Dr.Slaa kutoongea na waandishi wa habari kesho jumapili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr.Slaa kutoongea na waandishi wa habari kesho jumapili

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by magessa78, Nov 6, 2010.

 1. magessa78

  magessa78 JF-Expert Member

  #1
  Nov 6, 2010
  Joined: Sep 28, 2009
  Messages: 271
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  katika facebook yake,Dr Salaa ameandika hivi:
  Tunaulizwa kwaninii hatukushiriki kutangazwa au kuapishwa kwa JK

  Tungeweza vipi kuhudhuria kutangazwa kwa mshindi au kuapishwa kwa Rais ambaye ametangazwa katika mazingira ya wasiwasi na mchakato mzima? Hatuna tatizo binafsi na Kikwete au hata yeye kuwa Rais, tatizo letu la msingi kabisa ni kuwa mchakato wa utangazaji matokeo ulikuwa mbovu sana kutishia kuaminika kwa matokeo hayo. Kama Kikwete angeshinda kwa asilimia 99 au asilimia 50.01 kwenye mchakato ulio huru, wazi na wa haki tusingelalamika kabisa.

  Hivyo, kama tungeshiriki kama watu wanavyopendekeza na kukumbatiana kama walivyofanya wengine tungekuwa tumetuma ujumbe kuwa hatuna matatizo na mchakato mzima wa matokeo. Tungehalalisha vitendo vya tume na watumishi wake kuvuruga uchaguzi.

  Tulipanga kuzungumza na waandishi kesho, lakini imeahirishwa kwani kuna mchakato unaoendelea na ambao tunataka kuona utafikia wapi. Tunawasihi wanachama, mashabiki na wapenzi wetu waendelee kutulia wakati huu ili kutupa nafasi ya kuandaa mpango mzuri wa mwitikio wetu.

  asanteni.
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Nov 6, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kunani tena jamaniiiiiiiiiiiiiiii
   
 3. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #3
  Nov 6, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sisi tumetulia tuli kama maji ya mtungini...hakuna matata kwani we sent a very clear message to them
   
 4. d

  deecharity JF-Expert Member

  #4
  Nov 6, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 831
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Thnx alot kwa information... 2peane taarifa mchakato unavyoendelea naamini kila k2 kinaenda kwa evidence ndio mana hamna haraka... People'ssss power.
   
 5. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #5
  Nov 6, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  haina haja kuonekana mnafiki kama Lipumba mbele ya wanajamii. Kama mtu amekuudhi muonyeshe amekuudhi, then hawezi kufanya hivyo tena, kinyume cha hapo huyo si mzima. nashukulu president of United Republic Of Tanzania D. Wilbroad Peter
   
 6. BABU KIDUDE

  BABU KIDUDE JF-Expert Member

  #6
  Nov 6, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,368
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Eh wamesha chakachua tena?
   
 7. B

  Babasean Member

  #7
  Nov 6, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dr W P Slaa, is the president for all us who are the followers of CHADEMA!
  wewe u rais wetu, na ni rais wetu sisi walalahoi na waamka taabani.
  Tunakupenda na tunakujali ndiyo maana hata tulikuchangia Tsh. 350/- zetu kwa sms kupitia simu zetu ili uweze kupata mafuta ya Chopper yako.Huo ndio uliokuwa uwezo wetu sisi wana wa wakulima wa jambe la mkono.
  Tunazidi kufunga na kusali na kuomba ili yeye aliye Mkuu kuliko mkuu wa ulimwengu huu wa giza. ufisadi, wizi, na udanganyifu, akuwezeshe na akupe busara na hekima ya kufanya maamuzi yenye mkono wake wa kutuongoza na kutuonyesha njia iliyo sahihi.
   
 8. c

  chanai JF-Expert Member

  #8
  Nov 6, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 279
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Binafsi nakubalina kabisa na msimamo wa Dr Slaa kukacha sherehe za JK. Hata hivyo nawatakia mazungumzo mema. Mungu awape hekima zaaidi katika hili. Natumaini tutafika mahali pazuri kabisa kwa manufaa ya nchi yetu.
   
 9. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #9
  Nov 6, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nani refa wa mazungumzo haya? Yanazingatia sheria zipi? Ccm wajanja janja sana so awe makini sana
   
 10. nyasatu

  nyasatu Member

  #10
  Nov 7, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  dr dr take ur time,mm binafsi am moreee than patient,acha mafisadi waendelee ku party ushini by the time tunaibuka na ma evidence vitambi vitawashuka na wataiona dunia chungu kama sio kuomba ipasuke waingine
   
 11. K

  King kingo JF-Expert Member

  #11
  Nov 7, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 401
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Inawezekana hawa mafisadi wamekuja na mbinu mpya wanataka kujifanya wanafanya nae mazungumzo ili kupunguza morale ya watu, sio wa kuwaamini sana lakini ngoja tusubiri
   
 12. Ngigana

  Ngigana JF-Expert Member

  #12
  Nov 7, 2010
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 1,259
  Likes Received: 373
  Trophy Points: 180
  Dr., Mungu akupe hekima ktk kipindi hiki na mazungumzo yawe yenye heri! Jambo moja linajulikana kuwa Haki hucheleweshwa na huwa haipotei! Uwe na moyo mkuu, wa TZ wapenda haki na demokrasia ya kweli bado tunakuunga mkono.
   
 13. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #13
  Nov 7, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Good, tunakuheshimu kiongozi wetu. Hatutakuja Kinondoni. Pindi ukiwa tayari, na sisi tutakuwa tayari. Mungu awe nawe Dr. (PhD) Slaa
   
 14. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #14
  Nov 7, 2010
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,596
  Likes Received: 6,757
  Trophy Points: 280
  Je hii ni mbinu ya CCM ya kuzubaisha mambo ili wananchi wasahau mambo ya uchaguzi then baada ya hapo hata Slaa akisema anayoyataka yasiwe na impact kubwa kwa jamii?
   
 15. Mhafidhina

  Mhafidhina JF-Expert Member

  #15
  Nov 7, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Dr. Slaa,

  Kuwa makini sana, kuna vijana na baadhi ya watu ambao wanajitia wapo karibu na wewe kumbe ni watu wanaokusanya taarifa kwa ajili ya kuzipeleka kwa wakuu wao. Wapo wanajaribu kufuatilia kila aina ya mbinu na mikakati mnayopanga haswa wakifikiri kwamba mnampango wa kufanya machafuko...!

  Pia kuwa makini sana, usile wala usinywe vitu ovyo hasa wakati unapokuta vimeandaliwa na watu usiowajua (hii ni kwa ajili ya usalama wako binafsi)...! Matumizi yenu ya simu na mawasiliano muwe nayo makini sana kwani i guess you may be taped sometimes. Wanajaribu sana kufuatilia ni jinsi gani unapta taarifa hizi nzito ambazo zina ukweli mkubwa ndani yake. Hawa jamaa sasa naona wapo hatua kwa hatua kufuatilia nyendo zako zote.
   
 16. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #16
  Nov 7, 2010
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sio kweli Dr. Hajasema hivo bali kasema hivu:- Nawakilisha..Ndugu Watanzania nia na malengo yetu kwa taifa vipo palepale kabla na baada ya uchaguzi. Kuna page mpya ya Chadema ikiwa na lengo la kufuatilia na kuratibu halamashauri zote zinazoongozwa na CHADEMA katika kuhakikisha utendaji wake ni wa ufanisi. Tujiunge huko ili kupata fursa ya kutoa mawazo na kukosoa utendaji wa halamashauri hizi. Tuonyeshe mfano wa yale tuliyokuwa tunayapigania.
  Dr. Willibrord Slaa | Facebook
   
 17. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #17
  Nov 7, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  aaaah Dr...yaani mimi nimekaa kwenye mstari nangoja uzungumze tu....yaani neno lako ndo litaniamuru nifanye nini kupinga wizi wa kura uliofanywa na JK....Mi naapa ntakuwa wa kwanza kufa kueneza ujumbe huu kuwa JK kashinda kwa hila na wizi wa kura
   
 18. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #18
  Nov 7, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Dr Slaa kumbuka unachochea kuni wakati moto unawaka, ulipaswa kuongea na wanachi wako muda huu, kuna maswali mengi yalikuwa yanaihitaji majibu kutoka kwako hasa kipindi hiki, maana baada ya muda utakachoongea kitakuwa hakina nguvu tena
  1) kwa nini hukuhudhuria utangazaji wa Mshindi
  2) kwa nini hukuhudhuria sherehe ya kuapishwa JK
  3) Nini maoni na misimamo yako na Chadema kwa ujumla kuhusu uchaguzi uliopita
  4) wanachama na wapenzi wa Chadema tufanye nini?
   
 19. D

  Dot com Member

  #19
  Nov 7, 2010
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi namuunga mkono Dr. Slaa kwamba asiongee na waandishi wa habari mpaka mchakato unaoendelea ndani ya CHADEMA ukamilike. Aendelee kuwa makini kama siku zote ambavyo amekuwa akifanya. Sisi wapenda amani tunakuombea sana.


   
 20. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #20
  Nov 7, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,748
  Trophy Points: 280
  Dr. Slaa is a born leader and others like JK and Prof. Lipumba are just dedicated followers.................................
   
Loading...