Dr. Slaa atazishinda propaganda dhidi yake!

Dr. Slaa atazishinda propaganda dhidi yake!

mkuu hivi unajua maana ya uadilifu au unajisemea tu.

yani ur posts uwa znantia kinyaa, kwan wewe mda wako mwingi unautumia kuyatetea na kuyapamba mafisadi, lzm una laana wewe
 
.

Kwanza si vibaya kukumbushana maana ya uadilifu: Uadilifu ni:

a. Kukipa kila kitu haki yake inayostahiki.
b. Kuipa nafsi yako yale yaliyo ya haki tu.
c. Ni hali ya kuwa katikati baina ya kuchupa mipaka katika kufanya jambo au kujizuia kufanya jambo hilo bila ya kumdhulumu mwengine.

DR Slaa anakosa sifa za uadilifu kwa hivyo vigezo vitatu kwa kashfa ya kupora mke wa mtu na hasa kwa kuzingatia umri alionao.
Mengine itakuwa ni mahaba ya kipendacho moyo, Jicho huona kingeza!

naona wewe bado mtoto kwenye mambo ya ndoa....unadhani ndoa ni kuwa na cheti cha ndoa tu au?
 
naona wewe bado mtoto kwenye mambo ya ndoa....unadhani ndoa ni kuwa na cheti cha ndoa tu au?

Mzee DR Slaa alikosea tena kulingana na hadhi na umri alio nao ilikuwa bora baada ya kugundua (kama hakujua) angeacha akatafuta mchumba mwingine. Kupora mke wa mtu ni hatari sana hasa kwa mwana dini kama DR.
 
Mimi namwona Dr Slaa ni kiongozi mkweli sana. Kwani angekuwa mwongo kama magamba angekanusha tu kuwa hana kadi hiyo ya CCM. Si mtu mwenye tamaa ya mali, ni mkali sana kwa wazembe na wala rushwa na mtu ambaye yupo karibu na Dr atakuthibitishia hili. Nina imani 2015 nchi itapata Nyerere mpya. As a country under Dr Slaa we will rise again, we will lead again!
hapo umenena jembe achana na propoganda za wachumia tumbo
 
Mzee DR Slaa alikosea tena kulingana na hadhi na umri alio nao ilikuwa bora baada ya kugundua (kama hakujua) angeacha akatafuta mchumba mwingine. Kupora mke wa mtu ni hatari sana hasa kwa mwana dini kama DR.

narudia tena wewe bado mtoto mchanga kwenye mambo ya ndoa
 
narudia tena wewe bado mtoto mchanga kwenye mambo ya ndoa

Nakurudia tena wewe mtu mzima, hakuna justification yoyote na popote ambayo inaweza kuruhusu kupora mke wa mtu. Ni kigezo muhimu ktk kupima uadilifu wa mtu hasa mbaye ni Padri anajua elimu ya dini. Halafu katika dini ya kikristo inaruhusiwa kuacha na kuoa mke mwingine (isipokuwa kwa kifo na uhasherati)?
 
soma hapa hapa ukimaliza huandika tena hiki unachoandika hapa. hivi mpaka leo hii hujui kuwa josephine walishapeana talaka na mume wake wa kwanza? naona unachukulia ndoa kama tukio na siyo kama taasisi...

http://www.ruthinstitute.org/ITAF12/faculty/readings/marriageInstitution.pdf
 
Nilisema humu mapema kuwa CDM itakabiliwa na magumbu mengi na hii ni kwa sababu ina nguvu. Maana wasio tishio watasemwaje? unaona vyama vidogo vidogo nanI anavifuatafuata? Ikitokea bahati mbaya mtu timamu akaghafirika akavaa kandambili tofauti kila mtu atamcheka. kichaa hata atembee uchi... Dr Slaa usikate tamaa. NA MWINGINE MWENYE NIA NJEMA ASIKATE TAMAA
 
Acheni malumbano ya kitoto. Dk Slaa ni kiongozi imara kabisa wala hatishwi na propaganda za CCM. Chadema msikubali kuyumbishwa na mambo madogomadogo kama kadi. Most of wapinzani walikuwa makada wa ccm before. What's the problem?
 
Angekuwa sio mroho wa pesa na msaliti kwa Mungu kama unavyomtetea,nijibu swali moja tu,Kwanini aliiba michango ya pesa za ujio wa Papa Paul ndo maana akakimbia kanisani??

......Kwa namna anavyofanya kazi zake, tangu akiwa bungeni, namna alivyotaja “orodha ya mafisadi (list of shame) iliyohusisha viongozi wa Serikali na CCM, alivyoombwa kugombea urais na kuungwa mkono na watanzania, anavyosimamia utendaji wa CHADEMA na kuhakikisha chama chetu kinatekeleza wajibu wake katika kila jukwaa dhidi ya serikali ya CCM, ni kijana mpuuzi na msaliti anaweza kusimama kumnyooshea kidole kwa kutumia propaganda za CCM na vibwagizo vya Nape Nnauye na CCM.....

Hebu ona aibu! angalia wenzio wenye uwezo wa kufikiri wanavyoongea!
 
Mimi namwona Dr Slaa ni kiongozi mkweli sana. Kwani angekuwa mwongo kama magamba angekanusha tu kuwa hana kadi hiyo ya CCM. Si mtu mwenye tamaa ya mali, ni mkali sana kwa wazembe na wala rushwa na mtu ambaye yupo karibu na Dr atakuthibitishia hili. Nina imani 2015 nchi itapata Nyerere mpya. As a country under Dr Slaa we will rise again, we will lead again!
Bahati mbaya kabisa taifa letu limezoeshwa kwamba kusema uongo haionekani kama ni tatizo katika nchi ya Tanzania. Uongo ulianza kama mazoea na sasa kusema uongo imekuwa ni tabia. Kwa hiyo shishangii hao wanaojiita CCM - NAPE, BAVICHA au wanachama wa chadema kumtuhumu Dr Slaa ambaye ameonesha uungwana (honesty) na uwazi wa kusema kadi ya ccm anayo lakini hajasema anailipia au bado ni mwanachama wa ccm, na kwa kauli na matendo yake ni dhahiri si mwanaccm. Hivi wanandoa wakitarakiana iwe kimila au kiserikali huwa wanarudisha vyeti vyao vya ndoa walikofungia - iwe kwa sheikh/msikitini, kwa padri/mchungaji/kanisani? Au kila mmoja anaamua atakavyo apende kukichoma moto cheti cha ndoa au kuki-ignore tu, au kiwe kumbukumbu kwamba naye alipata kufunga ndoa? Au misikiti, makanisa au serikali (mahakama) huwataka watarakiana kurudisha vyeti vilivyokuwa vya ndoa ktk mamlaka husika? Je hivi ndoa inapimwa kwa vyeti au matendo? Je hivi uanachama wa kisiasa unatambulishwa kwa kadi au matendo? Hivi ilikuwaje Dr Slaa akawa mbunge kupitia cdm kwa miaka 15 pasipo ccm kusema lolote? Je masharti ya chama au society yoyote ni pamoja na kulipia kadi, kuhudhuria vikao kadhaa etc ili uwe active member? Sisi ambao tulilazimishwa kuwa na kadi za ccm wakati wa mfumo wa chama kimoja na baada ya vyama vingi hatukuambiwa kurudisha kadi lakini hatuzilipii bado Nape unatuita wanachama wako, hata kama kimatendo tunapingana na sera za kulindana na rushwa ndani ya ccm? Mbona ccm huwa wanawazuia wanachama kupiga kura katika kura za maoni ndani ya ccm kama hawana kadi hata kama majina yao yamo kwenye daftari la wanachama? Inanitia shaka sana kama Nape na serikali yake ya ccm wapo tayari kuacha kusema uongo katika maswala yenye maslahi ya taifa au katika utekelezaji wa sera zao pamoja na kushindwa kwa sera za ccm kutotekelezeka. Kwa kauli ya Nape ndiyo maana baadhi ya wasiojua siasa wanasema 'siasa ni uongo' na hii ni tafsiri ya nchi zisizopenda kuwapa mwanga wananchi wake, mbali na kuendelea kuwapumbaza ili waendelee kuwatawala kupitia gonjwa/radhi alilosema nyerere la ujinga.
 
Angekuwa sio mroho wa pesa na msaliti kwa Mungu kama unavyomtetea,nijibu swali moja tu,Kwanini aliiba michango ya pesa za ujio wa Papa Paul ndo maana akakimbia kanisani??
Kaka unauhakika??? mbona mnayumbisha mambo?? Lusinde alisema Dr alifukuzwa kwa kutia mimba masister/wanakwaya, wewe unasema kwa kula michango ya kanisa. Tushike lipi??? angalieni midomo isije ikajaa mate mkiambiwa mthibitishe maneno yenu.
 
Wewe unafikiri watu hawalali juu yake kwa sababu gani, mara sijui padri mara sijui ana kadi, mara sijui nini, kitaeleweka tu.
Mimi nawashangaa wanaohangaika kujibu tuhuma za kijinga zenye lengo la kuupoteza mwelekeo wa watanzania. Kitendo kilichofanywa na Nape kwa maelekezo ya kitengo chao cha propaganda nakiona kama tusi kwa watanzania ambao wana hoja nyingi muhimu kuhusu mustakhabali wa maisha yao.
Nashindwa kabisa kuelewa jinsi watu wenye akili zao kuhangaika na mjadala wa karatasi ambalo halina tija kwa mmiliki halali (Dr. Slaa) wala nchi ambayo kwa sasa iko katika harakati za kujinasua na utawala mbovu kabisa katika historia ya nchi yetu.
Kwa kweli kitendo hiki kinachoshabikiwa sana na wafuasi wa CCM kitawaathiri sana baada ya wtanzania kutafakari kwa kina. Ni sawa na kutuchorea mlango ukutani na kutushawishi tutokee penye picha! Watanzania si mazezeta kama CCM inavyodhani, muda si mrefu watagundua wamepotezewa muda na kwamba ule si mlango bali picha tu! Wakibaini hivyo, patachimbika.
 
