Jatropha
JF-Expert Member
- Apr 9, 2009
- 1,151
- 199
Tokea mwaka 1992 mfumo wa vyama vingi ulipoanza hapa Tz, vyama vya upinzani vimekuwa vikipokezana kuwa na nguvu na kuongoza upinzani hapa nchini. Kwanza ilikuwa ni zamu ya NCCR Mageuzi 1995-2000, ikafuata zamu ya TLP mwaka 2000, CUF 2005. Sasa imekuja zamu ya CHADEMA 2010.
Moja ya makosa ambayo yalipelekea vyama hivi kuporomoka toka juu hadi chini katika chaguzi zilizofuata ni viongozi wa chama kushikilia nafasi za ubunge hivyo kutumia muda mwingi katika majukumu ya kibunge na kusahau majukumu ya kukijenga chama ndani ya kipindi cha miaka mitano iliyofuata.
Safari hii angalau Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilabroad Slaa hakuingia bungeni, na nilifarijika zaidi pale nilipomsikia akidai kuwa hana mpango wa kwenda bungeni kupitia chaguzi ndogo ili apate nafasi ya kukijenga chama hadi ngazi za chini.
Kila kukicha nakutana na watu wa kada mbali mbali wazee, vijana, wanawake n.k kati ya 5-10 wanaohitaji kadi za CHADEMA. Lakini hawafahamu watazipata wapi au namna ya kadi hizo kupatikana. Wimbi hilo limeongezeka maradufu baada ya matukio ya mauaji ya Arusha na maandamnao ya kanda ya ziwa.
Hii inashiria kuwa bado CHADEMA haijaanza kazi ya kujijenga kwenda nagazi ya chini hata pale watanzania walipoonyesha kukikubali kwa kukipatia kura za uraisi, ubunge na udiwani
Hivyo nachukua nafasi kutoa ushauri kwa Dr Slaa na viongozi wote wa ngazi ya taifa, mikoa, wilaya n.k kubuni mikakati ya kukijenga chama kwenda ngazi ya chini badala ya watu wote kujirundika makao makuu kusubiri nini viongozi wa kitaifa watapanga na kutekeleza kwa kuwa mipango inayotoka makao makuu inaambatana na malipo ya posho n.k.
Ni wajibu wa wabunge walioshinda kuchangia gharama za uendeshaji ofisi za cahama katika majimbo yao ndani za Kata na Matawi ili anagalau watendaji wa chama waweze kukaa ofisini kufanya kazi za chama.