Dr. Slaa Atembelea Moja Ya Bandari Kubwa Marekani !

Dr. Slaa Atembelea Moja Ya Bandari Kubwa Marekani !

Rtackket

Member
Joined
Sep 24, 2013
Posts
74
Reaction score
373
Dr. Slaa anaendelea na safari yake ya kujifunza inayoitwa “Vision Tanzania” ambayo leo imemfikisha moja ya bandari kubwa nchini marekani. Bandari ya Mobile Alabama ambako alipokelewa na mkurugenzi wa Shirika la Alabama Ports Authority
Shirika la Alabama Ports Authority inapitisha makontena 100 kwa lisaa limoja na mizigo inayozidi tani million 30 kwa mwaka na kuipa shirika hilo linalojitegemea kiasi cha dola za kimarekani million 152 kwa mwaka ambazo ni faida. Shirika hilo lina wafanya kazi 600 tu, lakini imeweza kutoa ajira ambazo siyo za moja kwa moja 280,000.

Bandari ya Alabama inajitegemea kiuendeshaji; haliingiliwi na uongozi wa jimbo. Utekelezaji wa bandari hii ni wa kipekee kwa sababu mizigo uondoka bandarini punde tu zinapowasili au chini ya siku tatu. Alichojifunza Dr. Slaa katika ziara hii ni kwamba, mashirika ya umma yanaweza kufanya kazi kwa ufaninisi mkubwa pasipo uingiliaji wa kisiasa.

Dr. Slaa pia amejifunza kwamba, kama jimbo dogo kama Alabama inaweza kupitisha tani million 30 kwa mwaka, basi Tanzania inaweza kupitisha tani million 100 kwa mwaka kutokana na jiographia yake. Dr. Slaa anaamini kwamba Bandari ya Tanzania inaweza kuajiri vijana 350,000 chini ya utawala wa Chadema.

Dr. Slaa anaamini kwamba, mashirika ya umma kama bandari hayana ufanisi kwa sababu waendeshaji wake wanateuliwa kiurafiki na kindugu bila ya kuzingatia uwezo wa mtu. China ya utawala wa Chadema haya yote yatafikia kikomo kwa manufaa ya watanzania wanaoumia na umasikini


attachment.php

Dr. Slaa Akipokelewa na Mkurugenzi wa Mkuu wa Bandari ya Mobile Alabama
attachment.php

Mkuregenzi mkuu wa Bandari akitoa maelezeo kwa Dr. Slaa
attachment.php

mashine (crane) zinazotumika kunyanyua kontena
attachment.php

Sehemu maalum ya kushusha kontena
attachment.php

Mashine nzito bandarini ikishusha mizigo




Alabama Business Council.

Dr. Slaa amekutana na viongozi wa juu wawili wa “Alabama Business Council” Katika chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa ajili yake na taasisi hiyo. Mwenyekiti wa Alabama Business council ameahidi kuhamasisha makampuni makubwa kwenye jimbo la Alabama kumsaidia Dr. Slaa na Chadema kunyunyua uchumi wa Tanzania kwa kuwekeza kwenye sekta mbali mbali za uchumi wa Tanzania kama Kilimo, elimu, viwanda, miundombinu nishati nk.

attachment.php

Dr. Slaa akipokelewa na kiongozi wa Alabama Business Council ambaye pia alikuwa msaidizi wa Rais Bush Snr. kwenye maswala ya kiuchumi
attachment.php

Dr. Slaa na Msaidizi wa zamani wa Rais Bush wakiwa katika majadiliano
attachment.php