Mwanasiasa mahiri ni yule anayetumia muda wake wote kuonesha Watanzania namna ya kuondoa Ujinga, maradhi, umaskini na Ufisadi.

Akitoka nje ya hayo, huyo ni mbabaishaji.
 
Katika Nchi hii na pengine hata nchi nyingine sijawahi kumwona au kumsikia kiongozi wa kisiasa anayetajwa mambo yake mengi hadharani kama Dr. Slaa.

Wapinzani wake wana/wamemwongelea sana mambo yake mengine hadi ya ndani ya zipu lakini Babu amehilimi na kukabiliana nayo vizuri kabisa. Kwahiyo hata hizi propaganda za sasa nina uhakika Dr. Slaa atazishinda.

Kwasababu anajua uwezo wa kufikiri na kutenda na hata mbinu za wapinzani wake. Sina shaka kabisa na hili. Na huu unaweza kuwa mmoja ya mipango ambayo mtu mmoja aliiandika...

Kwamba ili CCM iendelee kuongoza ni:
1. Au wakiue CHADEMA
2. Au Wakiue CCM na kuanzisha chama kingine
3. Watumie Demokrasia.

Hili la kwanza lilipewa kipaumbele sana. LAKINI KWA TAARIFA YENU (MAGAMBA) HAMTAWEZA HATA KIDOGO. Uwezo wa Dr. Unaweza kuwa sawa au hata zaidi ya Sekretariati nzima ya CCM.
Malova hahaha kumbe umekiri Slaa ni KABABU hahahaha na ni hapa Tanzania tu utakuta BABU amabaye hajawai kuoa na mpaka sasa yuko na Girlfriend ambaye alikuwa mke wa mtu akambuiba its Strange....
 
Last edited by a moderator:
Nape..acha uchoko. Bado kijana mdogo sana wewe. Unaweza kuacha na ukawa kijana wa kawaida.
 
soma hapa hapa ukimaliza huandika tena hiki unachoandika hapa. hivi mpaka leo hii hujui kuwa josephine walishapeana talaka na mume wake wa kwanza? naona unachukulia ndoa kama tukio na siyo kama taasisi...
http://www.ruthinstitute.org/ITAF12/faculty/readings/marriageInstitution.pdf

Nimesoma na nimeona niquote baadhi ya maneno kutoka kwenye hiyo link:

'It is irrelevant whether or
not the couple is married or common-law, Catholic or Muslim, or share the output
of their union or have one party hired by a wage.Whatever the optimal outcome is, is independent of
the rules under which the trade and production takes place, because everyone in the
model operates in a friction less environment.'

Hizi neo - classical theories si za kutumiwa na mtu kama DR Slaa ambaye doctrate yake ni katika falsafa ya dini chini ya kanisa katoliki. Haki na sheria za kanisa ilibidi zitumike kumuongoza sio kumfuata Douglas Allen ambaye anaongozwa na akili zake badala ya maandiko kutoka kwa mungu. DR Slaa alipotoka na inabidi atubu na kumuomba radhi mume wa huyo dada Josephine kwa kumpora isivyo halali kwa kutmia influence na pesa alizonazo. Ni hatari sana.
 
Slaa ni homa kwa CCM, kumpaka matope, kumtukana, kumzulia uongo na fitina juu yake hakutaisaidia CCM, dawa ni moja tu kwa CCM, kuacha ufisadi,kutowakumbatia mafisadi, kujali wananchi kwa kutekeleza ahadi zao ipasavyo hiyo ndio salama ya CCM.Haya mambo ya kadi, sijui mke wa mtu, sijui babu huo ni woga na CCM ya leo haina tofauti na Mbwa koko, wala haitutishi tena, popote kwenye mechi (uchaguzi) tunaingia nao uwanjani pamoja na kwamba wanashinda kwa kubebwa lakini wakitoka wanasimuliana hali ilivyokuwa ngumu.
Magonjwa ya magamba ni kama kansa ya damu katika mwili, hakuna unachoweza kurekebisha kuiokoa ccm yaani kama ni mgonjwa dactari alisharuhusu wanandugu wamchukue wakamuuguze nyumbani
 
Malova hahaha kumbe umekiri Slaa ni KABABU hahahaha na ni hapa Tanzania tu utakuta BABU amabaye hajawai kuoa na mpaka sasa yuko na Girlfriend ambaye alikuwa mke wa mtu akambuiba its Strange....

Tanzania itakombolewa na wenye moyo wa kunitolea, ambao wapo tayari hata ku sacrifice maisha yao kwa ajili ya ukombozi wa wanyonge.
endeleeni kujadili maisha binafsi ya watu........ huku siw tunakata mbuga kuelekea kwenye ukombozi wa fikra.
pumba zenu hazijawahi kuwasaidia
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom