magessa78
JF-Expert Member
- Sep 28, 2009
- 270
- 31
katika facebook yake,Dr Salaa ameandika hivi:
Tunaulizwa kwaninii hatukushiriki kutangazwa au kuapishwa kwa JK
Tungeweza vipi kuhudhuria kutangazwa kwa mshindi au kuapishwa kwa Rais ambaye ametangazwa katika mazingira ya wasiwasi na mchakato mzima? Hatuna tatizo binafsi na Kikwete au hata yeye kuwa Rais, tatizo letu la msingi kabisa ni kuwa mchakato wa utangazaji matokeo ulikuwa mbovu sana kutishia kuaminika kwa matokeo hayo. Kama Kikwete angeshinda kwa asilimia 99 au asilimia 50.01 kwenye mchakato ulio huru, wazi na wa haki tusingelalamika kabisa.
Hivyo, kama tungeshiriki kama watu wanavyopendekeza na kukumbatiana kama walivyofanya wengine tungekuwa tumetuma ujumbe kuwa hatuna matatizo na mchakato mzima wa matokeo. Tungehalalisha vitendo vya tume na watumishi wake kuvuruga uchaguzi.
Tulipanga kuzungumza na waandishi kesho, lakini imeahirishwa kwani kuna mchakato unaoendelea na ambao tunataka kuona utafikia wapi. Tunawasihi wanachama, mashabiki na wapenzi wetu waendelee kutulia wakati huu ili kutupa nafasi ya kuandaa mpango mzuri wa mwitikio wetu.
asanteni.