Dr Slaa: Nimewasilisha Ushahidi kumshtaki Chenge.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr Slaa: Nimewasilisha Ushahidi kumshtaki Chenge..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Emils, Jul 9, 2011.

 1. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa ameendelea kumkalia kooni Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge na sasa amewasilisha serikalini uchambuzi wa ushahidi utakaosaidia kumtia hatiani mwanasiasa huyo, dhidi ya tuhuma za ufisadi katika ununuzi wa rada.

  Dk Slaa aliwasilisha waraka wa uchambuzi wa kisheria kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka Nchini (DPP), Eliezar Feleshi, akiweka wazi kwamba Serikali ya Tanzania ina mamlaka ya kufanya uchunguzi dhidi ya uhalifu kwa watuhumiwa ambao ni raia wa Tanzania.

  Katika waraka huo ambao Mwananchi umeuona, Dk Slaa ameweka wazi kuwa kazi iliyofanywa na Ofisi ya Makosa ya Jinai ya Uingereza (SFO) ililenga kubaini makosa ya kuvunja sheria nchini Uingereza na kwamba Tanzania ilipaswa kufanya uchunguzi wake katika jambo hilo.

  "Kimsingi SFO ilikuwa inafanya upelelezi kuhusiana na uvunjifu wa sheria chini ya mamlaka yao yaani Uingereza, Wales na Ireland ya Kaskazini. Makosa ya ufisadi wa rada yaliyofanywa na Watanzania (na mawakala wao) ni makosa dhidi ya Sheria za Tanzania," inaeleza sehemu ya waraka huo na kuongeza:

  "Ni kwa msingi huo mimi niko "on record" ndani ya Bunge na nje ya Bunge kuitaka Serikali ya Tanzania nayo kuanzisha upelelezi wa kwake kwa mujibu wa Sheria za Tanzania kwani walioibiwa ni Watanzania na fedha zilizoibiwa ni za Watanzania".

  Dk Slaa alisema hakuna mantiki ya upelelezi wa ufisadi uliofanyika Tanzania kuachiwa mamlaka nyingine.

  Aliliambia Mwananchi jana kuwa tayari amekamilisha uchambuzi huo na kwamba waraka husika ulikuwa katika mchakato wa kupelekwa kwa Feleshi.

  Hatua hiyo ya Dk Slaa ni kuitika wito wa DPP ambaye juzi, alimtaka kuwasilisha nyaraka zenye ushahidi dhidi ya watuhumiwa wa rada serikalini ili ziweze kufanyiwa kazi, akieleza kuwa ushahidi alionao hautoshi kumtia Chenge hatiani kama atafikishwa mahakamani. Msimamo wa Feleshi unaungwa mkono na Mwanasheria Mkuu wa serikali, Jaji Fredrick Werema, ambaye pia alimtaka Dk Slaa asaidie kupelekea ushahidi kwa kuwa sheria inaruhusu.

  Kadhalika, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah pia alishaweka bayana kwamba taratibu za kuwasilisha ushahidi ofisini kwake ziko wazi, hivyo kumtaka Dk Slaa kutumia njia hizo ili ushahidi huo akaufanyie kazi.

  "Kama Chadema wanao (ushahidi), kama alivyoeleza Dk Slaa, walete tutaulinganisha na ushahidi tulionao ili tuone kama unatosha kuitetea kesi hiyo mahakamani," alisema.

  Dk Hoseah Ambana Chikawe

  Katika waraka huo, Dk Slaa alisema kwamba Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe alilidanganya Bunge pale aliposema kwamba Serikali haina ushahidi wa kumfikisha Chenge mahakamani.

  Alisema Serikali kupitia kwa AG iliandikiwa barua na SFO yenye Kumb. Na SPCO1/D/MC ya Machi 21, 2008, iliyosainiwa na msimamizi wa kesi hiyo, Mathew Cowie kuhusu suala la rada.

