Dr. Slaa: Hakuna Uoga Wowote Juu ya Lowassa

Dr. Slaa: Hakuna Uoga Wowote Juu ya Lowassa

Nampa pole Dr. Slaa....
kashauona MOTO WA CCM THRU LOWASSA.....kaona vijana na wana CDM wengi ni TEAM LOWASSA...kaanza kushangaa ni nn hiki...!?? Akina #Ben Saanane na wengi CDM ni LOWASSA TU KWA URAIS....naona Dr. Slaa kaanza kuogopa mno, sio kawaida yake kutoa kauli za kujihami hivi....nategemea na yeye atajiunga kumpigia kampeni Lowassa....!!!

Soon, utasikia Dr. Slaa akisema, namkubali Lowassa, ila CCM siipendi, ndio hapo sasa, Dr. Slaa kashamezwa na UMAARUFU WA LOWASSA....simsikii, simuoni, haonekani ktk magazeti wala mitandao...kamalizwa kabisa.....CCM thru Lowassa ni MOTO MKUBWA..!!

keep watching...!!!
Labda amuofie nakule kutetemeka jukwani
 
Hakuna uoga wowote juu ya Lowassa au CCM kutaka Urais. Wanaosema kuna uoga wanapotosha ukweli. Kuna mshangao tu, kwamba "wana lipi jipya"?
Source😀r Slaa Tweet!
Katibu mkuu Chadema!
Ungeuliza ungejibiwa siyo account ya Dr. Slaa hiyo
 
Nampa pole Dr. Slaa....
kashauona MOTO WA CCM THRU LOWASSA.....kaona vijana na wana CDM wengi ni TEAM LOWASSA...kaanza kushangaa ni nn hiki...!?? Akina #Ben Saanane na wengi CDM ni LOWASSA TU KWA URAIS....naona Dr. Slaa kaanza kuogopa mno, sio kawaida yake kutoa kauli za kujihami hivi....nategemea na yeye atajiunga kumpigia kampeni Lowassa....!!!

Soon, utasikia Dr. Slaa akisema, namkubali Lowassa, ila CCM siipendi, ndio hapo sasa, Dr. Slaa kashamezwa na UMAARUFU WA LOWASSA....simsikii, simuoni, haonekani ktk magazeti wala mitandao...kamalizwa kabisa.....CCM thru Lowassa ni MOTO MKUBWA..!!

keep watching...!!!

Akili zako zakukariri ndio zimeishia hapo pole b7
 
Maswali ya msingi kwa Mh.Lowasa -
1. Gazeti la raia mwema la novemba 2010
liliripoti na kuonesha picha ya nyumba ambayo
familia yako inamiliki uingereza. Ukasema ni ya
mwanao, je kwa nchi masikini kama ya kwetu,
ni sahihi kwa kiongozi wa UMMA kumiliki
nyumba kubwa ya kifahari nje ya nchi?
2. Mkapa alipounda baraza jipya la mawaziri
mwaka 1995 alikuacha, wengi wanasema kuwa
Nyerere alimuambia asikupe hata uwaziri, Je
kwanini mwalimu alikukataa???
3. Tangu mwaka 1994, zaidi ya miaka ishirini
sasa (20 years), Afrika kusini imekuwa
ikikodisha nyumba yako masaki kama ubalozi
wake, kuna tetesi kwamba huko nyuma
walitaka kuhama lakini wakaogopa kuihama
nyumba inayomilikiwa na kiongozi mkuu, na
kulikuwa na tetesi kwamba wanataka kuhama
lakini wanatishiwa.
Ni kiasi gani cha fedha umepata kwa zaidi ya
miaka 20 ya kukodisha nyumba hiyo???Je kiasi
hicho kimeripotiwa kwenye fomu ya maadili????
4. Kuna maelezo kwamba nyumba hiyo ya
,masaki ambayo mzee mandela alikuja mwaka
1994 kuufungua ubalozi mpya wa afrika kusini
ndicho chanzo kikuu cha mwalimu kusema
inakuwaje kijana wa miaka 41, akiwa mtumishi
wa umma maisha yake yote na mshahara wake
unajulikana, anamiliki hekalu kama lile na tena
kukodishwa na serikali ya kigeni? unasemaje
kuhusu hili?
5. Pia unamiliki ranchi kubwa sana kule mzeri
handeni, ranchi hiyo ilikuwa ranchi ya taifa,
lakini ukajimegea na ukamega maeneo mengi
zaidi.
Ranchi iyo uliipata ukiwa bado kiongozi wa
Umma, Je, mtu aliyewahi kuwa waziri wa
mifugo na waziri mkuu, kujiuzia ranchi
iliyokuwa ya serikali, inaendana na dhana ya
uongozi uliotukuka??? Tukikupa madaraka
makubwa zaidi, hautajiuzia kila kitu? Vilevile,
katika nchi ambayo wananchi wengi hawamiliki
ardhi, Je, kiongozi kuhodhi eneo kubwa la
ardhi, inatupa picha gani wananchi?
6. Kwenye sakata la richmond, ujasiri nikusema
ukweli au kubwaga manyanga? Kama ungesema
ukweli na usingejiuzulu kwenye richmond,
chama kingeathirika vipi wakati unasema
hakuna kosa lililoanyika?
7. Kwanini kwenye kila tukio la kitaifa,
ukisimama tu karibu na kikwete, unahangaika
kutuma picha kwenye magazeti na mitandao
yote?
8. Katika miaka yako 40 ya utumishi wa
Umma,una lipi jipya ambalo umelisahau, na
sasa utalifanya katika huu urais wako
unaougharamia kwa pesa nyingi?
9. Umekuwa waziri wa ardhi, mbona matatizo
bado tele nchini? Umekuwa waziri wa maji,
mbona matatizo bado tele nchini?
Umekuwa waziri wa mazingira, mbona kuna
matatizo ya uharibifu na uchafuzi wa
mazingira? Umekuwa waziri wa mifugo, mbona
wafugaji bado masikini, na wanahangaika???
Huo urais unautaka wa nini kama uwaziri
umekushinda?
10. Umetoa mchango gani kwenye bunge
maalum la katiba katika kuyatetea maoni ya
wananchi, hali ulikuwa ukishuhudia
yakipotoshwa na chama chako

Japo namchukia Lowassa lakini nikiri kuwa umempa maswali marahisi mno.

1. Hakuna makosa kwa ndugu wa Rais kuwa na nyumba nje ya nchi

2. Sio kweli, ni uongo mtupu

3.Hakuna kosa baada ya Azimio la Zanzibar kwa kiongozi kuwa na nyumba ya kukodisha.Kama ni yake basi taarifa zake zipo Baraza la Maadili, kama hazipo leta vithibitisho kuonyesha kuwa ni nyumba yake

4. Utajiri ni uchu wa mtu, kuwa na cheo kikubwa sio kigezo cha kuwa tajiri.Utajiri ni uwezo wa kuzalisha pesa, uliyonayo iongezeke na sio kiwango cha mshahara.Hivyo inawezekana kabisa Mkuu wa Mkoa kuwa tajiri kuliko Rais, utajiri sio cheo cha mtu na akili ya mtu kutafuta utajiri, ata kwa njia halali.Sio kila utajiri ni njia haramu.

5.Sio kosa kumiliki ardhi, ata sasa juhudi kubwa ziongezwe kwa wanamchi kurasilimisha ardhi zao kuelekea mapinduzi ya kilimo

6.Kama alivyosema sababu ilikuwa Uwaziri Mkuu, kuna jopo kubwa la viongozi lilikuwa linahofu na utendaji wake, akaona kama visa vyote hivi ni sababu ya uwaziri mkuu na kwa kuwa yeye sio mroho wa madaraka, akaamua kujiuzulu.

7. Tatizo kubwa ni nyota, siwezi kuzuia mafuliko, waandishi kila wakiona Lowassa alipo wanamkimbilia

8. ELIMU Elimu Elimu na AJIRA KWA VIJANA AJIRA KWA VIJANA

9. Record ya utendaji kazi haina shaka, kama unakumbuka tulizuia Pepari mmoja kuchukua eneo la wazi mwaka 1995 na kwenye maji nadhani kila Mtanzania anajua juu ya maji ya ziwa victoria

10. Katiba ni maridhiano, kuna record isiyo na shaka kuwa ni rafiki wa vyama vyote, iwe CCM iwe Chadema; na makundi mbalimbali kwenye jamii.Kwa uzoefu huo palipo na kasoro tutarekebisha kwa pamoja.Kwa sasa kuna vitu kwa kuwa sio muamuzi wa mwisho hawezi kufanya.

Haya maswali yake naamini angeyajibu huku anacheka, nimejaribu kubashiri baadhi ya majibu rahisi ya maswali hayo.
 
Aliwazalo mjinga ndilo litakalomtokea!

Mzee Slaa ameanza kuogopa kivuli chake!
 
Naunga mkono hoja though najua kuna serikali ya umoja wa kitaifa.
 
Aliwazalo mjinga ndilo litakalomtokea!

Mzee Slaa ameanza kuogopa kivuli chake!

Lowassa ajui siasa wewe amezoea siasa zakimila zakuchinja siasa ya kushindana awezi ndio maana Arumeru kwa nassri tulimpiga zote yeye na Mkwe wake sasa ameshidwa kajimbo ni urais hongea kwa hoja usilete za mafisi hapa
 
Last edited by a moderator:
Mtu anatishwa na kagenzi tu ije kuwa ccm asitanie kakonda kama stiki anajihami tu.

Ccm maji kbs na wanamuogopa kwl, post ya kijinga huyo kagenz alitumwa na ccm na ndo maana tukamnyaka na mawasiliano na ccm
 
Utaratibu wa seminary za kikristo sodhani kama zinamuandaa mtu kuwa na elimu ya dini tu.
 
Dr Slaa kama Strategist hakuwa na haja ya kuonyesha mapungufu ya Lowassa kwa sasa! Tayari Pinda, Pengo, Masaburi, Membe Wanampiga Vita Lowassa... Isije ikasomeka kuwa ni mtanange wa Roman Catholic Vs KKKT ...
 
Back
Top Bottom