Dr. Slaa, Mnyika na Lema kukamatwa na Polisi wakati wowote kuanzia Leo

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,973
3,901
Taarifa tulizopata wakati tunaekwenda mitamboni zinasema kuwa, jeshi la polisi limeelekezwa kuwakamata viongozi wakuu wa Chadema kwa kile kinachoelezwa kuwa madai yao ya kutaka kuuawa yanaleta mtafaruku kati ya nchi na nchi wahisani.

Mpango huo ulipangwa kutekelezwa wakati wo wote kuanzia jana jumanne. ( Nimenukuu mwanahalis la Leo Juma tano)

My take;
Kama kusingekuwa na kuhofia mtafaruku na wahisani ina maana wangepuuza madai yao? Au wangeendelea na huo mpango wenyewe uliofichuliwa?
 
Hii nchi hii!? enhe wakiwakamata watawaambia nini!? kama wamefanya kosa kisheria mahakama si zipo wazi!? lets wait and see!
 
Taarifa tulizopata wakati tunaekwenda mitamboni zinasema kuwa, jeshi la polisi limeelekezwa kuwakamata viongozi wakuu wa Chadema kwa kile kinachoelezwa kuwa madai yao ya kutaka kuuawa yanaleta mtafaruku kati ya nchi na nchi wahisani. Mpango huo ulipangwa kutekelezwa wakati wo wote kuanzia jana jumanne. ( Nimenukuu mwanahalis la Leo Juma tano)

My take;
Kama kusingekuwa na kuhofia mtafaruku na wahisani ina maana wangepuuza madai yao? Au wangeendelea na huo mpango wenyewe uliofichuliwa?


Wakati unaenda mitamboni wapi? wakati unasema umekopy mwanahalisi?

Huu ni uhandishi gani? ndo tatizo kusoma shule za kata
 
Wajaribu kama LYBIA ajahamia Tanzania. Si wanadai wana JESHI na POLISI haya tuone kama wataeweza UMMA. Washenji sana hawa ma Polisi na Jeshi letu. Ndio maana yakusoma skuli ya KATA kweli haasa wengi wao awana Skuli kabisa ukitaka kujua cheki cheti chao. BURE KABISA SERIKALI HII. TUNAWASUBIRI SANA KWA HAMU WAJARIBU. Naona THE HAGUE inanukia BONGOLAND.
 
Polisi kazi ni kukamata na si kuchunguza, Tumeshakosa imani na jeshi hili la ccm

Mkuu nakubaliana na wewe, Tunataka jeshi la polisi linalowajibika kwa serikali. Jeshi la polisi la serikali litakalotoa ripoti ya kifaa alichowekewa Dr Slaa Dodoma.
Jeshi la Polisi la serikali litakalowakamata watesaji wa Ulimboka,
Jeshi la Polisi la serikali litakalokamata waliomtia tindikali kubenea na mwenzake.
Waliopo ni Jeshi la polisi la m/kiti wa Taifa wa CCM Mr Jakaya M. Kikwete - siyo la Serikal siyo la Rais wa Nchi. Hawa waliopo sina imani nao, wanawajibika kwa CCM.
 
Hii nchi hii!? enhe wakiwakamata watawaambia nini!? kama wamefanya kosa kisheria mahakama si zipo wazi!? lets wait and see!

Mkuu hata hizo mahakama na zenyewe si zimekuwa sehemu ya kuilinda govt iliyoko mahakamani. Kama ungekuwa unaangalia Bunge muda mchache ulopita serikali imeogopa kupitia Bunge kumruhusu Kafulila asilete ushahidi ambao serikali imekiri kuisababishia hasara ktk issue ya Dowans!
 
Mkuu nakubaliana na wewe, Tunataka jeshi la polisi linalowajibika kwa serikali. Jeshi la polisi la serikali litakalotoa ripoti ya kifaa alichowekewa Dr Slaa Dodoma.
Jeshi la Polisi la serikali litakalowakamata watesaji wa Ulimboka,
Jeshi la Polisi la serikali litakalokamata waliomtia tindikali kubenea na mwenzake.
Waliopo ni Jeshi la polisi la m/kiti wa Taifa wa CCM
Mh. Jakaya M. Kikwete - siyo la Serikal siyo la Rais wa Nchi. Hawa waliopo sina imani nao, wanawajibika kwa CCM.

