DR.SLAA awe na SUBIRA! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DR.SLAA awe na SUBIRA!

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by VUTA-NKUVUTE, Oct 20, 2012.

 1. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,872
  Likes Received: 6,623
  Trophy Points: 280
  Hakuna Mahakama hata moja nchini Tanzania itakayotamka kuwa kifungu cha 160 cha Sheria ya Ndoa,1971 kinaonesha uwepo wa ndoa badala ya Dhanio la Ndoa. Hata Jaji Laurence Kaduri anajua vyema. Ni jana tu Jaji Laurence Kaduri wa Mhakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam alitupilia mbali Pingamizi la Awali la Dr.Wilbrod Peter Slaa dhidi ya Shauri lililofunguliwa na Rose Kamili(MB) dhidi ya Dr.Slaa na Mchumba wake Josephine Mushumbusi.

  Katika shauri la Rose Kamili,msingi mkubwa wa shauri lake ni uwepo wa ndoa kati ya Dr. Slaa na Rose Kamili. Sheria ya Ndoa niliyoitaja hapo juu inabainisha wazi kuwa kuna aina mbalimbali za ndoa zikiwemo za kidini na za kimila. Nina uhakika,Mheshimiwa Rose Kamili hakuwahi kufunga ndoa na Dr.Slaa. Yeye ataegemea tu Dhanio la Ndoa chini ya kifungu cha 160 cha sheria ya Ndoa. Hiki hutumika tu pale panapotokea sintofahamu kwa watu wanaodhaniwa kuwa wameoana lakini kisheria sivyo.

  Kimsingi,Rose Kamili anaweza kupata matunzo ya watoto lakini si kukataza ndoa ya Dr.Slaa. Kuzuia ndoa si jambo la mchezo.Ni hadi athibitishe kuwa aliolewa na Dr.Slaa tena kwa ndoa ya mke mmoja ima ya kidini,kimila au bomani. Hapo patamshinda Rose. Lakini,Rose aweza kulalia muda hadi kesi ya msingi kuisha.Wakili Msomi wa Dr.Slaa,Mutakyamirwa,awe makini.

  Nimuombe Dr.Slaa kuvumilia kwa muda wa shauri hili ili aweze kuendelea na ndoa yake na Josephine. Hakuna haja ya kushtushwa na kutupwa kwa Pingamizi la Awali.Ni mambo ya kawaida Mahakamani. Ingawa ndoa iliyopangwa kufungwa tarehe 21/7/2012 imeshacheleweshwa vya kutosha,kama ipo ipo tu.Kama Dr. Slaa ameweza kuvumilia kwa muda wote uliopita,atashindwaje kuvumilia kipindi hiki cha kesi tu? Naamini hashindwi. Kila la kheri Dr.Slaa! Nakuaamini sana.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mods - peleka hii kwenye jukwaa la ndoa na mapenzi.
   
 3. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,872
  Likes Received: 6,623
  Trophy Points: 280
  Hii imekaa kisheria zaidi Mkuu
   
 4. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  kwani, what is the problem hapa? kuna tatizo gani mleta mada sema tukusaidie....dhana ya ndoa kifungu cha 160 inaingiaje hapa? unajua presumption of marriage huwa inaingia wakati gani? je? dr. slaa na mkewe wa zamani (ukiondoa huyu ambaye wamefunga naye ndoa hivi karibuni) si walipeana talaka? sasa dhana itatoka wapi hapa?

  kwa kifupi ni kwamba, hakuna ndoa kisheria ambayo inatambulika kama haijaandikishwa kwa msajili kule RITA. wakuu wa wilaya na viongozi wa dini ambao wamepewa delegated power kama wawakilishi wa msajili mkuu kila wakifungisha ndoa wanatakiwa kisheria kupeleka ndoa zote kwa msajili kila mwisho wa mwezi ili zikaandikishwe kweney register ya msajili mkuu kule rita dsm. ndoa yeyote ambayo imvunjwa huwa inaondolewa kwenye register kule kwa msajil mkuu. kama kuna ndoa inayoendelea, mtu hata akifunga ndoa nyingine ndoa iyo huwa ni batili tangu mwanzoni, haitatambulika kisheria kama mtu huyo alikuwa amefunga ndoa isiyo ya mitara (waislam na wapagani wanaruhusiwa ndoa za mitara, wakristo marufuku). na, suala la dhana ya ndoa kisheria halipo, isipokuwa, kukitokea matatizo hasahasa ya kimaslahi zaidi mfano pale mtu mmoja anaponyimwa haki yake, ndipo upande ule unaodhulumiwa huwa unaruhusiwa kutumia dhana hii, ni dhana tu si halisia, kwamba kama waliishi miaka miwili au zaidi, hakukuwa na ndoa iliyokuwa inaendelea, watu waliowazunguka wanajua kuwa wanaishi kama mke na mume, basi watadhaniwa kuwa walikuwa kwenye ndoa only for the purpose of kumpatia yule aliye upande wa kudhulumiwa haki yake, haki hiyo ikipatikana tu, suala linakuja palepale kuwa hapo hamna ndoa, muungano waliokuwa wanaishi ni batili kisheria.

  hivyo dhana ipo kama rungu la kupata haki kwa yule anayedhulumiwa tu, kama hakuna mazingira ya kudhulumiana au mmoja kupoteza haki fulani, basi sheria haitambui concubine hiyo kama ni ndoa. sasa kwa dr. slaa kama ndoa yake ya zamani ilikuwa haijavunjika, hata akikaa na hawara mpya kwa miaka hata kumi dhana hii haifanyi kazi kwasababu kulikuwa na ndoa inayoendelea. well, inasemekana walikuwa wamepeana talaka yeye na mkewe, na pia mchumbake inasemekana alipeana talaka na mmewe...kama hayo si ya kweli, muunganiko huo si halali na dhana haiwezi kufanya kazi. kama kweli pande zote mbili walikuwa wameachana na wapenzi wao wa zamani, basi dhana hii inaweza kufanya kazi. kama una swali lingine uliza.

  therefore, kama dr. slaa na mkewe wa kwanza walikuwa wamepeana talaka kabla, na mchumbake naye alikuwa ampeana talaka na mmewe kabla , basi dhana hii ingeweza kutokea tu pale dr.slaa au mchumbake mmojawapo kati yao angekuwa yupo upande wa kudhulumiwa. mf. wamechuma mali pamoja na mmoja anataka kumfukuza mwingine amiliki peke yake, dhana hi inaweza tumika kwa yuel mwengine kupata haki yake, na akishapata haki tu kwisha habari yake, sheria haitambui kama kuna ndoa hapa.

  pia, kama hawakuwa wamepeana talaka pande zote mbili, basi, hapo hakuna dhana, kwasababu vigezo vya dhana ni kwamba, kunatakiwa kusiwepo ndoa inayoendelea (ndoa huwa inaendelea hadi talaka itolewe na mahakama au mmoja afe, hata kama wametengana kwa miaka mingi kama talaka haijatolewa ndoa bado ipo na kule kwa msajili majina ya ndoa yao bado yapo, talaka ikitoka tu ndoa yao inakatwa toka kwenye register), pia asiwe kwenye umri usioruhusiwa, majirani wawe wanawatambua kama mme na mke, na vigezo vyote vinavyoifanya ndoa kutokuwa batili viwepo.....la sivyo, kama hakuna tatizo, sheria haitambui ndoa ambayo haijasajiliwa. hivyo basi hata zile ndoa za kimila ambazo mtu anatoa mahari tu halafu anaruhusiwa kuishi na mke, si ndoa kisheria na hazitambuliki, labda likitokea tatizo ndo upande unaodhulumiwa unaweza kutumia kama dhana ili kuokoa maslahi tu na si zaidi ya hapo.
   
 5. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #5
  Oct 20, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  zaidi ya yote dr. slaa ameshafunga ndoa na mkewe mpya, hivyo topic hii haina maana sana, labda kwaajili ya kuellimishana tu ili watu wajue sheria ya ndoa.
   
 6. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,748
  Likes Received: 12,842
  Trophy Points: 280
  Unajua unacho kinena?

   
 7. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,748
  Likes Received: 12,842
  Trophy Points: 280
  Ni kweli ana chotegemea rose ni pre-assumption of marriage hakuna lingine na ana jua fika watoto wanapata matunzo kwa hiyo sidhani kama ana dai haki za watoto!

  Na kutupwa kwa pingamizi sio ushindi kwa Rose bali ni kupisha tu case hianzwe kusikilizwa!
   
 8. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,872
  Likes Received: 6,623
  Trophy Points: 280
  Ndoa bado Mkuu.Ilisimamishwa kupisha kuisha kwa shauri hili
   
 9. h

  hacena JF-Expert Member

  #9
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 619
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  kwa wale waliopata bahati ya kusoma Law of Marriage nadhani watakuwa walipata bahati ya kusoma maamuzi mbalimbali yaliyotolewa na Mh. Jaji James Ladislaus Mwalusanya (marehemu sasa) akitafsri kifungu cha 160 cha Sheria ya Ndoa,kuwa hakileti njia mbadala ya kufunga ndoa bali ni dhanisho la ndoa pale wanandoa wanapokuwa wameishi kwa zaidi ya miaka 2, pamoja jamii inayowazunguka ikawachukulia kuwa ni mume na mke, na dhanisho litawekwe pale kutakapokuwa na shauri mahakamani la kutaka kuwaachanisha wanandoa hao na kugawa mali na matunzo ya watoto.

  hapo utaona aina majaji tulionao ni nourma
   
Loading...