The Khoisan
JF-Expert Member
- Jun 5, 2007
- 15,393
- 12,977
Kwanza hizo ofisi wanazo? Kipindi cha uchaguzi mwaka jana nilibahatika kuwa mkoani Kilimanjaro, nikabahatika kutembelea kata ya Korongoni kujionea mchakato wa uchaguzi, kwa macho yangu nilimuona bwana Ndesamburo akifungua ofisi ya tawi ya CDM katika mtaa wa Wireless kwenye duka la mtu nilishangaa sana, dukani kwa mtu unafungua ofisi ya chama kikubwa kama CDM?
Taarifa nilizopata ni kwamba duka hilo limefungwa kwa maana mtaji umekwisha je na ofisi bado iko? Na nini mpango uliopo? Kimsingi CDM wanapaswa kujijenga kwa sasa na si kujibizana na CCM, huwezi ku-assume kwamba utachukua nchi ili hali huna ofisi za kutosha!
CDM itumie rasilimali watu iliyo nayo kuchangia gharama za ujenzi wa ofisi ama kukodisha majengo mbalimbali, hamuwezi kujifanya mnaipenda CDM wakati mnakuwa wagumu kuichangia! You must change
CCM wana ofisi nyingi zilizojengwa na wananchi. Mali nyingi za CCM ni na umma ila CCM wameng'ang'ania.
Back to the point, Chadema hawatakiwi kufungua ofisi nyingi kama CCM ili wakubalike. Kama walivyokwisha sema watu wengi tu hapa JF, huo mtindo wa ofisi za matawi, nyumba kumi ni mfumo wa kijamaa ambao sasa umepitwa na wakati. Chadema inabidi waje na strategy mpya ambayo itawahakikishia support toka kwa wananchi. CCM wenyewe pamoja na kudai wana wanachama 5 million bado inabidi waalipe watu kuattend mikutano, kuwasafirisha, kuwalisha na bado inabidi wapate ushindi wa mezani kutoka NEC.