Dr. Slaa ni mtu makini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa ni mtu makini

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by tbetram, Nov 3, 2010.

 1. t

  tbetram Member

  #1
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nachukua nafasi hii kukupongeza Dr. Slaa kwa kuwa mtu makini. Na watanzania makini wamekukubali. Wamedhihirisha hili kwa kuwapigia kura nyingi wagombea wa chama cha Chadema katika ngazi ya udiwani, ubunge na urais.

  Dalili zinaonyesha sisiemu wanachakachua kura zako za kiti cha urais. Wanapata shida kuiba kura za ubunge na udiwani kwani mbunge na madiwani kabla msimamizi hajatangaza matokeo tayari wanakuwa na matokeo halisi kutoka vituo vya upigaji kura. Hivyo inakuwa vigumu kuchakachua. Ila kura za urais inakuwa rahisi kuchakachua kwani focus ya kuzilinda inakuwa ndogo na ngumu.

  Kwa hivyo basi, sisi wafuasi wako watiifu tunaomba ufanye utaratibu wa kuhesabu kura kwenye vituo vyote vya upigaji kura katika nafasi ya urais hasa katika majimbo ambayo wabunge walioshinda wametoka CHADEMA. Tutumie majimbo hayo kama sample size. Kwani itakuwa vigumu kuhesabu majimbo yote 239 ya uchaguzi.
  Ili tujue ukweli kama kura za urais zinazotangazwa na wasimamizi wa uchaguzi zinalingana na kura halisi zilizohesabiwa katika vituo vya kupigia kura.

  Lengo ni kuhakikisha kuwa kama CCM inashinda kiti cha urais basi ishinde kihalali na si kwa ujanja wa kuiba kura. Tuyakubali matokeo ya kiti cha urais endapo tutaridhika kuwa idadi ya kura zilizohesabiwa vituoni ni sawa kabisa na idadi ya kura zinazotangazwa na tume ya uchaguzi. Sisiemu itambue kuwa Dr. Slaa na wafuasi wa CHADEMA ni watu makini na si watu wakudanganywa kama watoto wadogo kama walivyozoea kufanya katika chaguzi zilizopita.
   
 2. KasomaJr

  KasomaJr JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 338
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Ninakupa Pongezi za dhati kabisa kwa kuwa na mawazo chanya. Ni imani yangu kwamba Dr. Slaa analifahamu hilo na yeye pamoja na Watanzania wote na si WA-CHADEMA kama wachache wanavyoamini, tupo pamoja nae katika kila hatua. Tunapaswa kulifanyia kazi kwa umakini kabisa na kwa moyo mmoja tena thabiti kuhakikisha ukweli huu unapatikana. Nitoe Pongezi binafsi kwa Dr. Slaa na kwa watanzania wote wenye mapenzi mema na nchi hii kwa kuonyesha uzalendo wao katika kupigania haki ya wanyonge.........Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki Dr. Slaa, viongozi wote wa CHADEMA, wafuasi, wapenzi, washabiki na Watanzania wote wanaotuunga mkono ktkt harakati za ukombozi wa Taifa letu.
   
Loading...