Dr. Slaa bado anayo kadi ya CCM?

kama aliilipia mara kadhaa anayo haki ya kuiweka kama souvenir.pengine kesho vichaa fulani kam hawa walioanzisha thread watataka aje thibisha kuwa aliwahi kuwa mwanachama na card yake aonyeshe.
 
kweli shule na vyuo vyetu vina kazi sana kama ndio watu wanafikiri hivi. Kama hajarudisha manake kuwa anayo? Yaani hakuna uwezekano mwingine wowote ule? Mimi pia niliwahi kuwa na kadi ya CCM na hadi leo sijairudisha na sina mpango wa kuirudisha....

CLUE: Uanachama wa CCM unakomaje?
 
Kwani ni jinai kuwa na kadi ya CCM!!? Anasubiri Mh. Kikwete akirudisha ya CDM naye arudishe ya ccm!! Sijui kama unalijua hili!!
 
kadi si lazima urudishe kuthibitisha kuwa si mwanachama,, KUTOILIPIA ada tu kwa muda uliowekwa inakuwa umejitoa uanachama. kama hailipii ada wewe unawashwa nini?
 
Sio Dr tu hata baadhi ya wabunge wa cdm bado wanazo kadi za chama chetu mfano,Selasini,na Mheshimiwa Zitto
 
Duh yaani CDM kiboko wameanza kumchafua Dr. Slaa!

Jana nilikuwa kijiweni na vijana tunakunywa kahawa nikasikia wanasema Dr. Slaa alitumwa na Nyerere kuingia upadri ili ajue huko mapadri wanafanya nini na hakuwa na utashi wa kweli.

Kwa kifupi wanasema alitumwa na serikali na ni mtu wao hadi leo. Vijana wakawa wanaonyesha wasiwasi juu ya Dr. Slaa na wakasema afadhali Mbowe. Leo naona hii post nimeshangaa. Naona mitandao ya Urais ndani ya CDM inafanya kazi kwa umakini mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…