Wanaukumbi.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema, Dr. Slaa anapenda sana kujinasibisha kwamba yeye ni mzalendo wa kupindukia, anayechukia vitendo vya ufisadi na anayeionea huruma nchi yetu.
Taarifa za uhakika kabisa zinathibitisha kwamba mwishoni wa mwezi Juni, mwaka 2013 Dr.Slaa na Mchumba wake walitembelewa na kundi la Wapani wapatao 20 nyumbani kwao Mbweni, Kinondoni ambapo wote kwa pamoja walikula cha jioni.
Dhumuni la ugeni huo wa Wajapani, ilikuwa ni kuthibitisha kama kweli Chadema kina mpango wa kujenga hospitali kubwa ya kisasa katika eneo la Mlalakuwa Dar es Salaam, Wajapani hao ndiyo walipangwa au kuteuliwa kujenga hospitali hiyo, wameakikishiwa pamoja na mambo mengine ya kimaslahi yao makampuni yao mengine, kwamba msimamizi wa hospitali hiyo ndiyo atakayekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2015, kwa maana ya Dr. Slaa.
Mipango yote ya kujenga hospitali hiyo, inaratibiwa na Askofu mmoja anayemiliki Kanisa lake maeneo ya Kawe, Dar es Salaam, Askofu huyo amekuwa akifanya safari za Japani akiwa ameandamana na mchumba wa Dr. Slaa, Josephine, mpango unafanyanyika vifaa vyote vitakavyoingizwa kutoka Japani vipitie mikononi mwa Kanisa ili tu visitozwe kodi na serikali.
Hii njama za kukwepa kodi, kwa Dr. Slaa na Josephine, inaonekana kazi njema na takatifu kwa Dr Slaa.
Ni Dr.Slaa huyu huyu, ambaye miaka michache iliyopita alitangaza orodha ya aibu ya mafisadi pale Mwembe yanga, leo hii anawakimbia Mamlaka ya Mapato nchini TRA.