huyu mzee naye anajichanganya.anataka kutuambia kwamba kikwete huwa anazungumzia zaidi chadema kuliko ccm au kuliko mikakati,mafanikio nachangamoto zinazoikabili serikali! aache usanii aisee! au slaa hataki asikie akitajwa au chama chake kikitajwa na kikwete? kuhusu ccm kuchukuwa sera ya kusomesha wanafunzi bure,kwa hiyo kumbe anachotaka slaaa si watanzania wapate nafuu kwa kusomesha watoto bali anachotaka ni kupingana tu hata kama mwenzako anataka kufanya jambo la msingi?Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kutotumia muda mwingi kuvishambulia vyama vya siasa.
Badala yake Dk. Slaa amemtaka Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutumia muda huo kuzungumza jinsi ya kutatua kero za wananchi ili kupunguza ukali na ugumu wa maisha unaowakabili sasa.
Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Mahakama Kuu ya Kanda ya Arusha kuhusiana hoja mbalimbali zilizozungumzwa katika mkutano wa CCM uliofanyika jijini Dar es Salaam juzi.
Akijibu shutuma mbalimbali zilizotolewa katika mkutano wa kuwapokea viongozi mbalimbali wa CCM waliochaguliwa mjini Dodoma, Dk. Slaa alisema katika mkutano huo viongozi wengi wa chama hicho akiwamo Rais Kikwete, walitumia muda mwingi kuelekeza nguvu zao jinsi ya kukabiliana na vyama pinzani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Alisema CCM imeelekeza nguvu zake kujifua ili kukikabili Chadema katika uchaguzi ujao na siyo kuwaeleza wananchi nini watawafanyia ili kuwaondoa katika janga la umaskini.
Aidha, aliwatuhumu viongozi wa CCM kuchukua sera mbalimbali zilizoanzishwa na Chadema ikiwamo ya kusomesha wanafunzi bure kutoka shule ya msingi hadi sekondari.
Aidha, alisema anashangaa uteuzi wa Katibu Mkuu wa ccm, Abdulrahman Kinana kwa madai kwamba siyo msafi.
Source:Nipashe Jumanne
Akijibu shutuma mbalimbali zilizotolewa katika mkutano wa kuwapokea viongozi mbalimbali wa CCM waliochaguliwa mjini Dodoma, Dk. Slaa alisema katika mkutano huo viongozi wengi wa chama hicho akiwamo Rais Kikwete, walitumia muda mwingi kuelekeza nguvu zao jinsi ya kukabiliana na vyama pinzani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Alisema CCM imeelekeza nguvu zake kujifua ili kukikabili Chadema katika uchaguzi ujao na siyo kuwaeleza wananchi nini watawafanyia ili kuwaondoa katika janga la umaskini.
Hapo kwenye red ni kete nzuri kwa CDM.
Chadema wanamnyima usingizi, badala ya kufikiria ni jinsi gani ataondoa rushwa kwenye chama chake, anapoteza muda kuwashambulia chadema.
Ilikuwa asubuhi ikawa jioni, CCM wakaondoka!!!
Maskini babuuuu, pole sana kwa kuikosa ikulu. Cheki ulivyochoka. Umeishiwa mashairi sasa umebaki kujibu hoja za J.K. Mwanzoni ulifikiri ungefanikiwa kwa maandamano ikawa hola, migomo hola, m4c holaaa. Na bado utapanga vingi lakini vitaishia kuwa hola. Pole Dr. Slaa uongo wooote mara makontena ya kura sijui nini, watanzania wameng'amua ujanja na uongo wako uliokubuhu. Utaisoma mzee CCM hiyoooooooooo na bado hadi ujinyon*********e mwaka huu.
Thanx dr Wilbrod..JK utadhani Rais wa Magamba pekee.mtu aige mfumo wa White house.tangu lini Obama kapiga siasa za democratic pale.