Dr. Shein ni dhaifu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Shein ni dhaifu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 23, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Unaonaje jinsi ambavyo Mwanasheria wake Mkuu anavyosimama hadharani kuukana Muungano na bado Shein amemwacha kwenye nafasi yake? Shein ambaye aliwahi kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ameweza vipi kuwa na Mwanasheria Mkuu anayepinga Muungano?

  Go figure!
   
 2. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  Mkuu MM,kwa kifupi kabisa Dr.Shein ndio mtu wa kwanza ambaye hautaki Muungano kule Zanzibar.Ila anajifichaficha.Hujiulizi kwanini harakati za kuukataa zimepamba moto chini ya utawala wake?
   
 3. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Ni dhaifu kwa TANZANIA ila ni imara kwa ZANZIBAR....naye hautaki muungano
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,321
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  Si wauvunje tu tujue moja?
   
 5. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #5
  Jul 23, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mbona jibu liko wazi kabisa. Ni kwamba naye hautaki muungano ila hajaamua kutamka kwa kinywa chake. Anawatumia wengine kufikisha ujumbe.
   
 6. Keren_Happuch

  Keren_Happuch JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 1,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hiyo inaonyesha yeye kama Dr. Shein, Muungano hautaki. Lakini kwa kuwa ni Rais wa Zanzibar, na ameupata urais chini Muungano, anashindwa kuweka wazi nini anatamani yeye Dr Shein na sio Rais!
   
 7. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 4,035
  Likes Received: 1,156
  Trophy Points: 280
  ..shein katoka pemba...seif..katoka pemba..sheikh farid (kiongozi uamsho)..toka pemba..kuna nani tena hapoooo..?
   
 8. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  wakuu...Kwani Dr. Shen aliapa kwa kutumia katiba ipi?
  alitumia kibwagizo kipi? ntailinda na kuitetea katiba ya....
   
 9. k

  kubenafrank Member

  #9
  Jul 23, 2012
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndiyo,Shein kama alivyo Kikwete wote ni dhaifu
   
 10. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Muungano wetu ulitokana na siasa za kijamaa na ki-socialist na leo hii nchi zilizojiunga huko ulay kamvile USSR, UJERUMANI MASHARIKI HAZIPO TENA .
  Watanganyika msishangaae kuvunjika muungano wetu kwani wenzetu tuliofanana nao tayari washamalizana, HAYO NDIYO MYATARAJIE.Kuanza kumlaumu shein haitawasaidia ni kwamba kila kitu kinazaliwa kinakua na kinakufa.Muungano pamoja na chama chake CCM LAZIMA VIONDOKE KABLA YA 2015.
   
 11. W

  WildCard JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Mwanakijiji,
  Dr Shein utakuwa unamwonea tu. Taratibu za kutoitumia Katiba ya JMT kule Zanzibar zilipamba moto baada ya Mwalimu kuondoka madarakani. Zikakolezwa zaidi waliomwita "Commando" wao Dr Salmini Amour baada ya kupata nguvu za ziada alipomsaidia Mkapa kuingia madarakani mwaka 1995. Amani Karume akalinogesha zaidi kwa kuamua kuirudisha Zanzibar Ujombani. Hapa ndipo alipoikuta Zanzibar huyu Dr Shein ambaye wala sio mwanaSIASA na cheo chenyewe alisukumiwa tu ili kumpata Rais MPEMBA. Dr Shein hana la kufanya. Yuko pale madarakani kama vile vikatuni tunavyofunga kwenye mashamba ya mpunga!
  Tunaweza tukachelewesha kuuvunja Muungano huu, lakini hatimaye utavunjika tu. Mbaya zaidi hata Rais wa JMT hailindi na kuitetea KATIBA ya JMT. CCM nayo haina habari na kinachoendelea Zanzibar. Enzi za Mwalimu ni NEC ya CCM ilikuwa inayamaliza haya kirahisi kabisa kwa kuwa Rais wa Zanzibar anateuliwa na NEC ya CCM.
   
 12. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #12
  Jul 23, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,945
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  MM naomba niseme hivi hakuna mtu yeyote nayetokea Tz visiwani anayeutaka huu muungano na nafikiri sisi wabara ndio tunawapapatikia tu ila kiukweli hawautak na viongozi wao wapo kiunafiki tu. ila ifike mhali wabara jujiulize hata kama huu muungano upo kwa heshima tu ila kiukweli hauna faida yeyote kiuchumi wala kijamii why do we need it?

  kwani wabara tunapata nini kutoka kwao? hivi tunatukanwa sisi na kuonyeshewa vidole kana kwamba sisi ni mbwa ama mipaka koko tu and then tunavumilia, tunavumilia kitu gani? nakubaliana kabisa na ndahani kwamba tuuvunje tuish kwa amani.

  tukumbuke kwamba sisi wat wa bara siyo asili yetu kubaguana ila wenzetu wanzanzibar ni wabaguzi sana si tu wa dini ,bali hata wa rangi na hata makabila na nyerere alishawah kuliona hili siku nyingi sana.
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  Jul 23, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,307
  Trophy Points: 280
  Dr. Shein sio dhaifu, yeye ni mtu mkimya, makini na mtulivu asiye na papara!. Kwa huu ni wakati wa mchakato wa maoni ya katiba mpya, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, yuko right kutoa maoni yoyote kuhusu uwezekano wa kuuvunja muungano!.

  Nilipoyasoma yale makubaliano ya Muungano, niliwahi kutamka humu kuwa makubaliano yale, hayana sifa ya kuitwa mkataba kwa sababu hayakuweka kipengele cha namna ya kuuvunja muungano!. Mkataba wowote halali kisheria, lazima uwe na kipengele cha namna ya kuuvunja!. Makubaliano ya muungano hayana kipengele cha kuuvunja, huo ni udhaifu mkubwa uliovumiliwa kwa kipindi kirefu bila kuhojiwa!.

  Katiba ya JMT inazungumzia kuwa hoja yoyote ya kuhusu kuuvunja muungano ni kosa la uhaini!. Zanzibar ina katiba yake na haisemi hivyo!. Dhaifu ni yule aliyiachia Zanzibar kupitisha katiba yenye vifungu vinavyokinzana na katiba ya JMT, na ilisemwa wazi, kunapotokea ukinzani wowote baina ya katiba hizi mbili, katiba ya JMT ndio ita prevail, kwa vile alichosema Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar sio kinyume cha Katiba ya Zanzibar, Dr. Shein hana sababu yoyote ya kumwajibisha, bali mwenye jukumu la kumwajibisha, ni yule aliyeapa kuilinda katiba ya JMT ambayo ndiyo iliyokiukwa!.

  Ikumbukwe, Kila Mzanzibar, kwanza ni Mzanzibari, kisha ndio Mtanzania, hivyo kama hajavunja sheria yoyote kwa Uzanzibari wake, na badala yake, amevunja sheria ya Utanzania, anatakiwa kuwajibishwa kwa uvunjaji sheria ya Tanzania!.

  Tena kutokana na ukimya huu wa Dr. Shein, umakini wake na utulivu wake, huyu ni mtu asiyefaa kabisa kuwa mgombea wa CCM kwa mwaka 2015 kwa sababu ni hatari kwa mustakabali wa ule ukombozi wa pili wa Mtanzania!
   
Loading...