  "Attorney General (Mwansheria Mkuu wa Serikali), ndiye Mshauri Mkuu wa Serikali kwa masuala ya kisheria, na hivyo ni dhahiri barua hiyo Serikali inaifahamu. Kutokana na barua hiyo, ni dhahiri Chikawe alipotosha Bunge na Taifa kwa kusema kuwa Serikali haina ushahidi," unasema waraka huo.

  Alisema barua ya SFO inawataja wahusika wote kwa upande wa Tanzania na kwamba miongoni mwao ni Chenge ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati mkataba huo uliposainiwa.

  "SFO wanaeleza fika kuwa nyaraka za mkataba zilikuwa moja kwa moja chini ya usimamizi na maelekezo ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali". Barua/Fax ya Mark Simpkins wa SPS ya tarehe 30 Agosti, 1997 ni ushahidi dhahiri wa ushiriki wa Andrew Chenge,"anaeleza DK Slaa katika barua yake na kuongeza:

  "DPP anao mkataba wenyewe wenye kuonyesha dhahiri "Financial Arrangement" na kama hana Ofisi ya Mwanasheria Mkuu inao. Dk Slaa aliweka bayana kuwa nyaraka zote husika ziko serikalini na kwamba wajibu wa raia mwema ni kutoa taarifa ya uhalifu kwa mujibu sheria zetu mbalimbali.

  "Isitoshe hisia za ufisadi huu hazikuanzia kwa raia tu bali hasa kwa chombo chenye wajibu wa kuisimamia Serikali yaani Bunge kwa mujibu wa Katiba, Ibara ya 63(2),(3)," unasema waraka huo na kuongeza: "Raia na wabunge hatuna vyombo vya dola. Kazi yetu ni kutoa mashaka (criminal suspicion na msingi wa suspicion hiyo). Kazi ya kupeleleza ni ya DPP na Dola".

  Kwa mujibu wa Feleshi kuna uwezekano wa nyaraka alizonazo Dk Slaa kuwa na ushahidi unaotofautiana na ushahidi uliopo serikalini hivyo kuwasilisha nyaraka hizo, kutasaidia kufanikisha jambo hilo.

  "Sheria zetu zina utaratibu mzuri wa kupokea ushahidi. Sheria ya Mwenendo wa Kesi na Makosa ya Jinai, kifungu cha Saba na ile ya kupambana na rushwa, kifungu cha 39, zinaeleza bayana kuwa mtu mwenye ushahidi anaweza kuuwasilisha kwenye vyombo vinavyohusika," alisema Feleshi.

  Feleshi alitoa kauli hiyo baada ya kutakiwa na gazeti hili azungumzie kauli ya Dk Slaa aliyoitoa Jumatano wiki hii kuwa Serikali ina ushahidi dhidi ya
  watuhumiwa wa ufisadi wa rada ila imeamua kuwalinda.

  Sakata la Rada Jumatano wiki hii Dk Slaa alisambaza ripoti ya SFO yenye kurasa 11 na kusisitiza kuwa ushahidi huo unatosha kumtia Chenge hatiani.

  Dk Slaa alisambaza ripoti hiyo kufuatia kauli ya Chikawe aliyedai Serikali haina ushahidi wa kuwafikisha watuhumiwa wa kashifa ya rada mahakamani. Kitendo cha Dk Slaa kukubali ombi hilo la Serikali kinabadili sura na msimamo waliokuwa nao yeye pamoja na chama chake wa kutowasilisha ushahidi na badala yake kufanya maandamano nchi nzima kuueleza umma kuhusu tuhuma hizo za rada.

  Dk Slaa alisema amefikia hatua ya kukubali kuandaa na kuwasilisha ushahidi huo kufuatia kauli ya DPP iliyotaka afanye hivyo kwa maelezo kuwa unaweza ukawa una tofauti na ule ambao Serikali inao.