Chakula cha jioni iliyotayarishwa kwa ajili ya Dr. Slaa
attachment.php

Dr. Slaa akipokea zawadi ya kitabu kutoka kwa rafiki yake​
 

Attachments

  • Akipokelewa na Viongozi Wakuu wa Bandari.jpg
    Akipokelewa na Viongozi Wakuu wa Bandari.jpg
    2 MB · Views: 403
  • Dr. slaa akipokelewa.jpg
    Dr. slaa akipokelewa.jpg
    68.4 KB · Views: 3,283
  • Berth.jpg
    Berth.jpg
    50.1 KB · Views: 3,214
  • Cranes.jpg
    Cranes.jpg
    48.6 KB · Views: 3,187
  • Tanks.jpg
    Tanks.jpg
    23.8 KB · Views: 3,154
  • Heavy cranes.jpg
    Heavy cranes.jpg
    54.8 KB · Views: 3,101
  • Dr. Slaa received by Alabama Business Council.jpg
    Dr. Slaa received by Alabama Business Council.jpg
    49.4 KB · Views: 3,083
  • Dinner1.jpg
    Dinner1.jpg
    43.7 KB · Views: 3,061
  • The Dinner.jpg
    The Dinner.jpg
    55.6 KB · Views: 3,017
  • Book.jpg
    Book.jpg
    38.9 KB · Views: 2,970
Dr. Endelea na hiyo ziara ya kimafunzo. Tuliowahifanya field excursion tunajua umuhimu wake. Dr. Jifunze na tourism sector ambayo ni almas imelala na inakanyagwa na nguruwe. Mfano ubomoaji wa Dar historic center, EIA zinazofanywa kuwafurahisha wenye meno na utawala bora kwa mapana yake, japo wengi wamefundishwa na ngwiji Prof. Ngware hawakuilewa concept ya good governance.
 
CCM bado mnaweweseka!Mwigulu Rais mtarajiwa kupitia CCM amesharudi hivi?Nchi haishi vimbwanga...Eti Mwigulu anastahili kuwa Rais wa Tanzania kwa kuwa ameenda Marekani!Kweli?
 
S
Hata utalii nao mwafanya issue kubwaa. Kweli Chadema ni mkia wa mbuzi
Mmesahau jamaa mmoja alikwenda visiwa fulani akabembea akarudi. Nchi yake walipotaka kuweka Tao la Mashariki kama kivutio cha utalii kwa dunia akazuia. Naomba ujufunze tafsiri ya neno utalii otherwise unaandika kama mtu mwenye wivu ama aliyetamauka.
 
Yap! Dr slaa tafiti,chunguza,ili ufahamu wapi pa kuanzia good job
 
Hivi Dr.Slaa ameishawahi kutembelea bandari zetu, Dar es Salaam, Tanga, Mtwara, Mwanza, Kigoma, Bukoba, kufahamu zinaitaji nini.

Dr. Slaa bandari ya Alabama haiuwezi kukusaidia kitu labda kupiga picha kama ni muendelezo wa safari yako ya utalii hakuna tatizo.

Kama una uchungu na nchi yako anza kutembelea bandari za nchi yako hili hujue maitaji yao.
 
Wakuu wetu
1. Zitto Zuberi Kabwe
2. John J Mnyika
3. Tundu Lissu
4. Joshua Nassari
5. Kitila Mkumbo
6. Tumaini Makene

With all due respects hebu naombeni msaada wa kueleweshwa rationale na funding behind this study
tour

Nchi ya demokrasia na maendeleo,nguvu ya wananchi ni pamoja na kupata taarifa sahihi kwa wakati kutoka vyanzo sahihi na vinavyoaminika
 
Wakuu wetu
1. Zitto Zuberi Kabwe
2. John J Mnyika
3. Tundu Lissu
4. Joshua Nassari
5. Kitila Mkumbo
6. Tumaini Makene

With all due respects hebu naombeni msaada wa kueleweshwa rationale na funding behind this study
tour

Nchi ya demokrasia na maendeleo,nguvu ya wananchi ni pamoja na kupata taarifa sahihi kwa wakati kutoka vyanzo sahihi na vinavyoaminika

Ni haki yako kujua kama kweli nchi unayosema inaendeshwa kidemokrasia, lakini pia kama si wivu na hoja mbisho juu ya safari zenye muono wa mafanikio kwa watanzania.
 
