Dr. Slaa Receives A State Reception In Alabama Capitol !

Dr. Slaa Receives A State Reception In Alabama Capitol !

Rtackket

Member
Joined
Sep 24, 2013
Posts
74
Reaction score
373
Katibu mkuu wa Chadema Dr. Willibrod Slaa katika ziara yake nchini Marekani iliyoandaliwa na umoja wa vyuo vikubwa nchini humo ya kujifunza mambo mbali mbali, imemfikisha leo katika jimbo la Alabama na kupokelewa na wakuu wa jimbo hilo akiwemo Gavana pamoja na Waziri wa biashara.

Alabama ni moja ya majimbo yaliyokuwa nyuma sana kiuchumi na kimaendeleo siku za nyuma. Uchumi wake ulitegemea kilimo kwa 90%. Miaka 25 iliyopita, viongozi wake walibuni mikakatati ya kulibadilisha. Leo, Jimbo la Alabama ndio moja ya majimbo yenye viwanda vikubwa vya magari kama Honda, Mercedes Benz, Airbus, Hyundai, Raytheon, Space station, Wallgreens na mengineyo Uchumi wake unakua kwa kasi kubwa.

Kupitia kauli mbiu yake ya “Vision Tanzania” Dr. Slaa alipata kukutana na viongozi wa jimbo hilo ili aweze kujifunza mbinu ambayo ataweza kuwarudishia watanzania ili nao waondokane na umasikini. Licha ya yote, Gavana wa jimbo hilo pamoja na mawaziri wake, wako tayari kushirikiana na Tanzania kwenye mambo ya biashara hasa miundombinu ikiwemo bandari, ujenzi wa madaraja na bandari. Dr. Slaa na mkewe Josephine walipokelewa na Gavana pamoja na mawaziri wake
attachment.php

Dr. Slaa akiwasili kwenye gavernor mansion baada ya kupokelewa na Waziri wa Biashara pamoja na Waziri wa mambo ya nje
attachment.php

Viongozi wa juu wakibadilishana mawazo na Dr. Slaa
attachment.php

Dr. Slaa Akimkabidhi Waziri wa Biashara Sera za Kiuchumi za Chadema
attachment.php

Dr. Slaa, gavana na mawaziri wake wakiwa katika mjadala wa ushirikiano
attachment.php

Dr. Slaa kwenye picha ya pamoja na gavana
attachment.php

Gavana akimnong'onezea Dr. Slaa neno wakati wa kuagana
attachment.php

Dr. Slaa akiongozwa kuelekea kwenye msafara wake
attachment.php

Uongozi wa jimbo na Dr. Wakila chakula cha mchana iliyotayarishwa kwa ajili yake
attachment.php

Dr. Slaa akimshukuru mmoa wa askari waliokuwa wakiongoza msafara wake

attachment.php


Kubwa ya yote alichojifunza Dr. Slaa ni kwamba, serikali inaweza kuwa na ufanisi hata ikiwa na baraza dogo. Jimbo la Alabama lina Mawaziri sita tu, huku CCM ikiwapa walipa kodi wa tanzania mawaziri 70 wasiokuwa na kazi. Wengi wao wakiwa na matumizi makubwa huku wakina mama wakijifungua sakafuni, walimu wakinyimwa haki zao, polisi na wanajeshi wakiishi hali duni na wanafunzi wakisoma chini ya miembe. CCM ni janga kubwa lililowakumba watanzania



Chuo Kikuu Cha Kilimo Auburn

Kadhalika Dr. Slaa ametembelea chuo kikuu cha auburn ambayo ni moja ya vyu vikuu vikubwa zaidi vya utafiti duniani. Auburn Inafanya shuguli zake nchini Kenya, Uganda, Senegal na kwingineko barani Afrika. Nchini Kenya, chuo cha auburn inawasaidia wakulima mbalimbali hasa wafugaji wa samaki na technologia za kisasa inayowawezesha kusafirisha samaki wengi kwenda ulaya Ulaya. Kati ya Kenya na Uganda, utafiti wao umetoa zaidi ya ajira 7000.

Walipoulizwa kwa nini walikwepa Tanzania, hawakuficha ukweli. Walinena kwamba ni vigumu sana kufanya kazi Tanzania. Ufisadi uliwazuia ingawa wangekuja na fedha zao kutoka benki ya dunia na shirika la kimarekani la USAID ambayo inadhamini miradi yao sehemu nyingi barani Afrika ikiwemo Kenya na Uganda. Viongozi wa chuo hicho wako tayari kurudi Tanzania ikiwa mazingira ya kazi yatabadilika hasa kukiwepo na serikali mbadala, ambayo Mh. Slaa amewahakikishia kwamba Chadema hiko tayari kufanya nao kazi.

Viongozi wa Auburn University wako tayari kusaidia vyuo vya Tanzania kama Sokoine kwa kuwafundisha waalimu na pia kubadilishana nao technolojia za kisasa za kilimo. Wako pia tayari kuwafundisha wakulima wa aina zote na hata walaji mbali mbali mbali.

attachment.php

Dr. Slaa akiwasili chuo kikuu cha Kilimo Cha Auburn. Nyuma yake ni walinzi kwenye msafara wake
attachment.php

Dr. Slaa akilakiwa na Dean wa Chuo cha Kilimo pamoja na viongozi wengine wa juu wa chuo hicho
attachment.php

Dr. Slaa akiwa kwenye mazungumzo na uongozi wa chuo cha kilimo kushirikiana na vyuo vikuu vya tanzania kwa lengo la kubadilishana teknolojia na ujuzi ili kuinyanyua kilimo cha tanzania na pia kuongeza ajira
attachment.php


