Dr.slaa na chadema twendeni mahakamani ushahidi upo tele!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr.slaa na chadema twendeni mahakamani ushahidi upo tele!!!!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by makoye2009, Nov 5, 2010.

 1. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Hili swala la CCM,NEC,UWT(Usalama wa Taifa) KUCHAKACHUA matokeo ya kura za Urais na Ubunge liko wazi kabisa na ushahidi upo.

  Mifano halisi ni ucheleweshaji wa kutangaza matokeo kwenye maeneo yenye nguvu kubwa ya Upinzani hasa CHADEMA. Hii haikutokea kwa bahati mbaya ni MAKUSUDI. Angali kilichotokea Dar,Arusha,Mwanza,Mbeya,Shinyanga na maneneo mengine mengi.

  Majimbo ya Nyamagana,Ilemera,Arusha Mjini,Karatu,Shinyanga Mjini kura zake mpaka jana Usiku NEC walikuwa bado HAWAJAZIJUMLISHWA KWENYE IDADI YA KURA ZA DR.SLAA KWA MAKUSUDI wakti tayari wasimamizi wa majimbo walizitangaza kwa SHINIKIZO ZA WANANCHI. Nec wamefanya kusudi kuchelewesha kujumlisha ili Kiwete aonekana kuwa anaongoza kwa mbali.

  HAINGII AKILINI MTU UMPIGIE KURA MBUNGE WA CHADEMA HALAFU KURA YA URAIS UMPE MGOMBEA WA CCM KIWETE. MTU UNACHAGUA SERA ZA CHAMA SIYO SURA YA MTU. MIFANO:

  JIMBO: CHAMA:----------------------------UBUNGE:-------------------RAIS:

  ARUSHA MJINI CHADEMA................................56,208..........................54,208
  CCM...........................................................36,107..........................39,107

  MBEYA MJINI CHADEMA.................................46,411........................42,917
  CCM...........................................................24,236........................32,249

  MWANZA-NYAMAGANA CHADEMA......................38,171.........................30,991
  CCM.............................................................27,883........................32,320


  MWANZA-ILEMERA CHADEMA............................31,256..........................29,701
  CCM..............................................................26,870........................9,143

  MASWA MAGH CHADEMA.........................17,456.........................11,742
  CCM....................................................12,824.........................17,104

  MASWA MASH CHADEMA......................17,075.........................12,203
  CCM............................. 17,014.........................21,150


  Kali zaidi ni hii ya JIMBO LA Musoma mjini: Kutoka KURA 14,723 za Mbunge wa CCM na kuongezwa kufikia KURA 49,858 za KIKWETE.

  MUSOMA MJINI CHADEMA....................21,335........................23,211
  CCM.................................................14,723........................49,858???

  Hii ni zaidi ya mara 3 ya kura za Mbunge.Haingii akilini mtu amkatae mbunge wa chama halafu ampe Rais wa chama cha mbunge huyu aliyemkataa. Labda kama mtu huyo anachagua SURA na siyo SERA!!!!!!!!!!!!!!


  Mpaka sasa ukiingia kwenye WEBSITE YA TUME: http:/www.nec.go.tz Bado KURA HIZO HAZIONEKANI KWENYE MTANDAO. KWANINI HAWATAKI KUZIJUMLISHA? WANOGOPA NINI?

  Soma hizi nukuu toka Gazeti la MWANANCHI toleo la leo 5/11/2010:

  ''..............Nao wasomi wameungana na madai ya Dk Slaa wakisema kuwa uchakachuaji matokeo ya kura nchini umekuwa aibu kwa taifa.
  Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam jana, wasomi hao walisema kuna dalili zinazotia shaka kwamba matokeo ya urais yamechakachuliwa kwa kuwa hawaoni sababu kucheleweshwa kutangazwa.
  "Tunajua kuwa hata kama CCM ingeshinda, isingeshinda kwa kura nyingi kiasi hicho. Kwa nini tumsifie mtu kuwa ameshinda kwa kishindo na huku amechakachua matokeo?"alisema Dk Fairles Ilomo, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Iringa.
  Dk Ilomo alisema haiingii akilini kuelezwa kuwa matokeo yamechelewa kutangazwa kwa sababu ya matumizi ya kompyuta katika hatua ya kuhesabu kwani wakati wa upigaji, wananchi hawakutumia kompyuta.

