Dr Slaa: Nimewasilisha Ushahidi kumshtaki Chenge..

Dr Slaa: Nimewasilisha Ushahidi kumshtaki Chenge..

Hatuna serikali iliyo serious kwa kuwa hakuna msafi wao rushwa kwanza na Tanzania baadaye .So ni sarakasi tu hawawezi kufanya lolote .
 
Naamini Dr Slaa yuko strategic na hili maana kilichowazi ni kwamba watatupilia huu ushaidi kwa madi kuwa hautoshi au wanaweza kufungua kesi ambayo ni legelege ili kuwasafisha kupitia mahakama. Wote tunajua kuwa serikali haina nia ya kuwashitaki hawa watu na kwa jinsi mahakama zinavyofanyakazi kwa kuitegemea serikali ni wazi hakuna cha maana kitakachopatikana.

Najua Dr. Slaa yuko strategic na hili na amejiandaa kukabiliana nalo kwa mbinu tofauti. Kama hawataukubali ushahidi na kufungua kesi basi itakuwa rahisi kwa Dr. Slaa kuwakabiri na mbinu nyingine na hapa nguvu ya umma itatumika bila shaka.


Iwapo waatakubali na kufungua kesi legelege kumfool Dr. Slaa na kutumia zaidi ya miaka miwili au zaidi kuendesha kesi, basi Dr. Slaa lazima awe na strategy ya kukabiliana na hili.

Nadhani pressure zaidi inatakiwa iwe kwa serikali kutuambia ni nani aliyehusika kama wanansema chenge hausiki ili hali ukweli ni kwamba wizi wizi upo! Wizi hauwezi kufanyika pasipo mwizi! Hapa ndo pa kubana hadi mwisho bila kulegeza..

Hapo anawamaliza maana watasema ni muongo hawatachukua hatua then anarudi kwa mahakama ya wananchi basi kitaeleweka tu .Kawapa sasa usikie longo longo nasi tuta hoji kujivua gamba ni kupi then tunawabana .Hadi watumie polisi na jeshi .
 
Inasikitisha sana. Kwenye kesi za UFISADI mkubwa, si PCCB, CJ wala DPP wanachukua nafasi za viapo vyao. DPP anageuka kuwa Mtetezi wa Mashtaka badala ya kuwa Mwendesha Mashtaka na waliobaki wanageuka kuwa mataulo ya kuwasafisha Watuhumiwa, kazi ambayo wanaifanya hata kabla ya kesi kupelekwa Mahakamani. Katika msingi huu huwezi kutegemea matokeo ya hukumu iwe Mtuhumiwa kukutwa na hatia Mahakamani.

Iwapo DPP atakubali kufungua na kuendesha kesi hii, basi itakuwa ni kunyamazisha umma na mbinu ya kiufundi ili katika hukumu vijisenti akutwe hana hatia. Maana ya haya matokeo itakuwa ni:
  1. Dr. Slaa daima ni mzushi. Anawasingizia watu
  2. Dr. Slaa ameipotosha serikali na kuipotezea muda, hela na rasilimali zingine za walipa kodi
  3. Chenge na wengine waliowahi kutuhumiwa na Dr. Slaa ni wasafi
Nakuunga mkono kwa 100% subiri uone
 
Safi sana DR SLAA hakika upo kwenye mioyo ya watanzania,ja ajabu wabunge wa CCM na CCM wote wanamtetea mwizi CHENGE,watanzania tuamke na huu ujambazi wa CCM.
 
Hapa najua Dr. amewatega coz nina uhakika hata kama ushahidi wa hizo Tuhuma niwaukweli namna gani utapotezewa tu lazima,Wote tunaona yanayoendelea Bungeni hoja za Msingi zenye mashiko na Maslahi kwa Taifa zinapigwa chini kisa kasema Mbunge wa Upinzani Watu wapo Kiitikadi zaidi nakwakuwa hata hawa Wateule wa Mkuu bado wanapenda vitumbua vyao hawawezi kufanya tofauti.

Cha msingi hapa wapelekewe huo ushahidi kama Mtego wakishindwa kureact wenyewe watakuwa wametuhalalishia kuwalazimisha kwakutumia Maandamano kwa mujibu wa Katiba Mamlaka inatoka kwa Watu na Watu wenyewe ndo sisi tunaotaka kuwaona Mafisadi behind Bars.
 
PCCB wanalinda masilahi ya CCM, viongozi wake, na watoto wao tu lkn mwananchi mtanzania anazidi kuw amaskini
 
HIVI takukuru( PCCB) wandhani isingekuwa kulinda maslahi ya kampuni ya BAE na UK kina chenge na wenzake wangeshatiwa hatiani siku nyingi UK.

Uk wanajaua wakipeleka kesi mahakamni kampuni yao kubwa ikionekana na hatia ya kushiriki katka rushwa itazuiwa kufanya bishaara kwa mujibu wa sheria za EU.

Ni hiicho tu kilichowazuia SFO naBAE kuendelea na hiyo issue mahakamani na kuimaliza issue nje ya mahakama.

Sio kwamba kina chenge na wenzke hawana hatia.

Takukuru DPP hivi mtachezea na akili za watu hadi lini?
 
IANZISHWE TAASISI YA KUPAMBANA NA UFISADI, hii takukuru ya sasa ni kwa ajili ya RUSHWA ndogondogo hata maofisa wake mafunzo walizopewa ni kwa ajili ya RUSHWA ZA KUKU, ndo mana leo utasikia mtendaji wa kijiji amekamatwa kwa rushwa ya 15,000/= mara polisi na rushwa ya 2000/=, haraka sana anapelekwa mahakamani na TBC inaandaliwa pale kupiga picha, then TAKUKURU inatembea kifua mbele, SHAME ON YOU..! Rostam kajiuzuru akiwajibika juu ya tuhuma zinazomkabili lakini bado TAKUKURU watadai hawana USHAHIDI, kwanini Takukuru inajigeuza kuwa mahakama.?? Wapelekeni Mahakamani kwanza, yaani serikali inakubali kushndwa hata kabla kesi haijasomwa.! TUSIKUBALI, mbona tumewagomea kutoa ile TUZO KWA DOWANS kwanini haijatolewa, WANATUBEEP HAWA, MAAMUZI MAGUMU YAMEBAKI KWETU, ARUSHA WANAANZA TAR 24 MWEZI WA SABA...Kazi ni kwetu.. HEKO WATANANZANIA..
 
Back
Top Bottom