nilimsikia Tundu Lissu alipokuwa anaonge na mwandishi wa habari kwa njia ya simu. Binafsi nimeshaganzwa na namna ambavyo alijibu maswali ya mwanahabari yule. Anaposema kuwa Kamati Kuu ilishampitisha Dr slaa tangu mwezi January na kurudia tena mwezi April, hapa anatoa tena kuwa kuna ubabahishaji wa democracy ndani ya Chadema kwa kukiukwa kwa katiba ya Chadema maana utaratibu wa kumpata mgombea haukufuatwa maana ilipaswa kuwe na uwazi kila mwanachama kugombea kwa kuchukua fomu kisha vikao husika vya chama kupitisha kwa kupiga kura. Lakini pia anatupa maswali kama tangu mwezi January Slaa alipitishwa na Kamati Kuu, je ni kwan nn mwezi July waliitisha mwanachama anayetaka kugombea achukuwe form ya urais ili hali tayari walikuwa na mgombea tayari? Hapa wanakosa hoja ya Kusema Lowasa alionewa na mchakato wa kumpata rais ndani ya CCM maana nao walishafanya hayo mapema kama kweli mwenyekiti alifika kikao na majina take mfukoni. Pili anaposema kuwa mara baada ya kumpitisha lowasa Dr Slaa alitupiwa vitu njee na mkewe maaana tatizo ni ufirst lady. Sasa hapa anatupa maswali ya kujiuliza kama dokta slaa alifukuzwa na mkewe baada ya slaa kunyimwa urais na huku kuna Picha walisambaza wakionyesha wazee wa baraza la wazee Chadema wakiwa nyumbani kwa Dr slaa pamoja na mkwewe na kueleza umma kuwa dokta amekubali kurudi kuongeza nguvu ukawa na kusema kuwa alikuwa anapanga mikati ya ushindi na kipindi hiko alikuwa likizo, je wazee wale walienda nyumbani kwa Dr slaa kumwombea msamaha ili mkewe akubali kuendelea kuishi na Dr Slaa?
Kimsingi Lissu alipaswa kujibu hoja zilimtaja yeye.
Kwa mfano Dr slaa alisema kuwa kulikuwa na kikao cha watu wanne yaani Slaa, Mbowe, Lissu na Gwajima wakibishana kuhusu kama Lowasa ni mtaji au mzigo kwa Chadema. Sasa alipaswa ama akubali au akanushe uwepo wa kikao hicho. Na kama kilikuwepo na mazungumzo yalikokuwa ya kizungumzwa ni tofauti na aliyosema Slaa atuambie ni mazungumzo yapi ni sahii.
Mwisho nitoe rai kwa viongozi wa Chadema kukaa na kutafakari namna bora ya kumjibu Dr Slaa kwa hoja na sio majibu mepesi kwa hoja nzito. Pia baada ya uchaguzi mjitathini upya maana sasa kwa kipindi kilichobaki hakuna muda wa kujikosoa
By Kennedy Peter Chilala
Mtanzania mzalendo na mwanachama wa CCM