Dr Slaa: Kikwete acha kushambulia CHADEMA

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kutotumia muda mwingi kuvishambulia vyama vya siasa.

Badala yake Dk. Slaa amemtaka Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutumia muda huo kuzungumza jinsi ya kutatua kero za wananchi ili kupunguza ukali na ugumu wa maisha unaowakabili sasa.

Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Mahakama Kuu ya Kanda ya Arusha kuhusiana hoja mbalimbali zilizozungumzwa katika mkutano wa CCM uliofanyika jijini Dar es Salaam juzi.

Akijibu shutuma mbalimbali zilizotolewa katika mkutano wa kuwapokea viongozi mbalimbali wa CCM waliochaguliwa mjini Dodoma, Dk. Slaa alisema katika mkutano huo viongozi wengi wa chama hicho akiwamo Rais Kikwete, walitumia muda mwingi kuelekeza nguvu zao jinsi ya kukabiliana na vyama pinzani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Alisema CCM imeelekeza nguvu zake kujifua ili kukikabili Chadema katika uchaguzi ujao na siyo kuwaeleza wananchi nini watawafanyia ili kuwaondoa katika janga la umaskini.

Aidha, aliwatuhumu viongozi wa CCM kuchukua sera mbalimbali zilizoanzishwa na Chadema ikiwamo ya kusomesha wanafunzi bure kutoka shule ya msingi hadi sekondari.

Aidha, alisema anashangaa uteuzi wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwa madai kwamba siyo msafi.

Source: Nipashe Jumanne
 
Thanx dr Wilbrod..JK utadhani Rais wa Magamba pekee.mtu aige mfumo wa White house.tangu lini Obama kapiga siasa za democratic pale.
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kutotumia muda mwingi kuvishambulia vyama vya siasa.
Badala yake Dk. Slaa amemtaka Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutumia muda huo kuzungumza jinsi ya kutatua kero za wananchi ili kupunguza ukali na ugumu wa maisha unaowakabili sasa.
Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Mahakama Kuu ya Kanda ya Arusha kuhusiana hoja mbalimbali zilizozungumzwa katika mkutano wa CCM uliofanyika jijini Dar es Salaam juzi.
Akijibu shutuma mbalimbali zilizotolewa katika mkutano wa kuwapokea viongozi mbalimbali wa CCM waliochaguliwa mjini Dodoma, Dk. Slaa alisema katika mkutano huo viongozi wengi wa chama hicho akiwamo Rais Kikwete, walitumia muda mwingi kuelekeza nguvu zao jinsi ya kukabiliana na vyama pinzani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Alisema CCM imeelekeza nguvu zake kujifua ili kukikabili Chadema katika uchaguzi ujao na siyo kuwaeleza wananchi nini watawafanyia ili kuwaondoa katika janga la umaskini.
Aidha, aliwatuhumu viongozi wa CCM kuchukua sera mbalimbali zilizoanzishwa na Chadema ikiwamo ya kusomesha wanafunzi bure kutoka shule ya msingi hadi sekondari.
Aidha, alisema anashangaa uteuzi wa Katibu Mkuu wa ccm, Abdulrahman Kinana kwa madai kwamba siyo msafi.

Source:Nipashe Jumanne
huyu mzee naye anajichanganya.anataka kutuambia kwamba kikwete huwa anazungumzia zaidi chadema kuliko ccm au kuliko mikakati,mafanikio nachangamoto zinazoikabili serikali! aache usanii aisee! au slaa hataki asikie akitajwa au chama chake kikitajwa na kikwete? kuhusu ccm kuchukuwa sera ya kusomesha wanafunzi bure,kwa hiyo kumbe anachotaka slaaa si watanzania wapate nafuu kwa kusomesha watoto bali anachotaka ni kupingana tu hata kama mwenzako anataka kufanya jambo la msingi?
 
Akijibu shutuma mbalimbali zilizotolewa katika mkutano wa kuwapokea viongozi mbalimbali wa CCM waliochaguliwa mjini Dodoma, Dk. Slaa alisema katika mkutano huo viongozi wengi wa chama hicho akiwamo Rais Kikwete, walitumia muda mwingi kuelekeza nguvu zao jinsi ya kukabiliana na vyama pinzani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Alisema CCM imeelekeza nguvu zake kujifua ili kukikabili Chadema katika uchaguzi ujao na siyo kuwaeleza wananchi nini watawafanyia ili kuwaondoa katika janga la umaskini.

Hapo kwenye red ni kete nzuri kwa CDM.
 
Chadema wanamnyima usingizi, badala ya kufikiria ni jinsi gani ataondoa rushwa kwenye chama chake, anapoteza muda kuwashambulia chadema.

Ilikuwa asubuhi ikawa jioni, CCM wakaondoka!!!
 
CCM hawajui wajibu wa chama tawala.Ndio maana kwao kila baada ya uchaguzi mkuu wao wanajipanga kwa uchaguzi unaofata bila kujiuliza wajibu wao. Dr kasema kweli kuwa wanajisahau
 
Chadema wanamnyima usingizi, badala ya kufikiria ni jinsi gani ataondoa rushwa kwenye chama chake, anapoteza muda kuwashambulia chadema.

Ilikuwa asubuhi ikawa jioni, CCM wakaondoka!!!

mwanzoni alisema chama cha msimu anakumbuka kumekucha mchicha umekua na kuwa mbuyu ....
 
Nilifuatilia sana hotuba za wajumbe na viongozi wa ccm ktk mkutano mkuu. Pamoja na hotuba zilizotolewa na viongozi ktk mapokezi pale kinondoni, yote ilikuwa ni kulalamika tu juu ya rushwa ktk chama na mikakati ya kuendelea kushika dola ktk uchaguzi wa 2015, lakini hawkuongelea ni vipi watatatua matatizo ta uchumi kwa watanzania, kubuni ajira kwa vijana, kukuza uchumi unaodorora kila siku na kupambana na ufisadi uliokithiri ktk nchi. Ambao unateketeza karibu 80% ya mapato yote ya nchi na kubakiza 20% tu kwa maendeleo. Je nchi itaenda mbele kwa mtindo huo?.
Nchi hii inahitaji kiongozi shupavu na jasiri kuitoa hapa ilipo, mithili ya Marehemu Sokoine.
Hebu fikiria leo hii kwa katiba tuliyonayo ambayo watanzania wanaipigia kelele kuwa ibadilishwe, inampa kiongozi wa nchi madaraka makubwa sana, kiasi cha kutoulizwa, kuhojiwa au kushitakiwa. Lakini anashindwa kuchukua maamuzi magumu kuinusuru nchi katika wimbi la umaskini na kupambana na maovu bila kumwangalia mtu usoni.. Je itakapoundwa katiba ingine itakayokuwa na checks and balances na tukawa na kiongozi wa aina hii, atafanya kazi kweli?. Tujiulize na tutafute majibu.
 
Maskini babuuuu, pole sana kwa kuikosa ikulu. Cheki ulivyochoka. Umeishiwa mashairi sasa umebaki kujibu hoja za J.K. Mwanzoni ulifikiri ungefanikiwa kwa maandamano ikawa hola, migomo hola, m4c holaaa. Na bado utapanga vingi lakini vitaishia kuwa hola. Pole Dr. Slaa uongo wooote mara makontena ya kura sijui nini, watanzania wameng'amua ujanja na uongo wako uliokubuhu. Utaisoma mzee CCM hiyoooooooooo na bado hadi ujinyon*********e mwaka huu.
 
Natafuta ile orodha ya ahadi za CCM za 2010 nianze kuzidadavua ili nijue CCM ni wakweli ama waongo kwa kiasi gani kabla hatujafika 2014
 
Hata kusafirisha Twiga na Pembe Za ndovu na ni uongo!

Maskini babuuuu, pole sana kwa kuikosa ikulu. Cheki ulivyochoka. Umeishiwa mashairi sasa umebaki kujibu hoja za J.K. Mwanzoni ulifikiri ungefanikiwa kwa maandamano ikawa hola, migomo hola, m4c holaaa. Na bado utapanga vingi lakini vitaishia kuwa hola. Pole Dr. Slaa uongo wooote mara makontena ya kura sijui nini, watanzania wameng'amua ujanja na uongo wako uliokubuhu. Utaisoma mzee CCM hiyoooooooooo na bado hadi ujinyon*********e mwaka huu.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom