Dr. Slaa kumnadi Magufuli Jumatano

Ukawa bwana! Juzi juzi hapa mlikuwa mnamuona Dk.Slaa ni kichwa cha trein/garimoshi, leo hii mnamugehuzia kibao kwamba Dk.huyo wa uhakika si lolote si chochote na matusi juu, sasa kwa hulka zenu hizi za kukosa msimamo mnabadirika badirika kama monsoon winds, hivi mna mategemeo ya kupigiwa kura na Watanzania ambao hawasukumwi na saikolojia ya fuata MKUMBO ambayo kisayansi ni asili mia 30% tu ya wapiga kura wote?

Wenzenu walisha fanya homework siku nyingi tu,ndio maana wametulia kama maji kwenye mtungi.

Dr Slaa si ni Padre, aliwahi kusema akiwa Rais atamburuza Magufuli mahakamani kwa kuuza nyumba za Serikali kwa bei ya kutupwa, je leo hizo nyumba zimerudishwa? Au Padre alitudanganya? Nape alikua akimdhihaki Dr Slaa kwa kumuita babu kafilisika, je leo ni Kijana Mkakamavu?
Naona ni siasa majitaka tu zikishika kasi kwa sasa Tanzania
 
Amedataaa huyu mzee. Naona hayupo sawa kichwani. Amedhihirisha kuwa hakuna siasa Tanzania. Wote ni Ccm tuu na wengi kama slaa ambao kujitoa kwenye Chama kunawafanya washindwe kuishi. Uishia kutangatanga kama naniii
 
Madhara ya kuoa ukubwani ni hatari sana. Asipoenda ataiona kwenye pichu imetuna tu!!! Aaaahh Jose wewe ni balaa.
 
Dr Slaa si ni Padre, aliwahi kusema akiwa Rais atamburuza Magufuli mahakamani kwa kuuza nyumba za Serikali kwa bei ya kutupwa, je leo hizo nyumba zimerudishwa? Au Padre alitudanganya?

Mkuu wakati nyumba za Serikali zinahuzwa Mh.Sumaya ndie alikuwa Waziri Mkuu na alisema kwamba Mh.Magufuli hana hatia yoyote yeye alikuwa ni mtekelezaji tu wa mahamuzi ya Baraza la Mawaziri, why keep on reinventing the wheel wakati ukweli wa suala hilo limekwisha wekwa wazi na kinara wa UKAWA Mh.Sumaye.

Nape alikua akimdhihaki Dr Slaa kwa kumuita babu kafilisika, je leo ni Kijana Mkakamavu?

At least Mzalendo Nape alitumia lugha ya staha na sio lugha za vijiweni zinazo tumiwa na UKAWA specifically CHADEMA, siwezi kumsemea Nape lakini nafikiri ulikuwa anamaanisha masuala ya siasa na sio kifedha.

Naona ni siasa majitaka tu zikishika kasi kwa sasa Tanzania.

Nakubaliana nawe comments nyingine za kisiasa kwa pande zote mbili hazifai hata kidogo.
 
Slaa atawafilisi tu CCM.
Hana udhawishi tena.Siasa zake za kunanga watu hazina tija.
Watu wanataka umeme na maji.Sio mipasho.
 
Baada ya mambo kuwa magumu ndani ya ccm hasa baada ya kuona nguvu ya lowassa ikizidi kuongezeka kwa kasi, sasa aliyekuwa katibu mkuu wa chadema, Dr. Wilibrod Slaa atamnadi mgombea wa urais wa ccm Dr. Magufuli.

Habari kutoka lumumba zinasema kwamba, awali Slaa ilikuwa atumike kuinadi ACT-Wazalendo lakini ikaonekana kwamba asingeweza kushwawishi wapiga kura katika kipindi hiki cha kampeni kuikubali ACT.

Lengo la kuinadi ACT lilikuwa kupunguza kura za upinzani hasa katika mikoa ya kigoma, tabora, ruvuma, kagera na mikoa ya kaskazini, lkn ikaonekana kwamba bado asingefanikiwa kushawishi wananchi.

Hivyo Dr Slaa atatumika kumnadi magufuli chama ambacho yeye amekuwa akikipinga na kusema tatizo sio mgombea bali mfumo wa chama chake ndio mbovu.
Sasa tunashuhudia Slaa akisimamia asichokiamini.

source: mwanahalisi

Mbona alishasema hatojihusisha na siasa?
 
Tunafukua makaburi
 
Back
Top Bottom