Dr. Slaa ndani ya ukonga (kiwanja cha kampala)

Godwine

JF-Expert Member
Jan 15, 2010
1,371
281
Wajumbe kwa mujibu wa taharifa zilizonifikia Dr. wilbraod Slaa leo live viwanja vya kampala ndani ya jimbo la ukonga .ukifika gongo la mboto mwisho kuna kiwanja cha kampala karibu na kiwanda cha namera yaani kiltex na sungura tex kwa wale wanaovikumbuka.

Mkutano utaanza saa kumi jioni
 
Nipo hapa Banana nimeona matangazo namimi naelekea ktk eneo la tukio! PiPppppppppppooooooozzz Powwwwwwwweeeeeeeer!!!
 
Nimefurahi kuona tayari kuna wajumbe wawili watakaokuwepo huko. Tunaomba mtujuze yatakayojiri maana tupo mbali. Tunahamu sana kusikia atakayosema kuhusu Arusha.
 
kwa wajumbe mlioko huko naomba mmuombe haongelee njaa ya Arusha Monduli, tunakufa huku, hatujui nini maana ya chips mayai. Njaa ni noma. hawaombe angalau kwa siku moja wabunge wa ccm wachangie posho yao kwenye njaa ya mondoli.
 
swali langu kwa dr Slaa akimaliza kuhutubia hoja yake ya uzalendo wa nchi,itakua chanzo cha yeye kulipwa 7.5 milioni alikitoa wapi? pili kwa nini mshahara wake na chadema hwalipi kodi? nina wasiwasi hata jibu maswali haya!
 
swali langu kwa dr Slaa akimaliza kuhutubia hoja yake ya uzalendo wa nchi,itakua chanzo cha yeye kulipwa 7.5 milioni alikitoa wapi? pili kwa nini mshahara wake na chadema hwalipi kodi? nina wasiwasi hata jibu maswali haya!

mkuu usiwe na malengo madogo hivyo, kama unataka kukusanya kodi kwenye 7.5mio unaacha trilion of maoney bila kulipia kodi usizani itasaidia. Mkuu jitahidi kufikiria mbali, mkuu naomba hamsha ubongo wako. Fikiriha hata 10yrs to come. kwani mkuu huna watoto au wajukuu au ndugu ambao watahishi miaka 50 zaidi yako? je hao watakula nini kwa mwendo wa sasa. Wacha kufikiria vitu vidogo
 
kuna thread inayohusu dr.slaa kuwa moshi leo j/mosi.tatizo cdm huwa hawana updates.wa huko moshi sijasikia chochote,taarifa ni kongamano la duce pale chang'ombe.labda kama katoka moshi kaja dar kwa choppa.
 
kuna thread inayohusu dr.slaa kuwa moshi leo j/mosi.tatizo cdm huwa hawana updates.wa huko moshi sijasikia chochote,taarifa ni kongamano la duce pale chang'ombe na dr hakuwepo.labda kama katoka moshi kaja dar kwa choppa.
kaahirisha
 
Hawa watu inabidi mtu wao wa kutoa habari afukuzwe kazi..., hakuna feedback kabisa wala matangazo ya kuwaambia watu nini kinajiri
 
wajumbe nilishindwa kuwa live kutokana na mawasiliano ya huko yalikuwa yanasumbua kidogo lakini kulikuwa na wajumbe wa kutosha huko na
dr. slaa aliongelea mambo yafuatayo

1.Ujenzi wa taifa huru
2.kulinda rasilimali
3.hotuba ya nyerere ya mwaka 1968 akiongerea haki na wajibu wa taifa
4.shutuma dhidi ya IGP na kitabu chake na onyo kwa IGP na watendaji wake
 
Taharifa ya Dr.slaa na wajumbe wengine leo ni kuelekea ujerumani kwenye semina ya uongozi , yeye pamoja na wanachama wengine wa chadema kwenye mpango ule wa semina za ujerumani kwa wanachama wa chadema
 
Back
Top Bottom