Maswali ya msingi kwa Mh.Lowasa -
1. Gazeti la raia mwema la novemba 2010
liliripoti na kuonesha picha ya nyumba ambayo
familia yako inamiliki uingereza. Ukasema ni ya
mwanao, je kwa nchi masikini kama ya kwetu,
ni sahihi kwa kiongozi wa UMMA kumiliki
nyumba kubwa ya kifahari nje ya nchi?
2. Mkapa alipounda baraza jipya la mawaziri
mwaka 1995 alikuacha, wengi wanasema kuwa
Nyerere alimuambia asikupe hata uwaziri, Je
kwanini mwalimu alikukataa???
3. Tangu mwaka 1994, zaidi ya miaka ishirini
sasa (20 years), Afrika kusini imekuwa
ikikodisha nyumba yako masaki kama ubalozi
wake, kuna tetesi kwamba huko nyuma
walitaka kuhama lakini wakaogopa kuihama
nyumba inayomilikiwa na kiongozi mkuu, na
kulikuwa na tetesi kwamba wanataka kuhama
lakini wanatishiwa.
Ni kiasi gani cha fedha umepata kwa zaidi ya
miaka 20 ya kukodisha nyumba hiyo???Je kiasi
hicho kimeripotiwa kwenye fomu ya maadili????
4. Kuna maelezo kwamba nyumba hiyo ya
,masaki ambayo mzee mandela alikuja mwaka
1994 kuufungua ubalozi mpya wa afrika kusini
ndicho chanzo kikuu cha mwalimu kusema
inakuwaje kijana wa miaka 41, akiwa mtumishi
wa umma maisha yake yote na mshahara wake
unajulikana, anamiliki hekalu kama lile na tena
kukodishwa na serikali ya kigeni? unasemaje
kuhusu hili?
5. Pia unamiliki ranchi kubwa sana kule mzeri
handeni, ranchi hiyo ilikuwa ranchi ya taifa,
lakini ukajimegea na ukamega maeneo mengi
zaidi.
Ranchi iyo uliipata ukiwa bado kiongozi wa
Umma, Je, mtu aliyewahi kuwa waziri wa
mifugo na waziri mkuu, kujiuzia ranchi
iliyokuwa ya serikali, inaendana na dhana ya
uongozi uliotukuka??? Tukikupa madaraka
makubwa zaidi, hautajiuzia kila kitu? Vilevile,
katika nchi ambayo wananchi wengi hawamiliki
ardhi, Je, kiongozi kuhodhi eneo kubwa la
ardhi, inatupa picha gani wananchi?
6. Kwenye sakata la richmond, ujasiri nikusema
ukweli au kubwaga manyanga? Kama ungesema
ukweli na usingejiuzulu kwenye richmond,
chama kingeathirika vipi wakati unasema
hakuna kosa lililoanyika?
7. Kwanini kwenye kila tukio la kitaifa,
ukisimama tu karibu na kikwete, unahangaika
kutuma picha kwenye magazeti na mitandao
yote?
8. Katika miaka yako 40 ya utumishi wa
Umma,una lipi jipya ambalo umelisahau, na
sasa utalifanya katika huu urais wako
unaougharamia kwa pesa nyingi?
9. Umekuwa waziri wa ardhi, mbona matatizo
bado tele nchini? Umekuwa waziri wa maji,
mbona matatizo bado tele nchini?
Umekuwa waziri wa mazingira, mbona kuna
matatizo ya uharibifu na uchafuzi wa
mazingira? Umekuwa waziri wa mifugo, mbona
wafugaji bado masikini, na wanahangaika???
Huo urais unautaka wa nini kama uwaziri
umekushinda?
10. Umetoa mchango gani kwenye bunge
maalum la katiba katika kuyatetea maoni ya
wananchi, hali ulikuwa ukishuhudia
yakipotoshwa na chama chako