Dr. Slaa aikalia kooni serikali ufisadi wa Fedha za ESCROW

Dr. Slaa aikalia kooni serikali ufisadi wa Fedha za ESCROW

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa amevunja ukimya na kuitaka serikali iache porojo kuhusu ufisadi mkubwa wa Fedha Escrow.

Dr Slaa ambaye kwa sasa ndiye kiongozi mashuhuri zaidi wa upinzani nchini ametaka hatua za haraka kuchukuliwa kuhusu wizi huo ikiwemo kukamata wahusika wote na kuwafungulia mashtaka.

Kiongozi huyo tishio kuu kwa chama tawala amesema serikali imekosa uwajibikaji kwa kuendelea kunyamazia wizi huo huku wahalifu wa hujuma hiyo wakilindwa.

Soma pia: Uzi maalum wenye matukio yote yaliyojiri kwenye sakata la ufisadi wa ESCROW

Kutolea kauli suala hili kwa Dr Slaa kunafanya sakata hili kuchukua sura mpya zaidi ikikumbukwa jinsi Kiongozi huyu alivyosimamia kidete suala la wizi wa Fedha za EPA mpaka ikalazimu Rais kuingilia kati na kuunda tume maalum kuhusu suala hilo.

Source:Tanzania Daima
 
ndani ya ccm hakuna wa kumfunga kengele mwenzake maana wote majambazi na wengine wauza sembe, majangili.....
 
Escrow ni dili na wizi uliofanywa kwa kushirikiana na serikali,
Kamwe Serikali haiwezi kujikamata.

Yaani mfano DPP hawezi kutoa maamuzi AG akamatwe, sio kwa Tanzania kaka Molemo!!
 
Last edited by a moderator:
Kwa mujibu wa barua za mwanasheria mkuu wa serikali kwenda kwa Governor wa BOT, barua ya wizara ya nishati na madini kwenda kwa Governor wa BOT na barua ya TRA kwenda kwa Katibu mkuu hazina ni dhahiri kuwa Werema, Maswi, waziri wa fedha na Tanesco walicheza deal ili kuiba fedha kutoka escrow account kwahiyo lazima wawajibishwe.
 
Hapo kazi ipo kwa huyu raisi ajaye kuamua kuingilia huu wizi wa serikali ya c.c.m lumumba lazima watapike kila walichokula.
Thanks our next president dk.w.p.slaa.
 
Hapa sasa ndo nategemea kumuona JK anachukua hatua, this instruction has come lately though.
 
Asante Dr. Huko intarahamwe nimajanga wezi wauza pembe watu nikulindana tu nakuacha watanganyika hawana lakufanya
 
Huyu naye mabaki anatupigia kelele tu bora anayamaze kabisa anatia aibu tu.
 
haya mambo ya Escrow ni mbwa kala dog yan mbwa kamwe hawezi mshitak dog mana anajua tofaut ni jina kwa Kizung lakin mind zao ziko sawa sawa
 
Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa amevunja ukimya na kuitaka serikali iache porojo kuhusu ufisadi mkubwa wa Fedha Escrow.

Dr Slaa ambaye kwa sasa ndiye kiongozi mashuhuri zaidi wa upinzani nchini ametaka hatua za haraka kuchukuliwa kuhusu wizi huo ikiwemo kukamata wahusika wote na kuwafungulia mashtaka.

Kiongozi huyo tishio kuu kwa chama tawala amesema serikali imekosa uwajibikaji kwa kuendelea kunyamazia wizi huo huku wahalifu wa hujuma hiyo wakilindwa.

Source:Tanzania Daima

angalia source ndio utoe mawazo yako
 
Huyu Mzee hana credibility ya kuongelea ufisadi, kwani takwimu zinaonyesha kuwa naye ni fisadi wa aina yake.
 
Escrow ni dili na wizi uliofanywa kwa kushirikiana na serikali,
Kamwe Serikali haiwezi kujikamata.

Yaani mfano DPP hawezi kutoa maamuzi AG akamatwe, sio kwa Tanzania kaka Molemo!!

Duh!! Inasikitisha sana.Hatufiki mbali kama Taifa kwa hali hii.
 
Last edited by a moderator:
Huyu Mzee hana credibility ya kuongelea ufisadi, kwani takwimu zinaonyesha kuwa naye ni fisadi wa aina yake.

Yaani kama yale matumizi ya kifisadi ya Bil 10 points something angeyaongelea data kwa data na ufafanuzi makini kwa public angekuwa na uwezo mkubwa wa kuuambia mti wa ufisadi ng'oka na ukang'okaa na Dunia ingemgeshimu sana
 
Huyu naye mabaki anatupigia kelele tu bora anayamaze kabisa anatia aibu tu.

kama hizi buku 7 mnazopewa ni za huu wizi wa escrow jiandaeni kunyea debe wapuuzi nyie!
 
Hapo kazi ipo kwa huyu raisi ajaye kuamua kuingilia huu wizi wa serikali ya c.c.m lumumba lazima watapike kila walichokula.
Thanks our next president dk.w.p.slaa.

Tuzidi kumuomba Mungu tupate Rais atakayelisimamia vyema hili jambo
 
Yaani kama yale matumizi ya kifisadi ya Bil 10 points something angeyaongelea data kwa data na ufafanuzi makini kwa public angekuwa na uwezo mkubwa wa kuuambia mti wa ufisadi ng'oka na ukang'okaa na Dunia ingemgeshimu sana

endea kujifariji,hapo lumumba team haichomoki.Rudisheni pesa tu na muombe msamaha tuwasamehe!
 
Back
Top Bottom