 

Attachments

  • Dr. Slaa Akikaribishwa Kwenye Gavernor Mansion.jpg
    Dr. Slaa Akikaribishwa Kwenye Gavernor Mansion.jpg
    53.4 KB · Views: 8,801
  • Viongozi Wa Jimbo Wakimkaribisha Dr. na Mama Slaa.jpg
    Viongozi Wa Jimbo Wakimkaribisha Dr. na Mama Slaa.jpg
    53 KB · Views: 13,022
  • Dr. Slaa akimbakibidhi Waziri Wa Biashara Sera Za Uchumi Za CHADEMA.jpg
    Dr. Slaa akimbakibidhi Waziri Wa Biashara Sera Za Uchumi Za CHADEMA.jpg
    39.7 KB · Views: 12,885
  • Slaa na Baadhi ya mawaziri.jpg
    Slaa na Baadhi ya mawaziri.jpg
    72.9 KB · Views: 12,808
  • Dr. Slaa na Gavana.jpg
    Dr. Slaa na Gavana.jpg
    54.3 KB · Views: 12,744
  • Gavana Akinongoneza Jambo Kwa Dr. Slaa.jpg
    Gavana Akinongoneza Jambo Kwa Dr. Slaa.jpg
    60.5 KB · Views: 8,298
  • akiongozwa kwenye msafara wake.jpg
    akiongozwa kwenye msafara wake.jpg
    84.8 KB · Views: 8,131
  • Chakula Cha Mchana.jpg
    Chakula Cha Mchana.jpg
    62.9 KB · Views: 12,741
  • Dr. Akimshukuru moja wa Askari waliotoa ulinzi kwenye msafara.jpg
    Dr. Akimshukuru moja wa Askari waliotoa ulinzi kwenye msafara.jpg
    38.7 KB · Views: 12,467
  • Dr. Akiwasili Chuo Cha Kilimo. Nyuma ni Walinzi.jpg
    Dr. Akiwasili Chuo Cha Kilimo. Nyuma ni Walinzi.jpg
    62.6 KB · Views: 8,060
  • Viongozi wa Chuo Cha kilimo Wakimpokea Dr. Slaa.jpg
    Viongozi wa Chuo Cha kilimo Wakimpokea Dr. Slaa.jpg
    45.3 KB · Views: 7,991
  • Mazungumzo na Viongozi Chuo Cha Kilimo.jpg
    Mazungumzo na Viongozi Chuo Cha Kilimo.jpg
    42.1 KB · Views: 7,949
  • Chuo Kilimo.jpg
    Chuo Kilimo.jpg
    54.2 KB · Views: 7,962
  • Baraza la mawaziri.jpg
    Baraza la mawaziri.jpg
    36.9 KB · Views: 7,855
Sasa hiyo ndio "state reception" au kaomba appointment apeleke makaratasi yake ya ufataani?

Mijitu mingine mna mnanga mtu ambae hanangiki.

Alipewa dakika ngapi na Gavana?
 
"Walipoulizwa kwa nini walikwepa
Tanzania, hawakuficha ukweli. Walinena
kwamba ni vigumu sana kufanya kazi
Tanzania. Ufisadi uliwazuia ingawa
wangekuja na fedha zao kutoka benki ya
dunia na shirika la kimarekani la USAID
ambayo inadhamini miradi yao sehemu
nyingi barani Afrika ikiwemo Kenya na
Uganda"

ridiculous eti ni vigumu kufanya kazi tanzania

mashirika mangapi ya US yanafanya kazi Tz

abbott fund
CDC
ASCP na kadhalika
 
Wadanganyika, masikiini watanzania, wanasiasa wananiacha hoi kwelikweli. Paliponiacha hoi ni huyo askari aliyeshiriki msafara. Huyo rais wa nchi kupata ulinzi wa namna hiyo huko usa si rahisi sembuse kijikatibu mkuu wa chama fulani tanzania ? Duu majanga. Freemason chagawood ltd wapo kazini. Amkeni watz na usanii huu wa wanasiasa wetu hata ccm wapo wa aina hiyo.
 
Hivi hiyo ilikuwa ziara binafsi au ziara ya kichama? Nauliza kwa sababu naona kwenye meza ya mazungumzo yupo Dr. Slaa na Mama Josephine lakini upande mwingine naambiwa kuna Gavana na Mawaziri. Kwa hiyo ujumbe wa CHADEMA uliongozwa na Dr. Slaa na Mama Josephine peke yao? Inakuwa kama Mseto vile; kwa upande wa Alabama State uwakilishi ni wa viongozi wa Jimbo lakini kwa upande wa CHADEMA uwakilishi unakuwa wa familia zaidi!

 
😛eace: sio safari za kikwete zisizo na tija kwa taifa.kazi yake kuhangaika na vimada wake wa marekani. Viva dr slaa.
 
Sasa hiyo ndio "state reception" au kaomba appointment apeleke makaratasi yake ya ufataani?

Mijitu minngine mna mnana mtu ambae hanangiki.

Alipewa dakika ngapi na Gavana?

Naona kuna document zinabadilishana mikono pale lakini tatizo ni kwamba Dr. Slaa yupo peke yake. Isije ikawa ni mikataba kati ya CHADEMA na Alabama?
 
attachment.php

Uongozi wa jimbo na Dr. Wakila chakula cha mchana iliyotayarishwa kwa ajili yake​


Mijitu mingine kwa kuzuwa, mpaka inachafuwa. Hicho chakula kiko wapi hapo? au hayo makaratasi ndio chakula?
 
Back
Top Bottom