Ndugu Mwigulu Nchemba ameionya serikali
kuacha kuendekeza anasa, semina na sherehe
wakati wananchi wanaishi maisha ya dhiki.
"Haiwezekani serikali inafanya sherehe kubwa
wakati wanafunzi wanakaa chini na wananchi
hawana huduma ya maji, barabara na umeme.
Hatujawahi kusikia fedha za semina na sherehe
zimekosekana lakini kila siku tunaambiwa fedha
za kuchimbia visima vya maji na kununulia
dawa za hospitali hakuna! Kuna wengine
wanadiriki hadi kufanyia semina nje ya nchi",
alisema Nchemba.
Bwana Nchemba alimuagiza mlipaji mkuu wa
serikali asiwe anaidhinisha fedha za umma kwa
ajili ya sherehe na anasa ambazo hazina tija
katika maendeleo ya wananchi. Alisema
atakayekiuka agizo hilo ajiandae kufutwa kazi.
MAONI YANGU
Nampongeza Bw Nchemba kwa kuwatetea
wanyonge na kukataza matumizi ya ovyo ya
fedha za umma. Serikali imekuwa ikipoteza
fedha nyingi kwenye sherehe nyingi za kipuuzi
huku wananchi wakiishi maisha ya dhiki. Sasa
tutaanza kuona MAISHABORA KWA KILA
MTANZANIA.
Chanzo:RFA