  "Kwanini matokeo yasubiri kompyuta? Hakuna logic (mantiki) kusema kuwa kuingiza data kwenye kompyuta kulisababisha ucheleweshaji maana hata uchaguzi wa Marekani, walitumia kompyuta na matokeo yakawahi kutolewa," alisema Dk Ilomo.
  "Ni kweli uchaguzi ulifanyika vizuri na kulikuwa na amani lakini katika hatua ya kuhesabu kura na kutangaza matokeo kulikuwa na uchakachuaji hasa katika maeneo nyeti.
  "Rais aapishwe, lakini Dk Slaa ana haki ya kuendelea na malalamiko yake. Kama malalamiko hayo yakionekana yana ukweli, maamuzi mengine yafuate."

  ..............Mhadhiri mwingine chuoni hapo Harod Tairo alisema amestuka kuona matokeo hayo yanaonyesha kuwa watu wengi wamewapigia kura wabunge wa Chadema lakini si mgombea wake wa urais, yaani Dk Willibrod Slaa
  "Mimi naamini kwamba wabunge wengi wa Chadema walichaguliwa kwa juhudi za Dk Slaa. Wananchi hawawezi kuchagua mbunge wa Chadema halafu rais wamchague wa CCM. Mimi naona matokeo hayaakisi halihalisi," alisema Tairo.

  Hawa wasomi na Wahadhiri naungana nao kwa 100%.
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Nov 5, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Ulichosema ninakubaliana nacho.

  Swali: Twende mahakama ipi? Maana hapa kwetu kila kitu kipo chini ya Mkwere
   
 3. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #3
  Nov 5, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mpaka sasa hivi nawaza hawa jamaa wanawaona Watanzania ni mbumbubu??

  This is ridiculous shame on you NEC
   
 4. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #4
  Nov 5, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  waliweka sheria, ati matokeo yakitangazwa, basi hakuna kuhoji
   
 5. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #5
  Nov 5, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nadhani itakuwa ni kupoteza muda kuanza kufukuza fursa iliyopotea. Nadhani wakati huu ni wakati wa kujipanga kwa ajiri ya kurekebisha kasoro zilizopo katika tume na mfumo mzima wa upatikanaji wa takwimu za NEC kupitia harakati.
  Kazi nyingine ambayo inatakiwa kufanywa ni kuimalisha chama kuanzia kwa wananchi na hasa hasa vijijini.

  Kama kutakuwa na ulazima wa kwenda mahakamani basi iwe kushinikiza mabadiriko katika mfumo wa uchaguzi, muundo wa tume na mambo mengine yaliyosababisha kura zetu kuibiwa ama watu kupotoshwa kwa propaganda za uwongo.
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Nov 5, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,527
  Likes Received: 19,947
  Trophy Points: 280
  ndio maana walimtuma shimbo
   
 7. C

  CHAUPEPO New Member

  #7
  Nov 5, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  swali la msingi hapa chadema waende mahakama gani coz wote ni wale wale nafikiri issue ya mgombea binafsi mliona kilichotokea hata friends of court nao walichakachuliwa sembuse hili:bowl:
   
 8. Rugas

  Rugas JF-Expert Member

  #8
  Nov 5, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,053
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Umesahau K.

  Mengine uko sahihi kabisa,japo sheria zetu hazitupi mwanya wa kujitetea.Hapo wamechakachua haswa...
   
 9. kisu

  kisu JF-Expert Member

  #9
  Nov 5, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 803
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Hii NEC chini ya serikali na chama tawala ndio matatizo. Kikubwa ni kushinikizwa Tume iwe na wateuliwa kutoka vyama vyote.
   
 10. e

  ethink Member

  #10
  Nov 5, 2010
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jumla ya wapiga kula ilikuwa ngapi?
   
 11. K

  Kinara New Member

  #11
  Nov 5, 2010
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani from my understanding, Rais akisha apishwa haiwezekani kumfungulia kesi mahakamani, na pia haiwezekani kufungua kesi kama hauna uhakika na matokeo hadi watakapo mwapisha, na akiapwishwa haiwezekani kutenguliwa.

  mimi nadhani tuifuate haki yetu mtaani maana penye sheria hatuwezi kufika, maana ndo hao hao.
   
 12. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #12
  Nov 5, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Naona ata utaalamu wa kuchakachua hawanaaaaaaaaaaaaa
   
 13. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #13
  Nov 5, 2010
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  MBEYA MJINI CHADEMA.................................46,411........................42,917
  CCM...........................................................24,236........................32,249

  MWANZA-NYAMAGANA CHADEMA......................38,171.........................30,991
  CCM.............................................................27,883........................32,320


  MWANZA-ILEMERA CHADEMA............................31,256..........................29,701
  CCM..............................................................26,870........................9,143

  MASWA MAGH CHADEMA.........................17,456.........................11,742
  CCM....................................................12,824.........................17,104

  MASWA MASH CHADEMA......................17,075.........................12,203
  CCM............................. 17,014.........................21,150


  Kali zaidi ni hii ya JIMBO LA Musoma mjini: Kutoka KURA 14,723 za Mbunge wa CCM na kuongezwa kufikia KURA 49,858 za KIKWETE.

  MUSOMA MJINI CHADEMA....................21,335........................23,211
  CCM.................................................14,723........................49,858???

  Ukiangalia hesabu ya kura za ubunge na urais hazina uwiano. Inaonekana wapiga kura wengi zaidi walipiga kura za urais kuliko za ubunge. Tume ituambie idadi ya wapiga kura waliojitokeza kupiga kura vs matokeo. Na si blabla tu. Mfano Musoma mjini, kura za DR. Slaa na JK ni 73,069 na za wabunge wa ccm na chadema ni 36,058 hivyo kuna kura 37,011 ambazo ama zilienda kwa wagombea ubunge wengine, au wapiga kura hao waliamua kupiga kura za urais pekee. Bila kujumlisha kura walizopigiwa wagombea urais wengine, kura za ziada pekee zinatosha kubadili matokeo ya kura za ubunge katika jimbo hilo. Kwanini tusiamini kwamba matokeo ya urais ni batili?
   
 14. N

  Natural Member

  #14
  Nov 5, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbaya zaidi ni kwamba kura za JK zinaongezeka kwa majimbo ambayo CHADEMA imeongoza tu. Hii trend si sawa logically.
   
 15. Mtuflani

  Mtuflani JF-Expert Member

  #15
  Nov 5, 2010
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 323
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mi naona twendeni mahakama ya kimataifa ushahidi si tunao jamani
   
 16. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #16
  Nov 5, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Mtuflani nakubaliana na wewe kabsaaa.
  Hata mimi naona tumtafute Ocampo anayeshughulikia mgogoro wa Uchaguzi wa Kenya 2007.

  CHADEMA tuna wanasheria makini sana kama Mabere Marando na Tundu Lisu. Tukiwatumia hawa jamaa kesi yetu itawahenyesha CCM mpaka wajute kwanini walichakachua kura zetu.
   
 17. sensa

  sensa JF-Expert Member

  #17
  Nov 5, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa kila hali inaonekana uchakachuaji ndo umempa urais,kwa hiyo Dr ndio rais wa kuteuliwa na huyu aliyetangazwa ni rais wa kuchakachuliwa.
   
 18. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #18
  Nov 5, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  HILI NI SWALA LA WAZI KUWA KURA ZILIIBWA NA KUWEKWA KAMA WANAVYOTAKA WENYEWE,ILA TATIZO WALILOFANYA NI KUTOKUTUMIA AKILI VIZURI ILI KU-BALANCE MAENEO YOTE,HAPO TU NDIO IMEKULA KWAO,WANGEMPA KIKWETE HATA 48% ISINGEKUWA MBAYA SANA,LAKINI WALICHOTAKA ILIKUWA WALAU REDET/SYNOVATE inashabihana....:nono:
   
 19. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #19
  Nov 5, 2010
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Katiba 'yenu' hairuhusu kuhoji matokeo ya urais! Hivyo la msingi ni kuhangaikia mabadiliko ya katiba yatayohakikisha kuwepo kwa tume huru ya uchaguzi na uchaguzi ulio huru na haki. Kung'ang'ania kubishania matokeo ni kupoteza muda - kwa hali ilivyo katiba inawakingia kifua. Wahenga hawakukosea "maji yakishamwagika hayazoleki".
   
 20. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #20
  Nov 5, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Tusimwage maji makusudi alaf tuseme hayazoleki!
   
Loading...