Dr Slaa awakabidhi Kadi Makamanda Ester Wassira na Lilian Wassira

Baba yao je hakuwahi kuhama kama nakumbuka vizuri?aligombea hata ubunge.mtoto wa nyoka hatabadilika kuwa wa mnyoo ataendelea kuwa na sumu ya njoka
 

Hii siyo issue kabisa. Usijekuta wanaingiza mamluki
 

Hata mm mkuu, nina hamu sana ya kusikia kauli ya Wasira kwani alitamka haya maneno makali kwa urahisi sana, haya ndo mambo ya kuongea kwa kukurupuka
 
Karibuni sana makamanda tujenge nchi yenye kuzingatia haki na utu wa mwanadamu. Mungu awape maisha marefu.
 
Kweli nimeamini Wasira ni kichwa ameangalia upepo wa ccm ameona lazima 2015 cdm ichukue nchi hivyo amewashauri wanae wajiunge cdm ili 2015 waweze kuingia kwenye system. Nadhani hta baba riz1 karibu atawashawishi watoto wake wawahi nafasi cdm
 
Kama siyo tamaa ya madaraka MH. Steven Wassira angekuwa upinzani mpaka sasa. Kwa wale wasiojua, Wassira ambaye ni mbunge na waziri kupitia CCM alishawahi kuhamia NCCR MAGEUZI na akagombea ubunge kwa kupitia NCCR na akashinda then kwa tamaa akarud CCM
 
Habari njema sana . Ndio ccmweli wajue sasa nguvu ya cdm!
*******************
Cdm haitafikisha mwaka-wassira

Inaonekana wewe hufanyi kabisa research wewe, watoto wengi tu wa wakubwa, wengine wakubwa wa usalama wa taifa, wazazi wao wanawakati mgumu sana majumbani mwao, watu hawataki kuwa wanafiki kabisa, wanaona wafanye/waseme kile kinachowasukuma toka ndani ya mioyo yao, binafsi nimefanya kautafiti kadogo tu na nimegundua hilo, nilikuwa nasoma mara nyingi gazeti la Raiamwema ile makala ya Hidaya na mpenziye Frank, mara nyingi nilikua simwamini mwandishi kuhusu maisha ya waziri yule wa serikali ya mikiki, tena inaelekea wakati fulani mwandishi ni kama alikua anamsema Wasira huyu huyu, binti siku moja akabandika picha ya babaye akiwa anauchapa usingizi kikaoni kwenye wall ya face book, waziri aliye recordiwa akifanya hayo alikua huyu huyu Tyson, nilipo sikia suala la yule mwanae aliopo US nikajua kumekucha, so mkuu, usijidanganye ka eti ni ma spy, hii ndio hali halisi ya Tanzania kwasasa, nimalizie kwakusema hivi; Ukiona mtu anaipenda ccm ujue aidha ni mjinga, haelewi uhusiano wa maisha ya kila siku na siasa au mtu huyo ni fisadi/anafaidika na mfumo wa kifisadi nje ya hapo, huwezi kuipenda ccm hata kidogo, hata hao wanaipenda ccm kwasababu viongozi wengi ni wa dini yao, ni ujinga tu ndio unaowasumbua, sio kitu kingine!
 
Hawa mabinti ni watoto wa KAKA YAKE Steven Wassira (Mzee wa Gombe), Baba yao anaitwa George Wassira, kwa hiyo ni familia ya Wassira na kusema 'Watoto wa Wassira" ni sahihi na wala sio upotoshaji kama magamba wanavyojaribu kupotosha. Nakumbuka wakati wa uchaguzi mdogo wa Arumeru suala la Vicent Nyerere lilivyowatoa jasho magamba lakini bado wakaangukia pua
 
Sio watoto hasa wa tyson,kama sikosei wanamwita tyson baba mkubwa or something.
Ni kweli Bushloiyaiz. Si watoto wa Steven Wassira. Hebu na wataje majina matatu. Inaonekana ( it appears) ni watoto wa ndugu yake tyson na inaonekana ( it seems) familia hizo mbili hawaelewani
 
Ni kweli Bushloiyaiz. Si watoto wa Steven Wassira. Hebu na wataje majina matatu. Inaonekana ( it appears) ni watoto wa ndugu yake tyson na inaonekana ( it seems) familia hizo mbili hawaelewani
Nani amekuambia familia hazielewani? Labda kama hawaelewani kwa kutofautiana kimtazamo kuhusu ni chama kipi chaweza kujengaTanzania tunayoitaka. Usibuni tu mambo kwa kusema vitu ambavyo havipo
 
Hili linatoa changamoto kwa watoto wa waakubwa kuwa fikiria kwa kichwa chako unga mkono ukombozi badala ya kufuata mkumbo wa wazazi wako
 
Ni watoto wa wassira mwingine and not steven,baba yao ni wakili,george wassira,
 
Ni kweli Bushloiyaiz. Si watoto wa Steven Wassira. Hebu na wataje majina matatu. Inaonekana ( it appears) ni watoto wa ndugu yake tyson na inaonekana ( it seems) familia hizo mbili hawaelewani

ni wa George Wasira! Baba yao anaishi kibaha,na aliwatelekeza toka wakiwa wadogo akaoa mke mwngne! So wao hawaelewan na ding yao! Wanaishi ukonga.
 
ni wa George Wasira! Baba yao anaishi kibaha,na aliwatelekeza toka wakiwa wadogo akaoa mke mwngne! So wao hawaelewan na ding yao! Wanaishi ukonga.

We are missing a point. Tujadili sababu wanazosema zimewapeleka kwenye chama cha ukombozi badala ya hizi hadithi ambazo mbali na kwamba hazina ushahidi hazitusaidii katika hoja iliyopo mbele yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…