao hawotukubali kuunga juhudi) pia, nawaona c.c.m wakiitazama cdm kupitia site mirror. Kazi ipo. Kwa kumtoa dr slaa ni kama walipoteza uimara wa chama, kwa kumkaribisha lowassa walipata alama za juu za uwakilishi wa muda. Yamkini ni kama walionjeshwa. Wajifunze. Kuwapokea wanahomia kwa akili sana. Dr slaa unakumbukwa japo(ni ukweli usiosemwa) watasema chama si mtu ni taasisi. Lakini kumbe mgeni hakuja ili mgeni apone.
 
Back
Top Bottom