Dr. Slaa akabidhi msaada wa CHADEMA kwa waathirika Kahama

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Wilbroad Slaa amelakiwa kwa kishindo na wananchi wa Mwakata-Kahama waliopatwa na maafa wiki iliyopita.

Mara baada ya kuwasili Dk. Slaa amewasilisha mchango wa CHADEMA kwa Kamati ya Maafa kwa ajili ya waathirika hao.

Mchango huo ni bundle 50 za mabati, BUNDLE ina mabati 16 ya gage 30 kwa gharama ya 12.5M.

Akitoa pole kwa umati wa wananchi wa kijiji hicho Dr Slaa amewaambia chama chao cha CHADEMA ambacho ndicho kinaongoza serikali ya kijiji hicho kipo nao bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu.

Baadae mchana kiongozi huyo atakuwa na mkutano wa hadhara Isaka, Jimbo la Msalala.

Katibu Mkuu atapata fursa ya kutoa shukrani kwa wananchi wa Kanda ya Serengeti (zamani Ziwa Mashariki) kwa namna walivyoipatia heshima kubwa CHADEMA na kuonesha kuwa wana matumaini makubwa na chama hiki.

Kanda hii ndiyo iliyoongoza miongoni mwa kanda 8 za Tanganyika wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kupata asilimia 48 ya kura za mitaa, vijiji na vitongoji vyote katika mikoa ya Mara, Simiyu na Shinyanga.
 
Mungu aendelee kumtunza huyu Kamanda wetu mkuu na kumwepusha na hila Mbaya za watoa roho za watu.

Hakika ukombozi wa kweli sasa haupo mbali
 
Afya yake vipi? Angeisikilizia kwanza.
 
Attachments

  • 1426336849258.jpg
    1426336849258.jpg
    98.6 KB · Views: 2,038

Katibu Mkuu atapata fursa ya kutoa shukrani kwa wananchi wa Kanda ya Serengeti (zamani Ziwa Mashariki) kwa namna walivyoipatia heshima kubwa CHADEMA na kuonesha kuwa wana matumaini makubwa na chama hiki.

Kanda hii ndiyo iliyoongoza miongoni mwa kanda 8 za Tanganyika wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kupata asilimia 48 ya kura za mitaa, vijiji na vitongoji vyote katika mikoa ya Mara, Simiyu na Shinyanga.
 
Na watakaokuja na hila mbaya cdm mungu awahukumu kwa hila zao Mungu ibariki cdm ipatie viongozi watakaotekeleza ahadi wanazotoa majukwaani
 
Hakika huyu ndiye rais wetu atakayeliokoa taiga letu dhidi ya haya mafisadi ya ccm
 
Katibu Mkuu atapata fursa ya kutoa shukrani kwa wananchi wa Kanda ya Serengeti (zamani Ziwa Mashariki) kwa namna walivyoipatia heshima kubwa CHADEMA na kuonesha kuwa wana matumaini makubwa na chama hiki.

Kanda hii ndiyo iliyoongoza miongoni mwa kanda 8 za Tanganyika wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kupata asilimia 48 ya kura za mitaa, vijiji na vitongoji vyote katika mikoa ya Mara, Simiyu na Shinyanga.
Hakuna binadamu atakayeweza shindana na nguvu ya Mungu. Chadema ni nguvu ya Mungu
 
Kamanda Molemo tunaomba utupie kapicha ili story inoge.Mimi penda sana chama dume cdm
 
Back
Top Bottom