  CHANZO: Mwananchi
   
 2. Kitoabu

  Kitoabu JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 5,765
  Likes Received: 177
  Trophy Points: 160
  no action watayochukua hizo propaganda 2.
   
 3. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  Nasubiri comment ya @NYC,USA
   
 4. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #4
  Jul 9, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Taratibu naanza kuona namna DPP anavyovuliwa nguo kwa kushindwa kumtia hatiani A Chenge kama ambavyo Hosea alijiweka uchi kwa kusema Chenge hana hatia. Wenye akili waliachwa midomo wazi, kisha wakaifunika kwa vitanga vya mikono yao na kumsikitikia Hosea na yule Afisa Mahusiano.
   
 5. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #5
  Jul 9, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Inasikitisha sana. Kwenye kesi za UFISADI mkubwa, si PCCB, CJ wala DPP wanachukua nafasi za viapo vyao. DPP anageuka kuwa Mtetezi wa Mashtaka badala ya kuwa Mwendesha Mashtaka na waliobaki wanageuka kuwa mataulo ya kuwasafisha Watuhumiwa, kazi ambayo wanaifanya hata kabla ya kesi kupelekwa Mahakamani. Katika msingi huu huwezi kutegemea matokeo ya hukumu iwe Mtuhumiwa kukutwa na hatia Mahakamani.

  Iwapo DPP atakubali kufungua na kuendesha kesi hii, basi itakuwa ni kunyamazisha umma na mbinu ya kiufundi ili katika hukumu vijisenti akutwe hana hatia. Maana ya haya matokeo itakuwa ni:

  1. Dr. Slaa daima ni mzushi. Anawasingizia watu
  2. Dr. Slaa ameipotosha serikali na kuipotezea muda, hela na rasilimali zingine za walipa kodi
  3. Chenge na wengine waliowahi kutuhumiwa na Dr. Slaa ni wasafi
   
 6. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #6
  Jul 9, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Taratibu naanza kuona namna DPP anavyovuliwa nguo kwa kushindwa kumtia hatiani A Chenge kama ambavyo Hosea alijiweka uchi kwa kusema Chenge hana hatia. Wenye akili waliachwa midomo wazi, kisha wakaifunika kwa vitanga vya mikono yao na kumsikitikia Hosea na yule mahusiano.
   
 7. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #7
  Jul 9, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kwa historia ya hapa JF, huyo ni miongoni mwa wasiokuwa na kumbukumbu nzuri ya wanayo-yaandika. Hilo anaweza akawa halikumbuki!
   
 8. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #8
  Jul 9, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,257
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Utasikia ''Ah, Slaa ni mropokaji tu. Ushahidi wake ni heri huu wa kwetu una maana''
   
 9. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #9
  Jul 9, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  Juzi hapa jamvini aliandika uharo wake eti Slaa hafai kuwa rais kwa sababu hajathubutu kuwapeleka wezi akiwepo baba yake mahakamani
   
 10. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #10
  Jul 9, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Enewey, mie siuiti uharo ila mtazamo wake.
  Nilimsoma akimkweza Mch. Mtikila kwa hicho alichokiita uthubutu wa kufanya kazi na mahakama akibeza njia anayoitumia Dr. Slaa na CDM kushtaki kwa wenye mahakama na mamlaka kuu juu ya nchi yao=WANANCHI!
   
 11. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #11
  Jul 9, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Nadhani hatujawaelewa DPP na PCCB, hizi taasisi mbili zimejipanga kitaalamu kuhakikisha hakuna anaekwenda mahakamani. Ukisoma kwa makini, wanachosema wao si kwamba hawana ushahidi, bali walionao "hautoshi" kuwatia hatiani hawa jamaa.

  This is where things start getting complicated, tujiulize ni nani anayewatia watu hatiani? Ni mahakama au DPP na PCCB? Hawa wawili hata wapelekewe kontena la ushaidi watasema tu,"HAUTOSHI KUWAPELEKA MAHAKAMANI".