Hapo kwenye red and bolded: Umeweka hilo neno kwa dhamira itokayo moyoni na ukiamini ktk hilo au n mazoea tu. Hebu ondoa hilo neno plz!
 
Kwani wamekataa kwenda Polisi mpaka wakamatwe?Alichokataa Slaa ni kuhojiwa,na si kwenda polisi.
Kwani akifikishwa huko na akakataa kusema chochote watamlazimisha?
 
Raha ya kuwa na chama cha siasa kinachoongozwa kisomi ndiyo hii bwana. Magamba walidhani kuongoza nchi ni sawa na mtu anavyolala na mke chumbani tena wakati wa baridi, na Badooo!
 
Hii nchi hii!? enhe wakiwakamata watawaambia nini!? kama wamefanya kosa kisheria mahakama si zipo wazi!? lets wait and see!

Watatekeleza yale waliyotuhumu kwayo.
Tazama yuaja na mawingu ya mbinguni, na kila jicho litamuona na hata hao waliomchoma.
 
Kwanini wasiwapeleke mahakamani?

Hakuna mahakama ya kisiri mkuu. Huko watatokeza waandishi wa habari na kusambaza uchafu wa serikali unapowekwa wazi. Ndoo maana wanataka mahakama ya polisi, ya kisiri, iwahoji.
CCM hawachomoki piga ua, washauri wenyewe ni akina Zomba, Ritz sasa kuna la maana hapo.
 
Jeshi la Polisi ni jeshi linalolinda usalama wa raia na mali zake, na ieleweke kuwa dhamana waliopewa inatokana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.....
Usipende kuanzisha mada kishabiki ilihali ushahidi unao, nikupe mifano michache inayowafanya watu wenye akili timamu wasiliamini Jeshi la Polisi japo kuwa wapo kwa mujibu wa Sheria.

1. Regnald Mengi alilalamika kwamba Polisi wanataka kumbambikiza mwanaye madawa ya Kulevya aliwataja mpaka majina ya Polisi waandaminizi na kiasi cha pesa walichopewa, cha ajabu si Reginald Mengi aliadhibiwa kwa kusema uongo wala si hao Polisi waandamizi walichukuliwa hatua ilihali Mengi alisema ana ushahidi. Kwa mtu mwenye akili timamu ni lazima ajue kwamba Polisi kweli walihusika ila kuogopa kuchafuka wakaamua kulimaliza hili suala chinichini, kama unadhani nakudanganya hebu jaribu leo Mtaje Polisi yeyote kwa tuhuma kama hizo ilihali si ya kweli utaona kitakachokutokea.

2. Mwakyembe alitoa Taarifa Polisi mapema kabisa kwamba kuna watu wanataka kumdhuru akataja mpaka magari yaliyopangwa kumfanyia hayo madhambi, ikumbukwe pia unapotaja namba za gari inamaanisha umemtaja Muhusika, na Polisi walimwita kwa mahojiano akawapa ushirikiano, lakini cha ajabu wakaendelea kuwasitiri wauaji mpaka wakatimiza adhma yao ambayo ilikwamishwa na madaktari wa India, kibaya zaidi Polisi haohao kupitia kwa Manumba wakachukua Jukumu la madactari wa Mwakyembe kuanza kuzungumzia ugonjwa wa Mwakyembe, unaikumbuka hii ilipelekea mpaka matamko ya Serikali kutofautiana kati ya Waziri wa Afya na Msemaji wa Polisi?

Katika hali kama hii mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi kuendelea kuwaamini Polisi ndiyo maana hata siku moja nyumbani kwangu nikiwa na Tatizo siwezi kupiga simu Polisi, wakishindwa walinzi wangu basi ni bora nife. Nawachukia sana Polisi na the so called Usalama wa Taifa
 
Back
Top Bottom