Dr. Slaa in Tunduma (photo)

Dr. Slaa in Tunduma (photo)

Ni balaa, Juzi nilipita maeneo hayo nikielekea vijiji vya sumbawanga wimbo pekee uliokuwa unasikika ni slaa slaa Dr :decision:

Jiografia yangu imekaa vibaya, kwenda Sumbawanga unapitia Tunduma?
 
CCM (Makamba na Jakaya) watajilaumu wenyewe - we're up - ready for 2010 CHANGES. Sera za kofia, fulana na buku kumi kumi zimeshapitwa na wakati.
 
Mkubwa SIKONGE una update yoyote huko Jimboni kwetu? nilipiga simu majuzi nikaongea na watu wawili watatu hivi wanasema for the first time wanakipigia chama cha upinzani kwa sababu wameshamchoka mgombea wa CCM, miaka KUMI bila maendeleo yoyote jimboni.

Kama una news zozote kuhusu uchaguzi please!!
 
Hiki si chama cha wakulima na wafanyakazi. Wakulima wanafukuzwa kwenye ardhi zao, na wafanyakazi wanatishiwa kung'olewa ngeu.!
:llama:
 
kinamama_tunduma.jpg

Sehemu ya maelfu ya wakazi wa mji wa Tunduma, wakipunga mikono kuashiria kumpokea mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Tunduma, ambako alihutubia mkutano wa kampeni

slaa_in_tunduma.jpg

Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Tunduma, katika mkutano wake wa kampeni, kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Tunduma

huo ndo mpango mzima
 
Nipo magotini nikumuomba Mungu na kusambaratisha roho zote chafu, ili watanzania hawa waliokataa kudanganyika wamchague Dr Slaa,siku ya tarehe 31/10/2010, baada ya kuchagua wabaki maeneo waliyopigia kura kushinikiza matokeo halali kisha washangalie ushindi wa mwanamabadiliko huyu, Dr Slaa, Silaha ya ukombozi Tanzania.
 
Hivi hawa NEC wakimtangaza JK ndio mshindi, ataongoza watu gani? Mbona kila kona hakuna anayemuhitaji?
 
Mwaka huu ukishindwa tena basi UKAWA!

Mwaka huu ushindi uko wazi kabisa pamoja na propoganda za CCM kuwa kakosa mvuto. Kama kakosa mvuto ni kwa wanaCCM baada ya kuwapa kibondo kikali 2010 na sasa wanamwogopa kama umeme na siyo wananchi.
 
Back
Top Bottom