Viongozi wakuu CHADEMA kutikisa nchi leo na kesho

Viongozi wakuu CHADEMA kutikisa nchi leo na kesho

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Tunapenda kuwatangazia wananchi kote nchini hasa katika mikoa ya Dar, Bukoba, Mbeya, Tabora, Simiyu na Mwanza, ambako viongozi wakuu wa chama watakuwa na majukumu mbalimbali...

DAR ES SALAAM;

Leo Jumamosi Land Mark Hotel, Ubungo Wakili Mabere Marando, Prof. Baregu na Mbunge wa Ubungo Mnyika watahudhuria na kutoa mada kwenye kongamano la mahafadhali ya vijana wa CHASO wanaotarajia kuhitimu vyuo hivi karibuni. Kongamano litaanza saa 4.00 asubuhi.

KAGERA;

Katibu Mkuu Dr. Slaa anaanza ziara ya siku 3 mkoani humo ambapo leo atakuwa na mkutano wa hadhara mjini Bukoba, kisha Jumapili atakuwa Karagwe na Jumatatu atakuwa Muleba.

Mbeya Mjini;

Baada ya ziara iliyomfikisha juzi Rungwe na jana alikuwa Kyela, Mwenyekiti wa Chama Taifa leo atakuwa Mbeya mjini ambapo atakagua zoezi la uandikishaji wapiga kira katika vituo mbalimbali ili kujionea hali halisi inavyokwenda.

TABORA;

Makamu Mwenyekiti wa Chama Bara, Prof. Abdallah Safari atakuwa mjini Tabora siku ya Jumapili ambapo atafanya mkutano wa hadhara baada ya kuhudhuria mahafali ya CHASO Kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali mjini humo.

Mwanza na Simiyu

Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu leo Jumamosi atakuwa mgeni rasmi katika mahafali ya wanafunzi wa CHASO Chuo Kikuu cha SAUT, kisha atafanya mkutano wa hadhara mjini Magu na baadae jioni atakuwa na kikao cha ndani Mwanza Mjini.

Siku ya Jumapili atafanya mkutano wa hadhara mkoani Simiyu kabla ya kuelekea wilayani Sengerema Kwa ajili ya kongamano la mafunzo ya vijana wa CHADEMA kuhusu uzalendo Kwa nchi yao.

TAIFA KUZIZIMA KESHO

Kesho Mwenyekiti wa Taifa Freeman Mbowe atatetemesha nchi kwa kuzungumza na Taifa kupitia mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe DSM.Mkutano huo utarushwa moja kwa moja na ITV

Tunaomba wananchi na wafuasi wetu kote nchini waendelee kuunga mkono chama chao.


Tumaini Makene

MKUU WA IDARA YA HABARI NA MAWASILIANO-CHADEMA
 
Mbona mnatuchanganya mara mnajiita Chadema mara UKAWA.Amueleweki:what:
 
kila ukawa wakifanya mkutano nyomi ya watu CCM mpaka wakodi watu wa Kuja kwenye mkutano.
 
Inaelekea chadema wameshajitoa UKAWA kiaina
 
Hakika hii Ni taasisi si sawa na kile chama kilichopiga marufuku viongozi wenzao kufanya siasa isipokuwa Kinana na Nape, chama cha watu wawili. Ni tofauti na kikundi kinachosubiri 'kiongozi wa chama' afanye ziara bila yeye hakuna siasa,jeshi la mtu mmoja!
 
hivi kwanini chadema hamtakagikufanya ziara jimbo la Bukoba vijijini nawapeni ushauri tembeleen jimbo hilo mtalikosa bule nawakati kunawapiga kura wengi sana make sijawahi sikia mmefanya ziara yoyote huko
 
Mbowe anaenda Mbeya kumtangaza diwani mtarajiwa mh Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu.Waliompandisha ndio waliomshusha.
 
Tunashukuru kwa taarifa, huu mchaka mchaka ni hadi Octoba wamlete tu huyo wanayemsafisha.
 
Wale waliojifungia huko Dodoma wakisikia Ratiba hii, mipango yao ovu dhidi ya UKAWA inasambaratika vichwani mwao..!!!

Go go go Makamanda

Nchi ishawiva hii, kila mahali, kila pembe ya Nchi watu wamehamasika kiasi cha kutosha. Hizi ziara za kuwakumbusha zaidi ni Limao kwenye Supu ya Mbuzi...!! Inavutia sana.

Halafu watu wa Kyela hamjalitendea haki jukwaa hili. Mmekosa hata kapicha kamoja ka Mapokezi ya Kamanda Mkuu?? Jitafakarini Next time..!!!

BACK TANGANYIKA
 
Molemo huko Simiyu anaenda Tundu Lissu au Mwalimu? tetesi zilizopo ni kuwa Tundu Lissu ataenda Bariadi hebu toa ufafanuzi
 
Molemo huko Simiyu anaenda Tundu Lissu au Mwalimu? tetesi zilizopo ni kuwa Tundu Lissu ataenda Bariadi hebu toa ufafanuzi

Makamamda wameaanza kupotezana uwanja wa vita.
 
inapendeza, wajitaidi na kuongeza na wanachama.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom