Dr Slaa jenga chama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr Slaa jenga chama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jatropha, Mar 17, 2011.

 1. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Tokea mwaka 1992 mfumo wa vyama vingi ulipoanza hapa Tz, vyama vya upinzani vimekuwa vikipokezana kuwa na nguvu na kuongoza upinzani hapa nchini. Kwanza ilikuwa ni zamu ya NCCR Mageuzi 1995-2000, ikafuata zamu ya TLP mwaka 2000, CUF 2005. Sasa imekuja zamu ya CHADEMA 2010.

  Moja ya makosa ambayo yalipelekea vyama hivi kuporomoka toka juu hadi chini katika chaguzi zilizofuata ni viongozi wa chama kushikilia nafasi za ubunge hivyo kutumia muda mwingi katika majukumu ya kibunge na kusahau majukumu ya kukijenga chama ndani ya kipindi cha miaka mitano iliyofuata.

  Safari hii angalau Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilabroad Slaa hakuingia bungeni, na nilifarijika zaidi pale nilipomsikia akidai kuwa hana mpango wa kwenda bungeni kupitia chaguzi ndogo ili apate nafasi ya kukijenga chama hadi ngazi za chini.

  Kila kukicha nakutana na watu wa kada mbali mbali wazee, vijana, wanawake n.k kati ya 5-10 wanaohitaji kadi za CHADEMA. Lakini hawafahamu watazipata wapi au namna ya kadi hizo kupatikana. Wimbi hilo limeongezeka maradufu baada ya matukio ya mauaji ya Arusha na maandamnao ya kanda ya ziwa.

  Hii inashiria kuwa bado CHADEMA haijaanza kazi ya kujijenga kwenda nagazi ya chini hata pale watanzania walipoonyesha kukikubali kwa kukipatia kura za uraisi, ubunge na udiwani

  Hivyo nachukua nafasi kutoa ushauri kwa Dr Slaa na viongozi wote wa ngazi ya taifa, mikoa, wilaya n.k kubuni mikakati ya kukijenga chama kwenda ngazi ya chini badala ya watu wote kujirundika makao makuu kusubiri nini viongozi wa kitaifa watapanga na kutekeleza kwa kuwa mipango inayotoka makao makuu inaambatana na malipo ya posho n.k.

  Ni wajibu wa wabunge walioshinda kuchangia gharama za uendeshaji ofisi za cahama katika majimbo yao ndani za Kata na Matawi ili anagalau watendaji wa chama waweze kukaa ofisini kufanya kazi za chama.
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ni kweli kuna haja ya kutafuta uungaji mkono zaidi kwa kupata wanachama wapya na hai pale ambapo kuna hari ya wananchi wanahitaji wanataka.
   
 3. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kwanza hizo ofisi wanazo? Kipindi cha uchaguzi mwaka jana nilibahatika kuwa mkoani Kilimanjaro, nikabahatika kutembelea kata ya Korongoni kujionea mchakato wa uchaguzi, kwa macho yangu nilimuona bwana Ndesamburo akifungua ofisi ya tawi ya CDM katika mtaa wa Wireless kwenye duka la mtu nilishangaa sana, dukani kwa mtu unafungua ofisi ya chama kikubwa kama CDM?

  Taarifa nilizopata ni kwamba duka hilo limefungwa kwa maana mtaji umekwisha je na ofisi bado iko? Na nini mpango uliopo? Kimsingi CDM wanapaswa kujijenga kwa sasa na si kujibizana na CCM, huwezi ku-assume kwamba utachukua nchi ili hali huna ofisi za kutosha!

  CDM itumie rasilimali watu iliyo nayo kuchangia gharama za ujenzi wa ofisi ama kukodisha majengo mbalimbali, hamuwezi kujifanya mnaipenda CDM wakati mnakuwa wagumu kuichangia! You must change
   
 4. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nakubaliana nawe 100%. Pamoja na mkakati wa maandamano ya kuhamasisha umma nchi nzima, uwekwe mkakati katika ngazi za mkoa na wilaya jinsi ya kuimarisha chama n=vijijini ili kote kuwe na matawi na ofisi zenye watendaji wake sasa!! muda wa kujiimarisha ni sasa.
   
 5. F

  Froida JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  CHADEMA inatakiwa iwe chama ambacho ni Community based yaani kiwe nawafuasi wengi zaidi ambao waanaagaliwa na kiongozi anayekuwa wilayani hii kazi yakufungua matawi kila mahala ni gharama sana kiuendeshaji lakini wanaweza wakawa na waaumini wa CHADEMA ambao wanakuwa kama community supporters wa chama.

  Wananchi wanawafahamu kwa kusaidia kusambaza kadi kwa wananchi, taarifa za chama na labda wanawezeshwa kwa posho na hao wanaweza wakawa wanaratibu na vikao vya chama na hata uongozi wakijamii, matawi gharama sana, yaani namaanisha wanaweza wakawa na mfumo tofauti na mifumo tuliyoizoea ya ofisi za chama lakini ikawa na extension supporters
   
 6. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  pia chadema inapaswa iajiri wasomi katika ngazi ya mkoa na wilaya ambao watafanya kazi ya chama katika ngazi hiyo,kazi ya ukombozi sio kitu cha mzaha na cha kutegemea watu wakujitolea! lazima vijana wasomi waajariwe,wawezeshwe katika mambo mbalimbali na watakuwa responsible kutumikia chama na pia kuwe na zonal coordinator ambaye atakuwa na kazi ya kufatilia maendeleo ya chama katika zone yake!
   
 7. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  sasa hapa mkuu tupo pamoja saana KWENYE UKWELI NI UKWELI MKUU NA UKWELI UTABAKI DAIMA!
  HEKO KASHAGA!!!
   
 8. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Swala la Ofisi ni very expensive kwa sasa, hapo walipofikia CCM wote tunajua wamefanyaje. hata wakiweka ofisi nyumbani kwa mtu let them go ahead.
   
 9. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Si busara kudhani kuwa muundo wa CCM uwe copy pasted Chadema. It wont work. Tunazoziita ofisi za CCM ni mali ya serikali. Kuwa na muundo wa Taifa-Mkoa-wilaya-tarafa- Kata-Kijiji- Kitongoji-Balozi nyumba kumi/mjumbe ni wa ki-CCM na ukitaka vyama vyote viwe muundo huu haiwezekani.
   
 10. Kagemro

  Kagemro JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 465
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Mkuu, ofisi siyo kitu cha kwanza kukimbilia.

  Hata hizi za CCM unazoziona nyingi zilitaifishwa miaka ile, swala ni kujenga chama ndilo la msingi.
   
 11. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #11
  Mar 17, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Mimi kwa mtazamo wangu nadhani maandamano ndio ya msingi kwa muda huu, tuandamane kisha tupige picha za umati wa watu waliofika kwenye maandamano tuziweke hapa jamvini, wabunge wetu makini akina regia wata tusaidia sana katika hili.
   
 12. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #12
  Mar 17, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Kumbe Kashaga ikifika jioni unakuwaga na akili eeeh??nahisi mchana unatumia internet ya mafisadi, na jioni unatumia net yako private,manake upupu unaoandika mchana ukionwa na hao jamaa huna chako.
   
 13. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #13
  Mar 17, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Shamba la bibi sizinga
   
 14. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #14
  Mar 17, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Sijakusoma bado Sigma....shamba la bibi ndilo lipi hapo?
   
 15. Amigo

  Amigo Senior Member

  #15
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 150
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  Kwa hili lazima CDM waliangalie lazima kujipanga kuweza kuwa na ofisi au coordination ya njia moja au nyingine sio lazima kufata njia ya CCM kwani Ofisi nyingi ni kweli zilitaifishwa na zingine zilijengwa kipindi cha chama kimoja na watanzania wote walichangia na pengine kukatwa kwenye mishara yao, kwa hiyo cha msingi ni kutizama namna ya kujiimarisha kwa strategy.
   
 16. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #16
  Mar 18, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Great umetoa mawzo tofauti ambayo kwa kweli yanastahili kufanyiwa tafakuri ya kina. Hususan umeweka msisitizo katika suala la gharama za uendeshaji wa ofisi. Can you share with us some of the successful organisation ambazo zinztumia mfumo unoaupendekeza?
   
 17. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #17
  Mar 18, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Tangu hapo maduka, ofisi n.k nyingi zipo katika makazi ya watu. Hata maduka mengi Kariakoo yapo katika makzi ya watu. Lakini ofisi tunayozungumza hapa ni zaidi ya majengo.
   
 18. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #18
  Mar 18, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Kwa kuwa uchaguzi ufanyika kuwapata viongozi katika nganzi hizo ambazo hadi sasa zipo kikatiba, sula la kuw ana ofisi/watendaji katika ngazi hizo haliepukiki
   
 19. MFUKUZI

  MFUKUZI JF-Expert Member

  #19
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 932
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  si lazima chadema kikaiga kila kitu kutoka ccm, kwanza lazima ukubali kuendesha chama kwa maana ya kuwa na ofisi kila kata shughuli yake si ya kitoto. Ccm wenyewe pamoja na kutumia majengo yaliyojengwa na watz kipindi cha chama kimoja, bado wanapya. Lazima chadema kiwe makini zaidi kwa mfumo utakao kiwezesha kujitanua kwa makini. Nccr walifungua matawi mengi sana kipindi kile yako wapi sasa hivi. So lazima chadema wawe makini.
   
 20. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #20
  Mar 18, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  mawzo yako mazuri, usuri wako ni upi kwa kuwa hivi sasa watu wengi wanahataji kadi za CDM lakini haijulikani wapi pa kuzipata?
   
Loading...