  Slaa katimiza wajibu wake but DPP na PCCB hawataki kutimiza wajibu wao.
   
 12. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #12
  Jul 9, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Kwa kuwakumbusha tu wana jf wenzangu ni kwamba, kati ya kesi zote za rushwa zilizopelekwa mahakamani tangu mwaka 2005 hadi sasa, ni 1% tu ya kesi hizo serikali/PCCB wameibuka kidedea!
   
 13. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #13
  Jul 9, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Kesi ya nyani anapelekewa Ngedere mnategemea nini watanzania, Kama ingelikuwa enzi za Mwalimu Huyo Chenge tungeshamsahau kama kulikuwa na Mwizi anaitwa Chenge, angefungwa na funguo zingetupwa kwenye choo cha shimo au ingekuwa China chenge agekuwa yake kamba.

  Huu Utawala wa Kikwete mnategemea nini watanzania, utawala wenyewe unalinda Mafisadi na Kutetea majambazi.
   
 14. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #14
  Jul 9, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Naamini Dr Slaa yuko strategic na hili maana kilichowazi ni kwamba watatupilia huu ushaidi kwa madi kuwa hautoshi au wanaweza kufungua kesi ambayo ni legelege ili kuwasafisha kupitia mahakama. Wote tunajua kuwa serikali haina nia ya kuwashitaki hawa watu na kwa jinsi mahakama zinavyofanyakazi kwa kuitegemea serikali ni wazi hakuna cha maana kitakachopatikana.

  Najua Dr. Slaa yuko strategic na hili na amejiandaa kukabiliana nalo kwa mbinu tofauti. Kama hawataukubali ushahidi na kufungua kesi basi itakuwa rahisi kwa Dr. Slaa kuwakabiri na mbinu nyingine na hapa nguvu ya umma itatumika bila shaka.


  Iwapo waatakubali na kufungua kesi legelege kumfool Dr. Slaa na kutumia zaidi ya miaka miwili au zaidi kuendesha kesi, basi Dr. Slaa lazima awe na strategy ya kukabiliana na hili.

  Nadhani pressure zaidi inatakiwa iwe kwa serikali kutuambia ni nani aliyehusika kama wanansema chenge hausiki ili hali ukweli ni kwamba wizi wizi upo! Wizi hauwezi kufanyika pasipo mwizi! Hapa ndo pa kubana hadi mwisho bila kulegeza..
   
 15. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #15
  Jul 9, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,322
  Likes Received: 844
  Trophy Points: 280
  Uko sawa mkuu maana huyu jamaa alidai Dr.Slaa hawezi kuwafungulia kesi mafisadi wa nchi hii.
   
 16. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #16
  Jul 9, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,557
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  Still Dr. Slaa is in the right track.
   
 17. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #17
  Jul 9, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kwa ujumla toka PCCB ianzishwe imekuwa na lengo la kisanii kimataifa na la kuwasafisha mafisadi na viongozi wala rushwa wa CCM.
   
 18. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #18
  Jul 9, 2011
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Binafsi nitafurahi sana endapo huyu mwizi atafikishwa mahakamani.
  Inashangaza kuona kwamba serikali iko tayari kupokea pesa zilizorejeshwa na Bae lakini haiko tayari kufungulia mashtaka wahusika.

  Kweli nchi yetu ni ya viongozi wasanii na wasiowajibika.
   
 19. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #19
  Jul 9, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Huyu DPP kazi yake nini au aliokotwa wapi? anataka kutwambia kuwa Kesi zote za serikali ambazo wamewai kuzifikisha mahakamani wanashinda na hakuna kesi hata moja waliyowai kupereka Mahakamani wakashindwa? au anaongea akiwa hospiltali Mirembe!
   
 20. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #20
  Jul 9, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0

  Ni bora ifutwe haina maslahi yeyote kwa Umma wa Mtanzania wanabebesha wananchni mzigo wa Bure wakati hawana kazi yeyote.
   
Loading...