Naona tamthilia ya Dr. Slaa inaendelea.

Episode I ilikuwa kutembelea wanajeshi wa Marekani.

Episode II ilikuwa State Reception Alabama,ingawa kulikuwa hakuna wageni waalikwa wengine.

Episode III vision Tanzania kuzunguka bandari ya Alabama

Tusubiri Episode IIII sijui itatoka lini.
 
Hivi Dr.Slaa ameishawahi kutembelea bandari zetu, Dar es Salaam, Tanga, Mtwara, Mwanza, Kigoma, Bukoba, kufahamu zinaitaji nini.

Dr. Slaa bandari ya Alabama hauwezi kukusaidia kitu labda kama ni muendelezo wa safari yako ya utalii.

Kama una uchungu na nchi yako anza kutembelea bandari za nchi yako hili hujue maitaji yao.

Hakuna cha kujifunza kwenye Bandari zetu..

Kuwa CDM ni uchungu tosha kwa Tz..

Mtalii anajulikana..Mkuu wetu..mbona hatujaona picha zake?
Si nae alikua USA for 11 days?...
 
Naona Dr. Slaa anazidi kutumbua ruzuku ya CHADEMA.

Wajinga ndiyo waliwao.
 
Ama kweli magamba sijui ni ujinga ama ni kitu gani?Juzi Mwigulu Nchemba alisema anakuja Marekani ili ajifunze "wenzetu walifanyaje wakafanikiwa",akaishia kwenye sherehe za pilao na sasa yuko London.Kama ukitembelea nchi za watu na ukawa mtu wa kujifunza,halafu upo ama unatajarajia kuwepo kwenye nafasi ya uongozi,basi lazima utaleta mabadiliko.Ni mfumo wa ukoo wa panya ndo umeharibu nchi,but we can if we get leaders with vision and plans to get us there.Siyo kama magamba cowards ambao ubinafsi umewapofusha.Piga kazi Slaa,acha waendelee kubwabwaja,cha muhimu ni trip yako ya vision Tanzania ituimike kujifunza na kulisaidia taifa tujikwamuwe kutoka kwenye umasiki na ujinga uliokithiri,na si kuzunguka kuuza nchi na kutembeza bakuli.Halafu mnaita hii utalii,subirini muwekewe mambo ya kubembea Jamaica.
 
Wakuu wetu
1. Zitto Zuberi Kabwe
2. John J Mnyika
3. Tundu Lissu
4. Joshua Nassari
5. Kitila Mkumbo
6. Tumaini Makene

With all due respects hebu naombeni msaada wa kueleweshwa rationale na funding behind this study
tour

Nchi ya demokrasia na maendeleo,nguvu ya wananchi ni pamoja na kupata taarifa sahihi kwa wakati kutoka vyanzo sahihi na vinavyoaminika

Mkuu mimi naona hii tua inafaida kubwa kwa CDM kuelekea 2015. Majama ya Lumumba yanafika kwenye uchaguzi hayana jipya kwasababu yanawatuma wakubwa zao kubembea ulaya na china badala ya kuingiza nondo kichwani.
 
Naona tamthilia ya Dr. Slaa inaendelea.

Episode I ilikuwa kutembelea wanajeshi wa Marekani.

Episode II ilikuwa State Reception Alabama,ingawa kulikuwa hakuna wageni waalikwa wengine.

Episode III vision Tanzania kuzunguka bandari ya Alabama

Tusubiri Episode IIII sijui itatoka lini.

Acha wivu wewe gamba!
Mbona rais wako anatumia muda mchache chini au hapa Tanzania lakini hujawai claim hata siku moja.
 
moto mdundo RAIS wa mioyo ya WATANZANIA,MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI CHADEMA MUNGU MBARIKI,MPONYE,MPE HEKIMA,MTIE NGUVU dr slaa.
 
Back
Top Bottom