Dr. Slaa na Kasulumbai Waunguruma Igunga

Dr. Slaa na Kasulumbai Waunguruma Igunga

Leo ndio amewakumbuka wanaigunga? Alikuwa wapi siku zote hizi? Igunga hawapati kitu. Ngoja kina Bashe watue hapo ndio kitaeleweka.

.
Hivi Bashe ni nani vile? Hili jina ni kama nimewahi kulisikia vile, ila sikumbuki wapi.
.
 
.
Hivi Bashe ni nani vile? Hili jina ni kama nimewahi kulisikia vile, ila sikumbuki wapi.
.
Ni yule msomali jamii moja na lile vuvuzela la simba.....yote dugu moja!!!Alshabab.
 
Ama kweli kitokacho mtu chake hakimtapishi,leo CCM mna mzungumzia Bashe ilihalimlimnanga kuwa siyo raia!Kumbe mtu wakati mwingine hula matapishi yake.



Leo ndio amewakumbuka wanaigunga? Alikuwa wapi siku zote hizi? Igunga hawapati kitu. Ngoja kina Bashe watue hapo ndio kitaeleweka.
 
Ila jamani CCM wanapandikiza ukabila kwa makada wao! Hali hii itatufikisha pabaya sana!!!
 
V hadi 2015 ccm itakuwa imebakia mifupa tu
 
kwa ujumla magamba wamenaswa kote kila wakijaribu kutokea popote wanaendelea kudidimia tu,cha msingi ni kwamba watuachie jimbo letu kwa maana waliingia kwa dhuluma,nadhani kwa hali ya sasa tunahitaji uongozi makini sio wa kiujanjaujanja na kidhuluma kama wanvyotaka magamba mungu ibariki tanzania.
 
Leo Kumefanyika mkutano wa hadhara ambao umekwisha muda mfupi uliohutubiwa na viongozi mbali mbali wa CDM, lengo la mkutano lilikuwa ni kupongezana wana CDM kwa ushindi wa kesi, katika mkutano huu Dr. slaa amewapongeza wananchi wa Igunga katika kufanikisha ushindi wa kesi hii kwani walijitolea kwa hali na mali, pia amewaambia Polisi waepuke kutumika kisiasa kwani mwisho wa siku uhaibika kwa kukamata wananchi wasio na hatia na kuwaachia huru kama wakiona hawawezi kuacha basi wavue uniform na waingie kwenye ulingo wa siasa. Pia amegusia tamko la CCM kutaka kukata rufaa juu ya hukumu iliyotolewa na amesema kila kipengele kilichotolewa hukumu kina ushahidi madhubuti hivyo CCM watajisumbua bure kukata rufaa. pia amezungumzia suala la Magufuli kuuganganya umma wakati wa kesi kuwa ni mgonjwa mahututi na kushindwa kuja kutoa ushahidi wakati huohuo adubuhi akionekana kujibu maswali bungeni na hii Dr. Slaa amesema kama serikali inakuwa na waziri anayedanganya adharani na makusudi basi hapo hakuna serikali kwa hiyo kama Kikwete angekuwa kiongozi madhubuti angekuwa amekwisha mfukuza kazi magufuli kwa uongo ulioidhalilisha serikali yake. mwisho amewataka wanachi wa Igunga kushiriki Sensa kikamilifu kwani ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa letu.
View attachment 62825 View attachment 62827 View attachment 62828 View attachment 62829 View attachment 62830


Ukimpa mtu ugali wa siku moja atakusahau, ila ukimpa elimu ya kweli atakukumbuka. Hapa ni pale Igunga CCM ilipohonga hadi mwisho. Wananchi walikula walishasahau tena wana njaa kubwa kuliko ile. Slaa aliwapa elimu wanamkumbuka na wanaungana nae kuikomboa Tanzania.
Tuungane tupambane na mwizi hadi tumzike kabisaaaaaa! Huu ndiyo wakati wa ukombozi. Tanzania ya leo sii ile ya jana. Tuna uchungu sana na kodi zetu zinatafunwa na majuha wachache huku nchi ikiangamia kwa kukosa huduma bora za msingi. Wakenya walizika KANU na wametuacha mbali.
 
Leo ndio amewakumbuka wanaigunga? Alikuwa wapi siku zote hizi? Igunga hawapati kitu. Ngoja kina Bashe watue hapo ndio kitaeleweka.
Shh..! Angalia asije akakusikia mbunge wa Nzega, Mhe. Dr. Hamisi Andrea Kigwangalla, MD, MPH, MBA. Bashe, Kigwangalla, Bashe, Kigwangalla, Bashe, Kigwangalla...sijui nani zaidi? Hata hivyo mimi napendekeza atafutwe labda yule mbunge wa Igunga mstaafu...yawezekana yale majebere yaliyomwaga machozi siku anang'atuka bado yapo.
 
Watanzania wamechoka kucheka na nyani ( CCM ) na kuvuna mabua !
 
Kinachonifurahisha ni kuwa hao watu wote hapo mkutanoni hakuna hata mmoja aliyeletwa au aliyeahidiwa malipo bali wote wamekwenda wenyewe, na wote wamekwenda kupata habari njema ya UKOMBOZI.
 
Back
Top Bottom