Dr Slaa atoa Onyo kali kwa wabunge wa CCM

Dr Slaa atoa Onyo kali kwa wabunge wa CCM

slaa nae kichwa chake kama katuni . Eti wabunge wasiozidi mia tatu watakuwa wamekataa maoni ya watanzania milion arobain, hivi hao watanzania wako mfukon mwake,au mdomoni mwake yeye ameonana lini na watanzania wengi kuliko walionana na wawakilishi milion arobain. Wabunge ni wawakilishi wa kikatiba wa wananchi je slaa anqmwakilisha nani. Masaburi makubwa kichwani

Naona leo hata meza ya Boss hukusafisha kisa kuchezea PC yake ili upost utumbo wako. Hata sisi kuna mesenja wetu hivyohivyo tangu kajua net.....!!!!!
 
Bila Posho hakuna kitakachoeleweka. Posho kwanza! Lakini hiki kitisho cha kuvunja Bunge tena! Hapo lazima Mibunge ya CCM inywee maana inajua kabisa uwezekano wa kurudi tena uchaguzi ukiitishwa leo hakuna, hela walizokopa lazima ziwatokee puani.
 
sasa naanza kupata picha. Wanachokataa ni kupelekeshwa au ni mabadiliko?
 
Sio wa CCM tu kwa taarifa yako hata CDM wabunge wao wako hoi , wamekopa kwenye mabenki. Mfano, Mnyika Tshs 200m (CRDB), Selasini Tshs 210m (CRDB)


Kama projections za mapato yao zilielekezwa kwenye posho na mishahara basi atakayelipa deni ni bunge la Tanzania kwani ofisi ya bunge ndiyo ilimdhamini mkopaji.Na kuvunjwa kwa bunge itakuwa maamuzi ya rais kwa hiyo mbunge hana kosa.Lazima ofisi nya bunge itajitokeza kama mdhamini mkuu na ndiye atabeba msalaba na si Mnyika wala selasini.
 
anatoa onyo kali kwa wabunge wa ccm yeye kama nani?acheni siasa za maji taka.
 
Hivi wabunge wa chadema waliposusia bunge walikosa uzalendo? Na kama ndivyo dr Slaa alichukua hatua gani?

walipoamua Kutoka nje kwa sababu ya kutokubaliana na mabadiliko ya sheria ya muswada wa katiba ilikuwa ni kwa manufaa ya chadema au ya wananchi..? Ulitaka Dr Slaa achukue hatua gani km wabunge wamefanya kazi yao ya kupingana muswada wa sheria unaotaka kupitishwa kuwa sheria ambao haujali masilai ya wananchi.. Au unafikiri kazi ya wabunge pale ni nini kusema Ndiooooooooo tu,halafu posho mfukoni..? Kwa sasa lazima tuwashangae wabunge kupitia ccm ambao wao wameweka maslai ya posho na ushabiki wa ki chama mbele kuliko sisi wananchi..think before Act.. Penye ukweli lazima tuusimamie woote,achana na longolongo za siasa za mtaani.. Kama wewe ni Zumbukuku uliza ulimwengu ulipo upelekwe.... Acha kuwa mweupee
 
Kama projections za mapato yao zilielekezwa kwenye posho na mishahara basi atakayelipa deni ni bunge la Tanzania kwani ofisi ya bunge ndiyo ilimdhamini mkopaji.Na kuvunjwa kwa bunge itakuwa maamuzi ya rais kwa hiyo mbunge hana kosa.Lazima ofisi nya bunge itajitokeza kama mdhamini mkuu na ndiye atabeba msalaba na si Mnyika wala selasini.

Nilitegemea uende na fikra za mbele ww unarudi nyuma. Pesa ya bunge ni ya nani ? ukiisha jua jibu la hili swali hapo utajua msalaba uko kwa nani

 
posho ziongezwe zifikie laki tano na kuanzia sasa ziitwe UJIRA WA MWIA - Shibuda.
 
Nimemshangaa sana sana Slaa, nimeamini KWELI SLAA ANA AKILI ZA EMBE DODO


Wewe ni mtu wa kuhurumiwa kwa sababu unachojua ni matusi.Huna hoja yoyote unachojua ni kutukana tu
 
Ningefurahi kama JF tungepata copy ya mswaada huo in Swahili.
Nina uhakika hakuna mabadiliko ya maana yaliyofanywa... but I stand to be corrected.

Niliiona jana humi jamvini itafute tuu mkuu!!
 
Kikwete Simamia msimamo wako. Wewe unaondoka, na usitake uondoke kwa kukosa Heshima ya kuto kumbukwa. Tafadhali Fanya Katiba iwe utambulisho wa ulicho kifanya katika Uongoziwako. ukifanya Katiba nzuri Watanzania watakupa Heshima yako, ila ukiwasikiliza hao walipa MKadeni utajiangusha wewe na utapotea katika Historia

Fanya maamuzi na Wakileta Kokoro Vunja bunge ili tuone Mbichi na mbivu
 
Nimemshangaa sana sana Slaa, nimeamini KWELI SLAA ANA AKILI ZA EMBE DODO

Bado wapo wengi kama wewe wanahitaji kuelimishwa...kama watu wote wangewaza na kutoa maoni kama yako hatutafika...toa maoni kama mwananchi mzalendo kwa nchi yake na sio kifisadi kidogo kinachojifunza siasa...
 
slaa nae kichwa chake kama katuni . Eti wabunge wasiozidi mia tatu watakuwa wamekataa maoni ya watanzania milion arobain, hivi hao watanzania wako mfukon mwake,au mdomoni mwake yeye ameonana lini na watanzania wengi kuliko walionana na wawakilishi milion arobain. Wabunge ni wawakilishi wa kikatiba wa wananchi je slaa anqmwakilisha nani. Masaburi makubwa kichwani
we jamaa ni kilaza kweli....tumia maneno ya busara
 
MAREKEBISHO

Serikali imekubalikufanya mabadiliko katika kifungu cha 6 (1) cha sheria hiyo kwa kuondoa mamlakaya uteuzi moja kwa moja kwa rais.
Kifungu cha 6 (1) chasheria, sasa kinasema rais atateua wajumbe kutoka miongoni mwa majinaatakayopelekewa na vyama vya siasa, asasi za kiraia, taasisi za kidini na vyamavya kitaaluma kuwa wajumbe wa Tume ya Katiba.


Aidha, serikaliimeridhia matakwa ya CHADEMA ya kuongeza kifungu cha 17 (10), kinachoruhusuwatu binafsi, taasisi za kidini na vyama vya hiari kutoa elimu ya uraia. Asasihizo sasa zitakuwa zinaripoti kwa mkurugenzi wa halmashauri badala ya mkuu wawilaya.

Vile vile serikaliimeridhia kufutwa kwa kifungu ch 6 (5) (c) kilichokuwa kina waondolea sifawajumbe wa tume, watu waliowahi kuhukumiwa kwa kutenda kosa au mtuhumiwa katikashauri lililoko mahakamani linalohusu shitaka la kukosa uaminifu au maadili.


Ibara nyingine ambayoimefanyiwa marekebisho kwa mujibu wa makubaliano kati ya Rais Kikwete naCHADEMA ni 6 (5) (a) ambako madiwani au viongozi wa vyama vya siasa wa ngazizote waliokuwa wamezuiliwa kuwa wajumbe wa tume, sasa wameruhusiwa.

Jingine ambalo CHADEMAwalipendekeza na serikali kuridhia ni kuhusu kamati ya nidhamu ya Tume yaKatiba.

Awali sheria hiyoilikuwa kimya kuhusu kamati ya nidhamu, lakini sasa kimeongezwa na kitakuwakinaongozwa na mtu mwenye hadhi ya ujaji wa Mahakama ya Rufaa, akishirikiana nawajumbe wa nne kutoka Tume ya Haki za Binadamu, Utawala Bora, Tume ya Maadiliya Umma, Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Chama cha Wanasheria Zanzibar(ZLS).


tanzaniadaima=source

 
Hii inathibitisha kuwa Bunge letu ni genge la wahuni wasiona uchungu na nchi bali matumbo yao.

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema ameshangazwa na taarifa za tishio la wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) za kutaka kugomea kujadili muswada huo.
Amesema endapo watayagomea marekebisho hayo na kuyarudisha kwa Rais Kikwete anaweza kuamua kuvunja Bunge kwa mujibu wa Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Dk. Slaa alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, juu ya taarifa za wabunge wa CCM kutishia kugomea mjadala wa marekebisho hayo.
Alisema wabunge wa CCM wanapaswa kuzingatia utaratibu uliotumika kupata maoni mbalimbali yakiwamo ya vyama vya upinzani, taasisi zisizo za kiserikali ambazo zilitoa maoni yake.
Alibainisha kuwa wabunge wa CCM wasiozidi 300 hawawezi kuzuia maoni ya Watanzania wasiopungua milioni 40 na endapo watafanya hivyo watakuwa wanamwelekeza rais kuvunja Bunge.
“Wabunge wa CCM wakumbuke kwamba serikali imepeleka muswada huo kwao si kwa sababu yametolewa mapendekezo na CHADEMA au chama cha siasa tu, umejadiliwa na Watanzania wengi.
“Kama kweli wataugomea na kuurudisha kwa rais tena, rais anaweza kuamua kuvunja Bunge kwa mujibu wa Katiba,” alisema.
Dk. Slaa alisema anashangazwa sana na wabunge wa CCM ambao wamekuwa wakijigamba kwamba serikali inayoongozwa na chama chao ni sikivu halafu hao hao tena washindwe kutekeleza yaliyofikiwa na serikali hiyo hiyo.
Alisema wabunge ni lazima waonyeshe uzalendo wao kwa Watanzania kwa kujadili muswada wa mabadiliko ya sheria badala ya kushindana na mamlaka ya rais

SOURCE:TANZANIA DAIMA
 
Back
Top Bottom