Dr.Slaa ndani ya Mwanza.

cjilo

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
884
444
Ndiyo wakuu ! Dr Slaa ndo anaelekea saut malimbe kwa ajili ya kongamano katika viwanja vya Nyamalango. Naomba kuwasilisha.

picha hizi nmezikuta kwenye ukurusa wa fb la cdm mwanza
426342_253899871368379_100002451047207_558917_2026808590_n.jpg 426905_253901274701572_100002451047207_558920_1881507769_n.jpg 432105_253892548035778_100002451047207_558899_1387327697_n.jpg

View attachment 49548View attachment 49550View attachment 49551View attachment 49552update wakuu

Asante PRISCUS navojua huku ni bondeni kabisa ziwani ambako hata gari hazifiki zinaishia njiani.

attachment.php
 
Wanafunzi wa chuo kikuu cha mt Augustine na wakazi wa Nyegezi hivi punde wanamsubiria Mh Dr Slaa kutema cheche ndani ya viwanja vya s/m Nyamalango. Naona nyimbo mbalimbali za Chama zinapigwa, wananchi wanaimba kwa pamoja. Viongozi mbalimbali wa chama mkoa wanahutubia. Nitawapa updates.
 
Tunazisubiri.:)

Wanafunzi
wa chuo kikuu cha mt Augustine na wakazi wa Nyegezi hivi punde
wanamsubiria Mh Dr Slaa kutema cheche ndani ya viwanja vya s/m
Nyamalango. Naona nyimbo mbalimbali za Chama zinapigwa, wananchi
wanaimba kwa pamoja. Viongozi mbalimbali wa chama mkoa wanahutubia.
Nitawapa updates.
 
Sasa unataka tukusaidie nini?au unataka tumchangie nauri kama arumeru mnavyo fanya,kuwa wazi tuwasaidie
 
Vipi tena umepotelea wapi mkuu? Updates, wengine tuko mbali na tukio, na huko ndiyo nyumbani! Nyegezi Academic Hill
 
Anaambatana na wabunge wa Chadema mkoa wa Mwanza, mh Wenje na Highless na viongozi wengine wa kitaifa. Bado tunawasubiri, watu ni wengi bado wanaendelea kusubiria timu nzima ya viongozi wa CHADEMA. Zinapigwa zile nyimbo za maombolezo ya wananchi waliouwa na polisi mkoani Arusha. Naona wameweka viti uwanja mzima, jua kali sana ila bado wanafunzi wa SAUT na wananchi ktk viunga vyake bado wana hamasa kubwa kumwona Dr Slaa.
 
Ratiba inaonesha hivi 5:00 kuwasili nyamalango, 5:10-5:30 ufunguzi wa kongamano na utambulisho, 5:45-6:00 uwasilishaji mada na Fred mpendazoe na prof Mlambiti. 6:30 dr Slaa, 7:00-8:00 maoni na maswali kwa Dr Slaa. Naona msafara wa magari na pipikipiki (bodaboda) unaingia viwanjani wanamsindikiza Slaa. Tayari kaishafika uwanjani.
 
mtukwao12 tafadhali heshimu uhuru wa members wengine, sasa kuanza kupost vitu tofauti ina maana gani.
 
Wakuu tayari makamanda ameishaingia katika viwanja vya Nyamalango. Sasa ni utambulisho, katibu wa mkoa wa chama Mushumbushi anawatambulisha jukwaa kuu. Wenje, Highless, mbunge wa ukerewe, mzee Sylivester mwenyekiti wa baraza la wadhamini, mayor na naibu wake wa jiji la Mwanza, madiwani na viongozi wa SAUT. Sasa prof Mlambiti anamwaga cheche...anawaasa vijana kutolala, kupigania haki zao. Anasema ameingia CHADEMA kwasababu wanauongozi thabiti wasio na woga, anaongeza kwamba umasikini umezidi umekithiri tangu JK aingie madarakani. Thamani ya shs imeshuka....
 
Ratiba inaonesha hivi 5:00 kuwasili nyamalango, 5:10-5:30 ufunguzi wa kongamano na utambulisho, 5:45-6:00 uwasilishaji mada na Fred mpendazoe na prof Mlambiti. 6:30 dr Slaa, 7:00-8:00 maoni na maswali kwa Dr Slaa. Naona msafara wa magari na pipikipiki (bodaboda) unaingia viwanjani wanamsindikiza Slaa. Tayari kaishafika uwanjani.
don-oba endelea mkuu kutuhabarisha kinachoendelea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom