Katibu Mkuu wa Chamacha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa akiwahutubia wananchi wa mji wa Igunga na vitongoji vyake, katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wananchi kwa ushiriki wao katika kufanikisha kesi ya uchaguzi wa jimbo hilo, uliofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Igunga. Aliyekuwa mgombea wa jimbo la Igunga katika uchaguzi mdogo mwaka jana, kupitia Chadema, mwalimu Joseph Kashindye na aliyekuwa meneja wa kampeni, Slyvester Kasulumbai, wakiwasili kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Igunga, ambako kulifanyika mkutano wa hadhara.Picha zote na Joseph Senga)
Kiongozi wa upinzani nchini ambaye pia ni Katibu mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa leo anatarajiwa kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara mjini Igunga kuwashukuru wananchi kwa ushirikiano waliyokionyesha chama chake mpaka pale mahakama ilipotengua ubunge wa CCM ambao haukuwa halali.
Dr Slaa ambaye anaongoza operesheni M4C mkoani Morogoro imemlazimu kuwaacha makamanda wengine huku yeye na baadhi ya maafisa wakielekea Igunga.Kiongozi huyo amefuatana na Mkiti wa chama mkoa wa Tabora Kansa Mbarouk.
Mara baada ya kuunguruma Igunga leo ataondoka kurejea Morogoro ambapo Jumatatu atakuwa mgeni rasmi katika hitimisho la M4C mkoani Morogoro kwa kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara mjini Morogoro,mkutano unaotarajiwa kuutikisa mkoa mzima na kanda ya kati kwa ujumla kutokana na shauku kubwa wananchi waliyo nayo.
Source:Tanzania Daima.
M4c haitawaponyesha mafisadi kamwe!
Viva CDM!!
Hakika Dr Slaa afya yako ni ya uhakika maana kila siku upo barabarani na huchoki angekuwa yule Baba Mwanaasha sasa Hivi Chali
Mpaka wakae mwaka huu.Mungu awatangulie makamanda katika harakati za ukombozi
Hakika huyu ni kijukuu cha mtume....
Usiwasemehe Watanzania jisemehe wewe na Pro-Chadema wenzako...nani ana imani na Dr Slaa.
Mwaka huu lazima ufe kwa ugonjwa wa moyo unafanya kazi ngumu kuliko makuli wa bandarini.