Dr. Slaa, Hapa sijakuelewa ulichotaka kukimaanisha...

Dr. Slaa, Hapa sijakuelewa ulichotaka kukimaanisha...

Atubela

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2011
Posts
749
Reaction score
854
Jana wakati umehitisha kikao na waandishi wa habari, tamko lako la kwanza ulilolitoa ni "KULAANI" vurugu zilizotokea bungeni juzi. Bahada ya kuongea sana bila kuwataja hao unaowalaani, ukamalizia maongezi yako kwa "KUWAPONGEZA" waheshimiwa wabunge ulioanza kwa kuwaani kwa kufanya vurugu bungeni.

Katika hali ya kawaida kabisa usingeanza na "KULAANI" Hii inaonyesha kabisa kwamba kuna vitu vimefanyika ambavyo si vizuri vilivyotakiwa kukemewa na jamii yote kwa ujumla. na wewe ukaona bora uungane na jamii kulaaani matendo maovu, Hapo swali langu kwako "Hao unaowalaani ni kina nani?"

Pia kuna hili la "KUPONGEZA" Hii inaonyesha kabisa kwamba kuna vitu vimekufurahisha, vizuri na vyenye manufaa na wewe kama kiongozi mkubwa wa chama ukaamua kupongeza na hapo swali langu kwako "Hao uliokuwa unawapongeza ni kina nani?"

 
Mie naona mkuu wangu Dr. Slaa! ni bora ungefunguka tu moja kwa moja kuwa unawaunga mkono wabunge wako, kuliko kuwa na sura mbili tofauti "two in one" au "Ndimimbili" (Mnafiki).
 
Uwendawazimu na madeni yasiyolipika humfanya binadamu kuwa mwehu kama wewe...kalagabaho
 
Ipo hivi wakuu aliwalaani wabunge dhaifu wa ccm na serikali yao inayotufanya mandondocha na aliwapongeza wabunge wake kwa kazi nzuri ya kushupaa na upuuzi wa maccm
 
Kazi kweli kweli, unaanzisha post alafu unachangia mwenyewe. Ni sawa na kujitekenya na kucheka. Hata mmeya huwa na Pollination.
 
Unalipwa shilingi ngapi kuleta post za kijinga hivi?
 
Viroba kitu kimoja kibaya sana.....
Haya ni maswali kweli anayoweza kuuliza great thinker???
 
Kama humuelewi Daktari nenda kwa waganga wa kienyeji utawaelewa maana lugha za matunguli ndio muafaka kwako!
 
Ipo hivi wakuu aliwalaani wabunge dhaifu wa ccm na serikali yao inayotufanya mandondocha na aliwapongeza wabunge wake kwa kazi nzuri ya kushupaa na upuuzi wa maccm

Akili ndogo haziwezi ana hiyo. Kuna watu humu kwenye literature walitoka kapa.
 
Mie naona mkuu wangu Dr. Slaa! ni bora ungefunguka tu moja kwa moja kuwa unawaunga mkono wabunge wako, kuliko kuwa na sura mbili tofauti "two in one" au "Ndimimbili" (Mnafiki).

Naona unatamani post zitakazo fuatia zifanane na hii.. Kama umethubutu kuweka uzi na kuijibu kwa kutumia same ID tutegemee fake IDs katika mfululizo wa comments zitakazokuwa na mawazo kama yako!
 
Babu kuchanganya maneno ni matatizo ya umri na msongo wa mawazo.
 
Njaa ukiiendekeza sana unaweza kumtukana mama ako kwa kulpwa ujira mdogo.
 
Ili Vurugu itokee lazima kuwe na pande mbili. Mleta vurugu na Mfanyiwa vurugu

Vur
ugu za Bungeni:

kiini cha vurugu zile ni kiti cha speaker kuonekana kutotenda haki kwa mtoa hoja pamoja na taratibu kujulikana hoja imezimwa ndivyo sivyo hivyo watoa hoja wakapatwa na jazba. Kumbuka kuna rufaa za maamumuzi ya namna hiyo zimekatwa zidi ya kiti hicho bila kusikilizwa mwaka wa tatu sasa.

Kujibu maswali yako:

Mfanya vurugu ni kiti cha speaker na wabunge wake - hivyo walipaswa kukemewa kwa kusababisha vurugu

Katika hali ya kibinadamu (siku zote ukinyimwa haki yako kuna level ya uvumilivu ikifika mwisho lazima kuna reaction) walioreact baada ya kuonewa kwa muda mrefu ni wabunge hivyo waliamua kuchukua hatua (walipaswa kupongezwa kwa ujasiri wa kukataa kuendelea kuonewa.


Hitimisho:
Dr. Slaa yupo Sahihi kwa sababu amekemea upande wa unyanyasaji (wasababishaji wa vurugu) lakini ameupongeza upande (wabunge wa upinzani) kwa kukataa kuendelea kuonewa.


Swali kwa mleta MADA, Je Dr Kakosea wapi?
 
Back
Top Bottom